Ijue historia ya muziki wa Disko Tanzania

Weee nae bana muziki unakuona yaani unaongelea za darisalama tuuu!! kwani Wana sensera Ok Jazz Band! wewe unawajua!! haya kma haitoshi Mugumu all stars!! uliwahi kuwasikia wanapiga nyimbo za kikurya weye!

Butiama Jazz Band iko mpaka leo haifi ile!
 
Noma sana....aiseee umenirudisha nyuma sana enzi za ujana wangu....[emoji24][emoji24]
 
Disco zamani ilikuwa burdan

Sana

Ova
 
Inasisimua kuendelea kusoma
 
Huyu DJ ni tofauti na Msanii Niga Jay ambaye sasa anafahamika kama Prof. Jay, au ndo yy alikuwa DJ wakati huo?
Hao ni watu wawili tofauti, DJ Niga J kwa majina mengine anafahamika kama Masoud Masoud ni mtangazaji wa TBC siku hizi, Prof J mwanzoni alipokuwa kundi la Hard Blasters nae alitumia jina la Niga J
 
Weee nae bana muziki unakuona yaani unaongelea za darisalama tuuu

Angalizo lako limepelekea Utafiti kufanyika na umewezesha kutambua kuwa mbali ya Dar es Salaam pia zilikuwepo kumbi maarufu za Disco mikoani :

Tanzania bila kutaja kumbi za disco ktk miji ifuatayo haki itakuwa haikutendeka, Mwanza kulikua na Disco la Magnum, Kabibi, Savanna, Alshers, Natta Hotel, Pamba Roof, Rendevous Makutano Mwanza Hotel na Uptown Disco.

Pia kumbi zingine maarufu kitaifa ni Cave Disco Arusha, Kilimanjaro Disco pale Moshi, NK Disco Dodoma.
Source : OLD SKULI YA DJ BONNY LUV NA DJS WA ENZI HIZO!!
 
Habari kwa hisani ya Jeff Msangi

Mshauri wa muziki DJ Seydou mkongwe katika fani anaangaziwa :


Kunako miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90, majina ya Ma-DJ yalikuwa makubwa kama ilivyo kwa wanamuziki wa kizazi kipya na cha zamani hivi sasa. Mojawapo ya majina hayo ni DJ Seydou(pichani). Yeye na DJ mwenzake aliyekuwa anajulikana kama DJ Yaphet Kotto walitamba sana na disco lao la RSVP Discotheque pale Mbowe (siku hizi Club Billicanas). Enzi hizo vijana walikuwa waende wanakokwenda usiku unakuwa haujakamilika kama hawatofika Mbowe kupata ladha kutoka kwa DJ Seydou na mwenzake.Jina lake halisi ni Saidi Mkandara.

Tofauti na Ma-DJ wenzake wa enzi hizo, yeye alikuwa sio muongeaji sana. Badala yake yeye alisifika sana kwa uwezo wake wa kupangilia miziki. Akianza vitu vyake alikuwa hakai mtu kitini mwanzo hadi mwisho. Uwezo wake wa kusoma ukumbi na kujua aweke muziki gani ulikuwa unawastaajabisha wengi.

Isitoshe DJ Seydou alikuwa akisifika kwa kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote mwingine enzi hizo. Kila jumamosi alikuwa hakosi kuibua kibao ama vibao vipya kutoka kona mbalimbali za dunia.

Hivi sasa DJ Seydou ni mshauri wa muziki wa sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Club Ambience ya Sinza na Sanaa Pub. Hazina ya muziki wa zamani na wa sasa aliyonayo haina mfano. Uliwahi kuhudhuria disco la DJ Seydou? Tupe kumbukumbu zako kwenye sehemu ya comments.



Pichani DJ Seydou akiwapa vijana historia ya burudani nchini Tanzania tangu enzi hizo mpaka sasa. Hiyo ilikuwa hivi karibuni wakati wa matukio ya WAPI pale British Council jijini Dar-es-salaam.

Baadhi ya miziki ambayo Seydou alikuwa akiipiga enzi hizo ni kama huu hapa uitwao Get Down on It wa Kool and The Gang. Asante msomaji wetu Daniel kwa kutukumbusha tune ya wimbo huu. Pia unaweza sikiliza vibao Midas Touch kutoka kwa Midnight Stars, Don’t StopTill you Get Enough kutoka kwa Michael Jackson, A Night To Remember kutoka kwa Shalamar, Kleer- Intimate Connection
source : DJ SEYDOU – Bongo Celebrity
 
CLUB MAGNUM YA MJINI MWANZA , TANZANIA

Mmiliki wa Club ya Disco ya Magnum mjini Mwanza Tanzania miaka 1985 Mzee Henry Mtinda Matata


Alileta vifaa hatari kabisa vya muziki wa disco mjini Mwanza na kuzua gumzo Afrika Mashariki na Kati.

Ataja kwa uchache aliyoyaona Nairobi, Kampala, Johannesburg, Hong-Kong, New York, Cologne, London, Liverpool ni baadhi ya miji aliyotembelea na kuishi Mzee Henry Matata mfanyabiashara na ndiyo iliyompatia uzoefu na ilimpelekea kuvutiwa na jina la Club Magnum aliyoiona jijini London na kuamua kuanzisha Club Magnum mjini Mwanza ....anasimulia Mzee Matata ukali na umaarufu wa Club Magnum...

Sifa na jina la Club Magnum Mwanza zilizovuma kama moto mkali wa nyikani, ilipelekea wapenzi wa disco na maDJ kufunga safari toka maeneo mbalimbali ya Afrika ya Mashariki na Kati kuelekea Mwanza wakati wa wikiendi kwenda kujihakikishia ukali na viwango vya disco hilo na umahiri wa maDJ wake, anasimulia Mzee Matata ...
Source : Millard Ayo
 
Nseems Village-Musoma mjini, Ukumbi wa Maraha -Mugumu serengeti, Matumbi Bar non stop- kamunyonge!! nyakutonya!
 
16 June 2016

TANZANIA DISC MUSIC ASSOCIATION (TDMA) yaani Chama cha Muziki wa Disco Tanzania

Wanachama wakongwe wakiwemo DJ Sweet Francis, DJ Seydou, DJ John Peter Pantalakis , Asanterabbi siku ya kuadhimisha International Dance Day kila April 29 ulimwenguni kote


Picha na habari kwa hisani kubwa ya SIKU TDMA WALIPOSHEREHEKEA INTERNATIONAL DANCE DAY
 
Huyu DJ ni tofauti na Msanii Niga Jay ambaye sasa anafahamika kama Prof. Jay, au ndo yy alikuwa DJ wakati huo?
Dj Nigga J huyo ni Masoud Masoud manju wa muziki . Nigga Jay wa kizazi chetu ni Prof. Jay "Joseph Haule"
 
Ogaaah! Huyo jamaa si alkuwa pale Clouds FM??

Dj Steve B a.k.a Skills 2006​



Dj Steve B a.k.a Skills Steve Allen Mdoe akifanya vitu vyake ! Dj huyu inasemekana ni muanzilishi wa jina la bongofleva, ambalo kwa sasa linatambulika kuwa ni muziki wa kizazi kipya ! na kweli jina hilo limekubalika na kukaa mahali pake ! hata baadhi ya Wasanii (na Ma-Dj wenzake ) wa muziki huo wanatambua mchango wa Dj Steve B a.k.a Skillz
 
Katika huu muziki wa disco...
Pia ni lazima tuwajumishe wachezaji mashuhuri wakati huo...
Kama kina Black Moses(Musa Simba) na Athumani "Digadiga"....kwenye mchuano wao wa nani mkali pale Lang'ata Social club...miaka ile tunasoma primary school
Baadae wakaja kina "The Wacko Jacko" John Maganga ndio wakaharibu kila kitu......
 
ni nzuri lkn ndefu mnooo! mpaka nalala duuu!!! miaka ya zamani hukoooooo! na nyerere! mkoloni hwakuwepo ma DJ/ kwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…