Uchaguzi 2020 IGP Sirro awaonya wanasiasa walioanza kuonesha shari kupitia matamshi na sura zao kuelekea uchaguzi mkuu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Simon Sirro, amewaonya wanasiasa walioanza kuonyesha shari kupitia matamshi na sura zao kuelekea uchaguzi mkuu.

IGP Sirro alizungumzia masuala hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV. Kiongozi huyo wa Jeshi la Polisi aliwataka wanasiasa kutolichokoza jeshi hilo na pia wasililaumu litakapochukua hatua dhidi yao.

“Nimeona viongozi wa siasa wanazungumza mambo makali sana. Ninawaheshimu viongozi wote wa siasa katika ngazi zote lakini lazima sheria na kanuni zilizopo ziheshimiwe.

“Ukiangalia baadhi ya viongozi wanavyozungumza unaona kuna ushari. Ushari wanauonyesha wanaupeleka kwa washabiki wao wawe na ushari huo huo. Wao wanachozungumzia si uchaguzi wa amani na utulivu, sera yao ni ushari,” alisema bila kutaja viongozi wala chama cha siasa.

“Niwaombe sana (viongozi wa siasa) anayetaka kufanya siasa afanye siasa, anayetaka kufanya ushari aache mapema. Unamkuta kiongozi mkubwa anazungumza maneno ya ukali sana, anasahau amepata nafasi ya kuzungumza kutokana na amani iliyopo. Kama siyo amani angekuwa chini ya uvungu wa kitanda chake.

“Sheria na taratibu zimewekwa na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi), habari ya kusema nimeshazungumza nimemaliza basi hakuna wa kuhoji (anamrejelea kiongozi anayezungumza kwa shari), hii siyo lugha nzuri. Watanzania wengi wanapenda amani, hawataki shida…lakini wakumbuke kuna maisha baada ya uchaguzi. Uchaguzi utapita na tutaendelea kuishi tuna watoto na wajukuu, tunataka amani na utulivu,” alisisitiza.

Kwa mujibu wa IGP Sirro, viongozi wanaoanza na ushari wasilaumu vyombo vya dola kwa kuwa Watanzania wanaona kuna jambo wanalitafuta la ushari.

“Kwa kuwa nina dhamana ya ulinzi na usalama, wanaojiandaa kwa ushari wajue sisi tupo kwa mujibu wa sheria, na wanaozivunja sheria, tukianza kuwashughulikia asitulaumu,” alisema.

Sambamba na hilo, IGP alibainisha kwa Tanzania haiwezi kupata viongozi wazuri katika vurugu bali watapatikana kukiwa na amani tele na kwamba ni vyema viongozi hao wakaendelea kunadi sera zao kuliko kutafuta shari.

Aidha, aliwataka vijana kutojiingiza kwenye mambo yanayofanywa (shari) kwa maslahi ya wachache, na kwamba ni vyema wakaangalia familia zao na maisha kwa ujumla.
 
Vijana wa UVCCM wanaotoa matamshi ya hovyo mbona hajawahi hata kuwakemea?
 
Policcm wameshaanza vituko vyao vya kuibeba dubwasha Lao la kijani
He he! Soma aya ya pili kutoka mwisho na yamwisho yenyewe mbona ni ushauri mzuri tu..!
Sasa kiongozi atoe kauli za kuingiza watu barabarani aangaliwe tu..?

Hebu acheni kila chombo kiwajibike kiwezavyo na jinsi kilivyopangiwa na sheria .. sio kila siku lawama tu polisi Kama mnahimizana mihisia ya taharuki basi hicho ndo chombo cha kuwadhibiti siku yakiwashinda wataachiwa JWTZ.. 😅 Sasa hapo ndo mtalalama na kujua ipi mboga ipi ugali... Siasa si uasi.
 
Hivi ikitokea shari halaf lissu akapigwa bangili sijui kama ataweza kutembea
 
He he! Soma aya ya pili kutoka mwisho na yamwisho yenyewe mbona ni ushauri mzuri tu..!
Sasa kiongozi atoe kauli za kuingiza watu barabarani aangaliwe tu..?

Hebu acheni kila chombo kiwajibike kiwezavyo na jinsi kilivyopangiwa na sheria .. sio kila siku lawama tu polisi Kama mnahimizana mihisia ya taharuki basi hicho ndo chombo cha kuwadhibiti siku yakiwashinda wataachiwa JWTZ.. 😅 Sasa hapo ndo mtalalama na kujua ipi mboga ipi ugali... Siasa si uasi.
Anawaingiza barabarani baada ya nini? Atawaingiza barabarani sababu hakuna utaratibu wa kisheria wala wa kikanuni unaoweza kumpatia haki yake itakapoporwa.
Duniani kote ipo hivyo, kama sheria ipo kimya juu ya jambo fulani na mamlaka kama hazitaki sheria hiyo iwepo basi mahakama na majaji huwa ni umma wenyewe.
Na umma huwa mahakama zao ni mabarabarani.
 
Yaaani Lissu anawanyima watu wengi sana usingizi, hahahaha.
Inamaana wao kama jeshi la polisi hawaoni uchafu unaofanyika wakati wa uchaguzi? Sasa tunaamini kuwa wanatumiwa na mbogamboga.
 
Attachments

  • 2322192_tapatalk_1582962316900.jpeg
    2322192_tapatalk_1582962316900.jpeg
    33.1 KB · Views: 1
Police wamekuwa wakitoa matamko ya shari kwa kipindi kirefu. Tumewavumilia sana ila sasa ni zamu yetu.
 
Back
Top Bottom