DOKEZO IGP Wambura tunaomba ingilia Kati hili linaloendelea kwenye hiki Kituo cha Polisi Tabata Relini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yye mwenyewe ni mchafu unafikili atawakamata wachafu wenzake? Hawezi na hatoweza
 
Sasa Faini ya Bajaji ni Elfu kumi, halafu uombwe tena rushwa ya elfu kumi.Wewe sema wamekuandikia tu hao.
Madereva waende Driving School,ili wasijifiche kwenye kichaka cha kupewa elimu. Kama mtu umekosea pigwa Faini au uende Mahakamani tu.

Njooni Shambani tulime huku hakuna traffic kusimamisha jembe wala shamba lako
 
Habari ya stika ni kero sana hivi sasa, stika zinafichwa ili ziuzwe kwa bei juu na wahuni
 
Wapi nimesema Faini alipiga Bajaji pekee,Wewe Ziwa Jipe ni mmojawao au mfanya hayo mambo sehemu nyingine ndiyo maana unakuja mbio kuropoka kwa akili za tumbo bila kusoma mada kwa makini na kuelewa.
 
Kwa trafiki mbona ndo tabia yao.kila mkoa hali iko hivyo.Ni mwamba JPM tu ndiye aliyewapunguza makali lkn kwa sasa mambo yamerudi kule kule.trafiki alisimamisha gari yoyote dereva anasimama mbali kidogo na hawa jamaa halafu anateremka kuwafuata na kuwapa kitu kidogo na safari inaendelea.siku moja nilimwuliza dereva kwa nini unasimamisha gari mbali halafu unawafuata na kwa nn asije yeye hapa? akacheka na kusema nchi hii ni ngumu sana.
 
Polisi ni majambazi waliovaa sare za serikali ni aibu sana tena sana wandugu police wetu wana njaa mno mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…