Ifikie mahali utawala uliopo madarakani utambue haya

Ifikie mahali utawala uliopo madarakani utambue haya

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
1. Lengo la kukabidhiwa dola sio kufanya maisha yetu kuwa magumu kwa makusudi.

2. Hii nchi ni yetu sote, kuwa katika nafasi mlizopo ni kwa mchango mkubwa wa raia ambao mmeamua kuwafanya wanyonge makusudi.

Kweli muamue tu kuvuruga mitandao ya simu kwa kuwa mmejiskia tu kuumiza raia? Raisi wetu Mama Samia naamini una uelewa wa kutosha juu ya maisha kwa ujumla.

Mtandao ni kitu essential kwa maisha ya raia wako na ni sehemu pekee ambako tunapata mambo mengi ikiwamo habari, elimu na burudani.

Kitu kilichofanyika leo hakipendezi duniani wala mbinguni tuoneane huruma jamani maana wengine hujipatia riziki kupitia mauzo ya bidhaa mitandaoni. Ghafla tunapandishiana gharama kwa bei za kukomoana.

Haipendezi na mambo kama haya ndio hupelekea watu kujenga chuki na serikali iliopo madarakani bila sababu za msingi.
 
Nimeamini Watanzania wengi hawafuatilii vitu vinavyoendelea.

Wengi wanadhani vifurushi vya mitandao vimeongezwa leo ghafla bin vuu. Kumbe mchakato ulifanywa tokea mwezi wa pili wakati wa utawala wa Magufuli na utekelezaji wake ulipangwa uanze leo yaani Tarehe 1 April, 2021.

Ndugulile alivyokuwa akipita kwenye vyombo vya Habari kulieleza hili wengi walikuwa busy na umbeya wa Paula na Rayvanny.
 
Viongozi wa Wafrika na wanyonge wao utasikia

"Gharama zimepanda ili watu wafanye kazi''
Mwingine

Ili watu waache kukosoa serikali ndiyo maana tumefunga Twitter
 
Mambo kama haya ndiyo yalikuwa yanampendeza the late

Kuona wengine wakiumia lakini

Mungu amesimama na wengi hicho ndiyo tunaweza kusema

Hatukuwa tena na maamuzi yoyote kwa jambo lolote zaidi ya kungoja itaamuliwa nini na huyo mtu mmoja liwe zuri au baya hatukuwa na uwezo wa kukubali au kukataa

Mungu amesimama katikati ya hili

Kwa yule asiyekuwa na imani hili tu peke yake linatosha kuamini kwamba kuna nguvu ya asili (Mungu )anayesawazisha mambo
Kazi ya wale waliobaki ni kurekebisha makosa yote yaliyofanywa kwa wakati uliopita na maisha yaendelee kwa amani
 
Back
Top Bottom