Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Ninajua si utamaduni wetu mtu kujihisi hatia na kuamua kujiuzulu. Dhana ya kujiuzulu kwa Tanzania bado inaonekana kama udhaifu. Kwamba hata kama unanuka basi unakomaa tu. Unafia kitini.
Lakini kwa IGP Wambura ni muda muafaka kabisa wa kujiuzulu wadhifa huo ili ubaki kuwa mtu safi. Inakuwaje missions zako za kipolisi zinafeli kwa kutenguliwa na mteuzi wako? Huoni aibu na fedheha kwamba huna weledi?
Twende sawa: ulipowakamsta Slaa na wenzake mkapanga kuwapa kesi ya uhaini. Ikabatilishwa, wakaachiwa baada ya Mama kuagiza kufanya hivyo. Hukujipanga? Leo umemkamata Lissu na wenzake, sitoshangaa ukimwachia maana hutopata kesi ya kumbambikia. Huoni hii ni aibu?
Je, hatimaye Lissu akihutubia Ngorongoro na wewe ukilinda mkutano wake hutoona haya? Baada ya Lissu umepanga kumkamata nani? Naye ataachiwa. Hivi unafanya homework kabla ya kuamua jambo? Ili uwe mweledi jiuzulu usichafuke zaidi.