Kamanda Sirro amekuwa akijinasibu kuhamasisha watu na ulinzi shirikishi. Sirro amekuwa akihimiza kuwa:
"ushirikishwaji watu katika maeneo yao ndiyo njia pekee ya kuumaliza kabisa uhalifu katika maeneo husika."
Kamanda Sirro amekuwa akieleza zaidi kuwa, wahalifu wote wanajulikana katika jamii zao na hata wanafanya nini kwenye uhalifu wao. Kwamba mashirikiano ya karibu baina ya polisi na jamii yatamaliza kabisa uhalifu.
Kisa cha mauaji ya wafanya biashara wa madini wakazi wa Ifakara kwenye kesi maarufu ya Zombe kinayathibitisha maneno mazito haya ya kamanda huyu.
Kwenye kesi hiyo, Rais Kikwete alilazimika kuunda tume ya uchunguzi baada ya wananchi kuikataa ripoti ya polisi kuwa marehemu walikuwa ni majambazi.
Kwa upande wao, jamii ya wananchi waliokuwa wakiishi na marehemu hao (Ifakara na Dar es Salaam) waliikataa katakata taarifa hiyo ya polisi. Tume ya uchunguzi iliuthibitisha ukweli huo wa wananchi dhidi ya uongo, ubambikiziaji kesi, ufedhuli, uuwaji, ujambazi nk wa polisi.
Kamanda Sirro, wananchi tuliokuwa tukiishi na mheshimiwa Mbowe mitaani tunamfahamu. Mbowe anafahamika vyema na majirani zake.
Tambua kuwa katika maneno yako dhidi ya Mbowe na maneno ya Mbowe dhidi yako, Mbowe anaaminika zaidi kuliko wewe.
Kumbuka kamanda wewe na jeshi lako mnafahamika kuwa mu wabambikizia watu kesi mlio sugu. Mheshimiwa Rais Samia ametamka hivyo si mara moja. Kesi kadhaa mlizobambikizia watu zimekuwa zikifutwa hadharani.
Ni yesu au Mungu yupi unayemhusisha na Mbowe leo ambaye hamkuwahi kumhusisha wakati mkiwabambikizia watu kesi?
Kweli wewe utakuwa hujishangai kuwa ndugu, marafiki na majirani zake wanakushangaa wewe na madai yako haya ya ugaidi kumhusu bwana Mbowe?
Kama vile haitoshi umefikia hatua kututisha tusifike mahakamani kinyume cha katiba.
Kamanda Sirro haki zetu kama zilivyo za mheshimiwa Mbowe pia zina thamani.
Tukutane mahakamani.
Tusitishane.