Ijue bruxism, chanzo na tatizo la kusaga meno/kufunga taya kwa watoto wakiwa wamelala

Ijue bruxism, chanzo na tatizo la kusaga meno/kufunga taya kwa watoto wakiwa wamelala

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Habari JF, leo tutajifunza kidogo kuhusu hili tatizo la watoto kusaga meno .

Bruxism ni neno la kitabibu lenye maana kusaga meno au kufunga taya .Mara nyingi tatizo hili huwapata watoto wakiwa wamelala na ndio muda ambao walezi au wazazi huligundua, tatizo hili huisha kadri mtoto anavyokua.

Sababu za tatizo hili la kusaga meno na kufunga taya ni kama ifuatavyo :-

1.Meno ambayo hayajaunganishwa au kujipang vizuri , hivyo ni vizuri kumuona daktari wa kinywa upatapo mtoto wa aina hii

2.Wasiwasi na hofu , kwa mfano, kutokana na wasiwasi kuhusu mtihani au mabadiliko ya utaratibu shuleni au nyumbani .

3. Maumivu, kama vile maumivu ya sikio au meno

4.Kunyanyaswa ,ukiona mtoto anasaga meno jaribu kumfutilia vizuri anaweza akawa ni muhanga wa kunyanyaswa –angalia mazingira na watu anaoshinda nao tabia zao na wanamtunza kwa namna ipi .Tafiti zinaonesha Bruxism ipo zaidi kwa watoto wanaopitia unyanyasaji kuliko wasiopitia hali hii href="Exploring the Connection Between Domestic Violence and Masticatory Outcomes in the Pediatric Population: A Systematic Review - PMC">Exploring the Connection Between Domestic Violence and Masticatory Outcomes in the Pediatric Population: A Systematic Review - PMC

5.Sababu nyingine kama baadhi ya madawa , baadhi ya watoto wenye shida za ubongo –cerebral palsy ..nk

Madhara yake , tatizo hili mara nyingi, huwasumbua zaidi wanafamilia wengine kwa sababu ya sauti ya kusaga meno .

Lakini wakati mwingine inaweza kusababisha:

--maumivu ya kichwa

--enamel ya jino iliyoharibika au meno kukatika

--maumivu ya uso, sikio, au taya .

Namna ya kuzuia na kumsaidia mtoto mwenye hii shida ,haijalishi ni sababu gani imepelekea bruxism, msaidie mtoto kupumzika(relax) kabla ya kulala - anaweza kuoga kwa maji ya moto, kusikiliza muziki wa utulivu kwa dakika chache , au kusoma kitabu.

Hitimisho , bruxism au tatitzo la kutafuna meno huwa halina madhara sana lakini linaweza kukupa mwanga wa mazingira anayopitia mtoto husika ,hivyo si vizuri kupuuza .

muwe na siku njema​
 
Mwanangu pia anatafuna meno usiku, umri wake ni miaka 6.
 
Back
Top Bottom