Ifike wakati idadi ya kusajili wachezaji kumi tu wa kigeni itenguliwe

Ifike wakati idadi ya kusajili wachezaji kumi tu wa kigeni itenguliwe

change formula

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2020
Posts
729
Reaction score
1,559
Kwanza niipongeze TFF hii ya Wallace Karia, imefanya kazi kubwa sana licha ya mapungufu yaliyojitokeza katika uongozi wake ambayo ni machache na yanatokea kutokana na uelewa finyu wa watanzania walio wengi kuhusu mpira wa miguu na wengi kuendekeza ushabiki wa u-Simba na u-Yanga.

Kutokana na ligi kuu ya Tanzania kuzidi kukua na kuvuta mashabiki kutoka pande zote za jamhuri ya muungano wa Tanzania, mimi kama mdau wa michezo na mtaalamu wa masuala ya pesa na uwekezaji, napendekeza mambo yafuatayo.
Moja Tff ibadilishe kanuni za usajili ili timu zenye uwezo ziruhusiwe kusajili idadi zaidi ya kumi ya wachezaji wa kigeni ili kuongeza ushindani katika ligi yetu.

Itazisaidia timu zinazocheza mashindano ya kimataifa ziweze kufika mbali zaidi na kuitangaza nchi yetu, pia zitapata pesa nyingi ambazo zitasaidia kuboresha timu na hata wawekezaji kupata faida.

Pili kama hilo haliwezekani basi wachezaji wanaotoka E.A community wasiesabiwe kama wageni, hii itasaidia wachezaji wa nchi za Africa Mashariki kuja kwa wingi kwenye ligi yetu na ligi yetu itatangazika na kutazamwa zaidi kwenye nchi za afrika Mashariki.

Najua wapo watu wanasema wachezaji wa kigeni wakiwa wengi tutakosa wachezaji wa timu ya Taifa na Taifa stars itakuwa dhaifu!!! Hoja hii haina mashiko, wachezaji wa kigeni wakiwa wengi hii itasaidia wachezaji wazawa kujitambua na kujituma zaidi ili wafanye vizuri na kupata number na hii itakuwa ndio njia nzuri ya kuwajengea confidence ya kupambana na watu kutoka mataifa mbalimbali, wakizoea watafanya vizuri na timu ya taifa itafanya vizuri pia.
 
Mimi naona hiyo idadi ibakie hapo hapo! Au ikibidi wapunguzwe tu mpaka wachezaji watano au saba, ili kuepukana na changamoto ya sasa ya kusajili wachezaji wa kawaida.
 
Sikupingi lakini mimi kwa mawazo yangu natamani idadi iongezeke sana hata wakiweka idadi ya 20 sawa tu lakini kipengele kiwe kwa mechi moja.

Idadi ya wachezaji wa kigeni kwa mechi ya ligi kuu iwe 5 tu watatu wanaanza wawili wansubiri benchi hii itasaidia wachezaji wetu wajitume zaidi kwa maana ukizingua tu mtu yupo mgeni wa kucheza namba yako.
 
Mimi naona hiyo idadi ibakie hapo hapo! Au ikibidi wapunguzwe tu mpaka wachezaji watano au saba, ili kuepukana na changamoto ya sasa ya kusajili wachezaji wa kawaida.
Wachezaji wengi wa ligi za ndani hapa Africa hawatofautiani sana viwango, changamoto ipo kwa wachezaji wetu wa kitanzania ni wavivu sana na wanaridhika mapema, wakifika Simba na Yanga basi wanajiona wamefika kwenye kilele cha career yao.

Wachezaji wa kigeni wakija hata kama ni wa kawaida kama unavyosema watawaamsha wazawa watoke kwenye lindi la uzembe na uvivu.
 
Sikupingi lakini mm kwa mawazo yangu natamani idadi iongezeke Sana hata wakiweka idadi ya 20 sawa tu lakini kipengele kiwe kwa mechi moja. Idadi ya wachezaji wakigeni kwa mechi ya ligi kuu iwe 5 tu watatu wanaanza wawili wansubiri benchi hii itasaidia wachezaji wetu wajitume zaidi kwamaana ukizingua tu mtu yupo mgeni wa kucheza namba yako
Wacheze tu, wachezaji wetu wengi hawajitambui, mfano tu, tunasikia habari za kina Mkude, sijui Ajibu, Nchimbi na dizaini ya hao hawajielewi wala kujituma, wakikosa timu kubwa wakarudi kucheza timu ndogo na kipato kikapungua watajifunza na watajituma ili warudi timu za juu
 
Sikupingi lakini mm kwa mawazo yangu natamani idadi iongezeke Sana hata wakiweka idadi ya 20 sawa tu lakini kipengele kiwe kwa mechi moja. Idadi ya wachezaji wakigeni kwa mechi ya ligi kuu iwe 5 tu watatu wanaanza wawili wansubiri benchi hii itasaidia wachezaji wetu wajitume zaidi kwamaana ukizingua tu mtu yupo mgeni wa kucheza namba yako
Hii model sisi tumeitoa wapi kwamba wachezaji wetu lazima wacheze? Hapo nyuma ligi yetu ulikuwa na wazawa wengi na wanacheza lakini hatujawahi kufanya vizuri. Chukulia mfano EPL anasajiliwa anayejua na anacheza anayejua, saizi Uingereza imezalisha vijana wengi ambao wamepambania namba kwenye vilabu vyao, sio kwa sababu ya sheria Bali kwa uwezo wake, chama akae nje na ajibu acheza eti kisa sheria inataka acheze, Ridiculous. Tutakua tunaviumiza vilabu na mpira wa nchi yetu, kwa sababu tutakua tunakumbatia wajinga
 
Nimesikia leo kocha wa utopolo akilalamika kwa nininwasiruhusiwe hata wachezaji 10 wa kigeni katika mechi moja.

Mie nadhani wangeacha tu, hata wawe wote 11 pamoja na akiba.
 
Hii sheria ni upuuzi na aliyeitunga ni mpumbavu, na nikimuona nitampiga makonzi.....
Wabongo wangekuwa wanajitambua wangepata tu namba, Kwanini wazawa wengine wanapata namba ila hao wengine mpaka tuwasukume kama walevi kwa sheria zinazowabeba.
Saiv Duniani huko Uingereza ni sehemu ambayo vipaji vimejaa. Wanauwezo wa kutengeneza vikosi viwili na vyote vikafika fainali.
Je na wenyewe wana sheria za kijinga kama hizi?
Ni soko huria anayejua na acheze, sisi badala ya kutengeneza wanaojua tunafukuza wanaojua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom