IGP Sirro: Kinondoni inaongoza kwa uhalifu hapa nchini

IGP Sirro: Kinondoni inaongoza kwa uhalifu hapa nchini

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameutaja mkoa wa Kipolisi wa kinondoni kama kinara wa uhalifu nchini ambapo matukio ya uporaji, uvunjaji wa kutumia nguvu na uporaji kwa kutumia pikipiki yakiwa yameongezeka huku uhalifu mwingine mkubwa wa kutumia silaha za moto ukiwa umeshuka.

IGP Sirro amesema hayo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa, watendaji Kata, pamoja na watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi ambapo amewataka watendaji wote kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha usalama unaendelea kuimarishwa.

Aidha, IGP Sirro ametoa muda wa wiki moja kuhakikisha wanakomesha vya kihalifu kwa kushirikiana na watendaji wengine huku akitoa wito kwa mgambo kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa.

“Tutaendelea kutekeleza wajibu wetu kwa kuzingatia uzalendo, taratibu na kanuni na kuhakikisha maeneo yatu na wananchi tunaowahudumia yanakuwa salama”,amejibu Mohamed Mawal, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta huku Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa Suleiman Masare, akiahidi kutoa pikipiki mpya kwa Kituo cha Polisi Chuo Kikuu itakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi.

Kabla ya kukutana na watendaji wa serikali za mitaa na watendaji wa kata na watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi pia IGP Sirro, alifanya kikao kazi na maofisa na askari wa Jeshi hilo ambapo aliwataka kuendelea kutimiza wajibu wao na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.

Chanzo: Watetezi
 
Kinondoni ni sehemu yalipo makao makuu ya chadema.

Kinondoni ni sehemu yalipo madawa ya kulevya ya kutosha.

Connect dots.
 
Tunamshukuru aliyeleta uzi kwenye jukwaa linalofanana na content
 
Wagezeni Intapol website yao unaweza kumtaja muhalifu..fanyeni hivyo tuwataje wahalifu Kama mzee Mrema alivyofanya enzi zake
 
Kero ya kariakoo sasa hivi ni njia tu basi,
Yaani barabara za lami ni wamachinga wameziba, za vumbi ni malori yameziba,
Lakini majambazi si sanaaaa
 
Basi Kino imebalikiwa sana maana hata Mashoga wako wengi Kindondoni
 
kumbe kinondoni ndio sehemu hatari zaidi Ktk Mkoa wa DSM?!! hatari sana!!
wilaya au eneo linalo fuata kwa uhalifu ni lipi.

nadhani hii ndio mbinu muafaka ya kuwanyuka majambazi, kwanza tubaini wilaya zote zenye uhalifu mkubwa, kisha tarafa, kata na hata mitaa, tukiwabana hivyo naaamini majambazi, wauza madawa ya kulevya, wezi, vibaka na wabakaji watahama Jiji bila kupenda.

Dawa ya majambazi na wauza madawa ya kulevya ni moto tu hakuna kuremba.
 
Kinondoni ndio Wilaya kubwa kuliko zote hivyo lazima mambo kama hayo yawepo
 
Back
Top Bottom