Ijue Historia Ya Namanga Oyster Bay

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Hapo kale, palikuwa na shida ya bidhaa muhimu na adimu. Ilibidi bidhaa hizo ziwekewe mgao. Na zinapatikana kwa siku maalum... ukibahatisha.

Misamiati ya mikingamo, duka la kaya, mwendo wa kuruka, bei ya serikali, Tume ya Bei, Shirika la Ugawaji la Taifa, ilikuwa sehemu ya wimbo, ambao kibwagizo chake kilikuwa: "uhaba wa fedha za kigeni, kushuka kwa thamani ya shilingi, kupanda kwa gharama za uendeshaji, na sababu zisizoweza kuzuilika".

Eneo ambalo bidhaa adimu na muhimu zilikuwa hazikauki, ilikuwa ni Namanga, Arusha, kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

Kwa hapa Dar es Salaam, ilibainika kwamba maduka yaliyoko maeneo fulani ya Ostabei yalikuwa hayana shida ya kukosekana bidhaa muhimu na adimu, kama vile Namanga, Arusha.

Hivyo wananchi wakapaita jina la utani Namanga.

Na hiyo, ladies and gentlemen, ndiyo historia fupi ya Namanga, Oysterbay.
 
Kabla ya hapo.Namanga ya oysterbay paliitwa kwa Mpemba,ambapo alikuwepo mzee mmoja wa kipemba kwa muda mrefu ndiye alikuwa na Duka kubwa pale barabarani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiishi Namanga usipo mjua John Banzi Bado ujaishi mitaa ya Namanga


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…