IGA ni nini na inatofauti gani na HGA (Na mkataba nini na unatofautiana vipi na makubaliano?

IGA ni nini na inatofauti gani na HGA (Na mkataba nini na unatofautiana vipi na makubaliano?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Samahani wadau nawaalika katika huu mjadala wa kuelezea kwa kina juu ya mada tajwa hapo juu inayosema "IGA ni nini na inatofauti gani na HGA (Na mkataba nini na unatofautiana vipi na makubaliano?)

Kumekua na mkanganyiko juu ya hizo terminologies, mwenye kujua maana zake tunaomba ufafanuzi wa kina ili tupate kuelewa.
 
iga inter government agreement, makubaliano ya nchi mbili kushirikiana ama kuwa wamoja kwenye vitu kama kulinda mazingira, kuimarisha usalama, n.k. mfano umoja wa nchi za afrika mashariki tunashirikiana mambo ya usalama, mazingira, n.k. pia NATO ni nchi za ulaya na marekani zinasaidiana mambo ya ulinzi.

Hga - host government agreement, Hga inahusu Nchi flani kuwa na makubaliano na nchi ya nje ije kufanya shughuli zake kwenye ardhi yake, sana sana mambo ya uwekezaji, mfano sisi Tanzania ni Host country tunaruhusu nchi nyingine waje kuwekeza ama kuendeleza mirad, mfano ni hapa kwetu kwa sasa UAE anatajwa kuingia mikataba kibao kuwekeza / kusimamia / kuendeleza mbuga, bandari, misitu, Tanesco, n.k.
 
iga inter government agreement, makubaliano ya nchi mbili kushirikiana ama kuwa wamoja kwenye vitu kama kulinga mazingira, kuimarisha usalama, n.k.

Hga - host government agreement, nchi moja inatoa huduma nyingine inasaidiwa huduma, hii sana sana kwenye uwekezaji kwamba nchi moja inawekeza kwa host country, mfano kwenye huu mkataba wa bandari sisi ndio host
Ahsante
 
iga inter government agreement, makubaliano ya nchi mbili kushirikiana ama kuwa wamoja kwenye vitu kama kulinda mazingira, kuimarisha usalama, n.k...
Kwa suala la uwekezaji kwenye bandari zetu, kama hatuna ushirikiano na Emirate ya Dubai, tungeingia mkataba wa kimataifa wa kibiashara (Bilateral International Agreement BIT) unaotuwezesha nasi kuwekeza huko. Kama upo, kwa nini kuandaa IGA yenye vifungu batili?
 
Kwa suala la uwekezaji kwenye bandari zetu, kama hatuna ushirikiano na Emirate ya Dubai, tungeingia mkataba wa kimataifa wa kibiashara (Bilateral International Agreement BIT) unaotuwezesha nasi kuwekeza huko. Kama upo, kwa nini kuandaa IGA yenye vifungu batili?
Tunapigwa kanzu kwajili ya watu wachache
 
Back
Top Bottom