Ijue Arusha, Mahoteli, vivutio vya utalii na fursa mbalimbali za biashara vya mkoani humo

Ijue Arusha, Mahoteli, vivutio vya utalii na fursa mbalimbali za biashara vya mkoani humo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Uzi huu ni maalum kwa kuwajulisha Watanzania fursa zilizopo mikoa mbalimbali, hoteli na nyumba za wageni, biashara mbalimbali na vivutio mbalimbali vya utalii.

ARUSHA
Huu ni mkoa uliopo Kaskazini mwa nchi yetu. Ni mkoa ambao ni makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkoa huu umepitiwa na bonde kuu la ufa na umejaaliwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii kama Milima, kwa mfano, Meru, Oldonyo Lengai nk.

Kuna mbuga za wanyama wa kila aina. Ngorongoro ambapo ni eneo la urithi wa Dunia. Ngorongoro ni sehemu pekee ambapo Ni makazi ya wanyapori na binadamu.

Pia Arusha kuna maziwa na mito mbalimbali itiririshayo maji kwa mwaka mzima.

Hali ya hewa ya Arusha ni tulivu, hamna joto kali, kuna mvua za kutosha na kuna shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji zinaendelea.

Arusha ni mahiri kwa uzalishaji wa maua ambayo hupelekwa nje ya nchi yetu, pia kuna kilimo Cha ndizi, maparachichi, buni, mahindi, migomba na mbogamboga mbalimbali.

Arusha kuna muingiliano mkubwa wa watu, wazawa na wageni.

Kuna mahoteli mengi ya kitalii na yasiyo ya kitalii yenye kutoza gharama mbalimbali kutokana na kipato chako.

Arusha ni wafugaji wazuri wa wanyama, hivyo ukitembelea Arusha, usihofu kuhusu wapi utapata nyama choma.

Miongoni mwa sehemu local za nyama choma Ni pamoja na kwa Mromboo.

Ukitembelea Arusha hutojuta.

Arusha ndio baba wa Tanzanite madini pekee ulimwenguni yapatikanayo Tanzania.
 
Emb niambie ni sehemu gani Arusha kuna chimbwa madini ya TANZANITE?

😀ont folo folo me wizout ene bikoz:
Hata kama unadhani unajua sana lakini si vema kukosoa kitu ambacho mleta mada hajakisema. Hakuna aliposema Tanzanite inachimbwa Arusha, amesema Arusha ndiyo baba wa Tanzanite. Ni ukweli ulio wazi mbali ya Tanzanite kuchimbwa Manyara, mishe za masoko na utunzaji/ufichaji unafanyika Arusha na siyo Babati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila ya kusahau, Arusha ndo mkoa unaopokea wageni wengi toka mataifa mbalimbali, ndo maana mpaka mama ntilie huku wanaongea kingereza bila wasi😀😀😀😀
 
Arusha ni mkoa wenye wageni wengi sana kutoka mataifa mbalimbali na wengi wao watalii tatizo la arusha uchafu masoko mengi ni machafu kama kilombero tengeru mbauda mjini penyewe harufu ya kimba kawaida
 
Back
Top Bottom