Ijue hifadhi ndogo kuliko zote Tanzania

Funa the Wild

Senior Member
Joined
Aug 1, 2022
Posts
167
Reaction score
282
Hifadhi ya kisiwa cha Saanane ndiyo hifadhi ndogo kuliko zote Africa mashariki inayopatikana mkoa wa Mwanza na ndiyo hifadhi pekee iliyopo katikati ya mji. Ni mwendo wa kilomita mbili tu kutoka mjini na kuifikia iliopo. Inapatikana kwenye kingo za ziwa Victoria.



Ni hifadhi inayokupa nafasi ya kuona wanyama, ndege na mandhari hadhimu yanayozunguka ziwa Victoria. Ni eneo lenye kukupa hewa safi yenye kukufanya usijuutie kupoteza muda uliotumia kufika hapo. Mwenyezi Mungu akupe nini kama sio pumzi ya bure uzidi kujionea maajabu ya uumbaji wake.

Jiji la mwanza limebarikiwa kuwa na hotel na lodge nyingi sana Ivyo hupaswi kuwaza utapata wapi sehemu ya kufikia endapo utahitaji kutembelea hifadhi iyo.
 
Hifadhi ya kisiwa cha Saanane ndiyo hifadhi ndogo kuliko zote Africa mashariki na ndiyo hifadhi pekee iliyopo katikati ya mji. Ni mwendo wa kilomita mbili tu kutoka mjini na kuifikia iliopo. Inapatikana kwenye kingo za ziwa Victoria.
Nyoka wapo?
 
Nitakuja ngoja nimshtue mwanangu flani. Ila tusije Kuta tumejaa wanaume tu
 
Maajabu ya Mungu sijui walifikaje huko wakati kumezungukwa na maji, nilishangaa kuwakuta viboko Mafia sijui walivukaje bahari toka bara
Idadi kubwa ya wanyama huwa wanapelekwa uko/kusafirishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…