SoC03 Ijue Historia ya Kariakoo

SoC03 Ijue Historia ya Kariakoo

Stories of Change - 2023 Competition

saadala muaza

Member
Joined
May 12, 2023
Posts
38
Reaction score
38
IJUE HISTORIA YA KARIAKOO(Carrier corps)

Mwandishi:Saadala Muaza

Utangulizi
kariakoo ni jina la kata inayopatikana katika wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es salaam Tanzania iliyo na wakazi zaidi ya 13000 waishio humo.

Eneo hili ni maarufu sana nchini Tanzania kutoka na shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazofanyika katika eneo hili kama uuzaji na ununuaji wa nguo,vifaa vya ndani,mapambo na hata vitu vya jikoni.

ASILI YA JINA KARIAKOO
Jina la eneo hili lilitokana na historia ya wakazi wa asili kabisa wa eneo hili ambao walijulikana kama wapagazi.

Wapagazi ni kikosi maalumu ambacho kilitumiwa na makoloni ya kijerumani pamoja na Waingereza katika vita vya kwanza vya dunia.Vikosi ambavyo vilijulikana kwa jina maarufu la carrier corps jina ambalo lilitumika kwa watu maalumu ambao walisaidia majeshi ya kikoloni kubeba silaha pamoja na vyakula kutoka sehemu moja ya vita kwenda sehemu nyingine katika vita maarufu sana iliyoitwa WWI.

Mwanzoni kabisa mwa vita hii mnamo miaka ya 1914 vikosi hivi vilitumiwa na wajerumani wakiongozwa na koronel mkuu PAUL VON LETTOW VORBECK.Kiongozi huyu aliongoza jeshi maaraufu la kijerumani liloitwa SCHUTZTRIPPE.Jeshi ambalo lilitumia kikosa cha watu kadhaa wa jamii ya kiafrika kwa ajili ya shughuli hii kwakuwa watu hawa hawakuhitaji chakula zaidi kwani ni watu waliotumia baadhi wa vyakula vilivyopatikana katika mazingira husika tofauti na Waingereza ambao walitumia wahindi pamoja na watu kutoka mshariki ya kati.

Mnamo miaka ya 1916 Waingereza nao waliamua kuanzisha jeshi hili ambalo lilikuwa na zaidi ya watu 400,000 wa jamii hii kwa ajili ya kazi hii.Wakiliita

Baada ya vita hivi mnamo miaka ya 1919 mwanzoni kabisa mwa miaka hii serikali ya kiingereza iliamua kuwatunuku watu hawa ardhi katika eneo hili ambalo kwa sasa linajulikana kama kariakoo(carrier corps) kwa ajilo ya kuanzisha makazi yao. Japo inasemakana kuwa zaidi ya watu 95000 wa jamii hii walifariki kutokana na kukosa chakula na maradhi mbalimbali yaliyo wakabili.

Na eneo kama hili linapatikana pia kenya sehemu iitwayo(kariakor).

Asanteni
 

Attachments

  • Screenshot_20230515-114332.jpg
    Screenshot_20230515-114332.jpg
    54.7 KB · Views: 9
Upvote 2
Back
Top Bottom