IGP anatakiwa asichaguliwe na Rais

IGP anatakiwa asichaguliwe na Rais

De-zerbi

Member
Joined
Mar 7, 2024
Posts
82
Reaction score
103
Ukiangalia ishu ya malisa na boniface utagundua tatizo sio polis bali kuna kigogo mmoja anawashurutisha wafanye haya wanauofanya kuwalaumu polisi ni kuwaonea.

Mzizi wa tatizo ni igp kuteuliwa na Rais anakua anafuata matakwa ya Rais na sio tu anafuata matwaka ya Rais bali anafuata matakwa ya chawa wa rais na viongozi wengine wa chama.

Na hii loophole inapelekea polisi kufanya mambo maovu na hakuna atakayewakemea sababu huyo wa kuwakemea ndo huyo huyo mda anawatumia kufanya kazi chafu.

Swali la kujiuliza kama mtu mwenye umaarufu kama boniface anafanyiwa vile vip kuhusu wewe na mimi ambao hatujulikan na nani.

Suluhisho la haya yote ni mchakato wa kuchagua igp usifanywe na rais hii itapelekea igp kutokuwa mtumwa wa wanasiasa kazi ya Rais iwe ni kumwapisha igp tofauti na hapo haya mambo ya hovyo na kuvunja sheria wazi wazi yataendelea.
 
Tanzania katiba yake inampa rais nguvu za ki-mungu mtu. Siyo IGP tu ila kila mhimili, kila idara, kila chombo cha ulinzi, kila kiongozi, kila mtaalam yuko chini ya rais na na anafanya kazi kwa matakwa ya rais. Katiba mpya ndiyo suluhisho na possibly tuwe na serekali yenye kufuata parliamentary system.
 
Mimi siijui nchi ambayo afande mkuu hateuliwi na Rais , embu nisaidie mfano.
 
Hata jaji mkuu hatakiwi kuteuliwa na Rais, Spika wa bunge hatakiwi kuwa kwenye chama ambacho Rais ndo mwenyekiti wake.

Katiba iliyopo nchi ina muhimili mmoja tu mihimili mingine imepewa uhuru wa uongo ila yote ipo kwenye maamuzi ya Rais.
 
Ni kama hao wahalifu wachochezi wanatumwa sijui na nani kufanya upotoshaji, ili wapate sympathy kitu ambacho hakina maana yoyote 🐒

lazima wawajibike, Lazima kushirikiana na polisi kadiri inavyoonekana inafaa. hiyo ya sijui nani ana faa au haifai, sijui anafuata maelekezo kutoka wapi na wapi.

ni maoni na mtazamo wako tu, na ni haki yako. Lakini ile muhimu na yalazima, hao wangwana wapende wasipende, mpende msipepende Lazima wawajibike 🐒
 
Kaka IGP na wateuliwa wote lazima wawe na kadi za chama cha sisiemu.
 
Mimi siijui nchi ambayo afande mkuu hateuliwi na Rais , embu nisaidie mfano.
Nchi zote zenye utawala wa Kidemokrasia, viongozi wengi wateule wa Rais huwa wanapitia Kwanza mchujo mkali kabla Rais mwenyewe hajamtangaza kwa umma. Rais mara nyingi huwa anamuidhinisha tu kufuatana na matakwa ya kisheria, lakini anakuwa hana mamlaka ya moja kwa moja ya kumteua mtu na kumuidhinisha au kumuapisha.Rais huwa analetewa majina au jina moja tu la mtu ambaye ameteuliwa na kupitishwa ktk mamlaka za uteuzi ili amtangaze kwa umma.
 
Hata Tz kitu ni hichohicho Rais analetewa majina yakiwa teyari yashapita kwenye mchujo hawezi akasema mtu yeyote awe IGP kuna vetted list analetewa yeye ndio anateua kupitia hapo.
 
Hata Tz kitu ni hichohicho Rais analetewa majina yakiwa teyari yashapita kwenye mchujo hawezi akasema mtu yeyote awe IGP kuna vetted list analetewa yeye ndio anateua kupitia hapo…
Siyo kweli hata kidogo, hususani kwa nafasi kubwa kama ya cheo cha IGP. Rais mwenyewe kwanza huwa anapendekeza majina kadhaa ya watu anaopenda kuwteua, kisha majina hayo yanapelekwa kwa 'wavaa kaunda suti" kwa akili ya kufanyiwa 'vetting.' Baada ya vetting kukamilika majina hayo yanarudishwa tena kwake yakiwa na maoni au mapendekezo ya wafanya vetting, kisha baadaye Rais ndio huteua jina moja na kulitangaza kwa umma.

Ni kwa wateule wachache sana ambao Rais huletewa tu majina ya watu ambao anatakiwa kuwateua.
 
ni kama hao wahalifu wachochezi wanatumwa sijui na nani kufanya upotoshaji, ili wapate sympathy kitu ambacho hakina maana yoyote 🐒

lazima wawajibike, Lazima kushirikiana na polisi kadiri inavyoonekana inafaa. hiyo ya sijui nani ana faa au haifai, sijui anafuata maelekezo kutoka wapi na wapi.....

ni maoni na mtazamo wako tu, na ni haki yako. Lakini ile muhimu na yalazima, hao wangwana wapende wasipende, mpende msipepende Lazima wawajibike 🐒
Makosa yao yana dhamana kwanini hawapewi dhamana
Unatakakiwa umkamate mtu baada ya kukamilisha upelelezi

Na yule kada wa ccm kule kagera aliyesema atawapoteza/kuwaua wote wanaomsema rais mbona hajaitwa na polisi kuhojiwa
 
Hata jaji mkuu hatakiwi kuteuliwa na Rais, Spika wa bunge hatakiwi kuwa kwenye chama ambacho Rais ndo mwenyekiti wake.
Katiba iliyopo nchi ina muhimili mmoja tu mihimili mingine imepewa uhuru wa uongo ila yote ipo kwenye maamuzi ya Rais
Sio hao hata
Dpp, na jaji mkuu hawatakiwi kuteuliwa na Rais
 
Back
Top Bottom