Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Jeshi la Polisi Tanzania chini ya IGP Wambura limetangaza mabadiliko madogo kwenye safu za uongozi wa Kikosi cha Usalama Barabarani. Katika mabadiliko hayo:
Jeshi la Polisi Tanzania chini ya IGP Wambura limetangaza mabadiliko madogo kwenye safu za uongozi wa Kikosi cha Usalama Barabarani. Katika mabadiliko hayo:
- Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ramadhani Ng’anzi amehamishwa kutoka Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania kwenda Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma. Atakuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Maadili ya Jamii.
- Nafasi yake sasa inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) William Mkonda, aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
- Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Boniphace Mbao, aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, amehamishiwa Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Mkonda kama Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
- ACP Michael Deleli, aliyekuwa Mkuu wa Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma na sasa atakuwa Kaimu Mkuu wa Maadhimisho ya Kitaifa.
- ACP Nassoro Sisiwa, aliyekuwa Mkuu wa Operesheni za Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, amehamishiwa Mkoa wa Kilimanjaro kama Mkuu wa Usalama Barabarani wa Mkoa huo.