SoC02 Ijue homa ya ini

SoC02 Ijue homa ya ini

Stories of Change - 2022 Competition

SHEBBY-INC

New Member
Joined
Aug 14, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Historia inaanza miaka zaidi ya million 82 iliyopiya ambapo virusi vinavyosababisha Homa ya inni (Hepatitis B) viligunduliwa uko afrika ya kaskazini mapoja na masharikI ya kati huku wataalamu wakidai kwamba virusi ivyo vilitokana na ndege pamoja na samaki kisha vikaenda kwa binadam. Ni miaka mingi sana ambapo leo hii virusi vya homa ya inni vimekuwa tishio kwa mamilion ya watu Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kusabisha kansa ya inni ambayo upelekea vifo.

JE HOMA YA INNI NI NINI?

download-1.jpg

Homa ya inni ni kuvimba kwa inni kunakosababishwa na Virusi (hepatitis Virus) pamoja na sababu zingine kama vile mtindo wa maisha ambao unachagiwa kwa kiasi kikubwa na kufanya mapenzi bila kitumia kinga ,matumizi ya tumbaku pamoja na sigara yanaweza pia kuleta matatizo kwenye inni.

lakini kwakuwa tunajikita kwenye namna gani virusi hivi vinavyomaliza maisha ya waanzania kimya kimya basi ngoja tuangalie undani wa homa ya inni inayosababishwa na virusi na kwanini inauwa kimya kimya.

Mamlaka za kimataifa zinazohusika na afya yaanI shirika la afya duniani (WHO) imeitaja homa ya inni kuwa ni moja katika ya magonjwa yanayozembewa zaidi katika mataifa mengi ya afrika yaani ( Neglected diseases ) na hii kwa sababu ya gharama za matibabu ya ugonjwa wenyewe ambapo rasilimali fedha na watu wamekuwa wachache kwenye mataifa ya afrika ndio maana mataifa mengi hayajashika uthubutu wa kupambana na homa ya inni.

KIPI CHA KIPEKEE KWENYE HOMA HII?
Report zinasema zaidI ya watu milion 296 dunia mzima wanaishi na Homa ya Inni pia zaidi ya watu milion moja hupoteza maisha kutoka na homa ya inni kila mwaka. Shirika la afya duniani limegawanya idadi iyo kutokana na kanda zake yaani ( WHO Region Offices). Kuna kanda sita za WHO ambapo Homa ya inni imeonekana kuwa tishio zaidi ambapo ni pasific ya magharibi ambapo zaidi ya watu 116 wanaishi na maambukizi ya homa ya inni ikifuatiwa na africa ambapo zaidi ya watu 81 millioni wana maambuzi sugu ya homa ya inni. Kwengine ni Mediterranean mashariki ambapo zaidi ya watu million 60, ikifuatiwa na kusini-mashariki mwa Asia ambapo zaidi ya watu million 18, ikifuatiwa na ulaya million 14 na mwisho na marekanI mbapona watu zaidi ya million 5 wanaishi na maambuzi ya hayo.

JE HOMA YA INNI INAAMBUKIZWAJE?

Katika maeneo yanye maambukizi makubwa ya Homa ya inni sababu kubwa imedaiwa kuwa ni maambuzi toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakatI wa kuzaliwa. Hii ndo imakuwa sababu inayobeba asimilia kubwa sana ya maambukizi. Homa ya inni pia inaambukizwa kupitia kujichora mwilini yaani tatuu, mchanganyiko wa damu wakati wa tendo la ndoa au kutiwa damu ya mtu mwenye maambukizi.
Homa ya inni pia huambikizwa kutumia vifaa vyenye ncha kali kama kiwembe, sindano na vingine vingi.
Pamoja na hayo ni kwamba homa ya inni ina chanjo ambayo ufanisi wake ni wa asilimia 98 mpaka 100 katika usalama wa kumkinga mtoto atakaezaliwa asipate maambukizi na kinga ya homa ya inni iliza kitolewa mwaka 1991 baada ya mpango wa kinga unaoitwa Extended Programs on immunization (EPI)

JE HOMA YA INNI INAUWAJE WATANZANIA KIMYA KIMYA?

Report ya siku siku ya Homa ya inni Dunia mwaka 2022 yenye dhamira ya kwamba homa ya inni haiwezi kusubiri (Hepatitia Can't wait) , inadai homa ya inni inaongoza kwa kusabanisha vifo vingi kupitia kansa ya inni kuliko hata ukimwI na maralia, hii ni kwa sababu kila baada ya sekunde 30 mtu mmoja anafariki dunia kutokana Homa ya inni ambayo ina chukua asilimia 60 ya vifo vyote vinavyosabaishwa na kansa.

images.jpg

Swala limekuwa la kimya kimya kwa sababu watanzania asilimia kubwa hawana uwelewa juu ya homa ya inni kiasi kwamba hata ukiwa na dalili ni ngumu sana kujua kwakuwa mara nyingi dalili zake sio za moja kwa moja na hazikupi mashaka ya kutamani kuchukua hatua ya kwenda kufanya vipimo labda mmpaka hali yako itakapokuwa mbaya zaidi ndipo utagundua wakati hakuna namna tena ya kukusaidia.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom