Pre GE2025 IGP Wambura: Polisi tumejipanga vizuri kuelekea Uchaguzi Mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa, IGP Wambura alieleza kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kipekee kutokana na maandalizi madhubuti ya kuhakikisha amani inaendelea kudumu.

Aidha, IGP Wambura aliongeza kuwa hali ya usalama nchini kwa sasa ni shwari, na hakuna matukio ya kuhatarisha usalama yaliyotaarifiwa hivi karibuni.

Ila Tanzania yaani uchaguzi ni wa kiraia ila polisi inaonekana Ndio wapiga Kura😭😭😭😭
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa, IGP Wambura alieleza kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kipekee kutokana na maandalizi madhubuti ya kuhakikisha amani inaendelea kudumu.

Aidha, IGP Wambura aliongeza kuwa hali ya usalama nchini kwa sasa ni shwari, na hakuna matukio ya kuhatarisha usalama yaliyotaarifiwa hivi karibuni.

View attachment 3195542
Tunajua kujipanga kwao ni kushiriki wizi wa kura kukisaidia chama cha mafisadi kiendelee kufisadi nchi.
 
huyu igp ndo mfano wa watumishi mazuzu, eti tume jipanga kwa ajili ya uchaguzi.

kwanini msi jipange kuchunguza na kujibu tuhuma, kuhusu watu wanao uliwa na kutekwa nchini??.
Hivi waandishi wa habari hawaulizi ripoti ya uchunguzi wa mzee Ali Kibao au wanaogopa kuuliza?
 
Huyu IP ni mjinga. Badala ya kuongelewa matukio ya usalama wa watu ya kutekwa, kupotezwa na kuuliwa, anatoa kauli za kinafiki akijua kuwa wanafiki wa madaraka, watamsifu wakiona ameongelea uchaguzi!!
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa, IGP Wambura alieleza kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kipekee kutokana na maandalizi madhubuti ya kuhakikisha amani inaendelea kudumu.

Aidha, IGP Wambura aliongeza kuwa hali ya usalama nchini kwa sasa ni shwari, na hakuna matukio ya kuhatarisha usalama yaliyotaarifiwa hivi karibuni.

View attachment 3195542
 
Attachments

  • 5929282-43d7e58f930fba84b8de7085be6f9086.mp4
    19.9 MB
Back
Top Bottom