Pre GE2025 Ijue idadi ya wanawake Kamati Kuu za CCM, ACT Wazalendo, CHADEMA na CUF. Uwiano huu ni sababu hawana uwezo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,580
Reaction score
1,987
Ijue idadi ya wanawake katika Kamati kuu za CCM, Chadema, ACT Wazalendo na CUF

ACT WAZALENDO

1741688813186.jpeg
  • Kamati kuu ya ACT Wazalendo ina wajumbe 55 ambao kati yao 23 ni wanawake. Wajumbe hao ni pamoja na Kiongozi wa chama, Naibu kiongozi wa chama, Mwenyekiti wa Taifa, makamu wenyeviti (Bara na Zanzibar), Katibu Mkuu, Manaibu Katibu wawili (Bara na Zanzibar).
  • Wengine ni Wenyeviti wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee Taifa, wenyeviti wa kamati za kudumu (Kamati ya Maadili), makatibu wa kamati za kudumu na makatibu ngome za chama wanaoingia kwa nafasi zao lakini hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
  • Wengine ni wajumbe wanane waliochaguliwa na Halmashauri Kuu kwa kuzingatia kuwa, wajumbe sita watatoka Bara na ambao angalau wawili wawe wanawake na wajumbe wawili watoka Zanzibar ambao angalau mmoja awe mwanamke.
  • Kuna wajumbe watano wanaoteuliwa na Kiongozo wa Chama.
  • Wengine ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar waliotokana na ACT Wazalendo.
  • Nafasi nyingine ni ya Waziri Mkuuau kiongozi wa Kambi rasmi ya katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na Kiongozi wa kambi ya upinzani katika Barza la Wawakilishi Zanzibar.
  • Wengine ni Washauri wa chama Taifa na Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
1741688860245.png
  • Chama cha Demokrasia na Maendeleo kina nafasi 52 za wajumbe wa kamati kuu, lakini mpaka sasa nafasi zilizojazwa ni 39 ambazo wanawake ni saba tu.
  • Wajumbe wa kamati Kuu ni pamoja na Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti Bara, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Bara, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
  • Nafasi nyingine ni za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na Chama, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na Chama, Rais wa Zanzibar anayetokana na Chama, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar anayetokana na Chama, Spika wa Bunge na Spika wa Baraza la Wawakilishi watokanao na Chama.
  • Wengine ni Wawakilishi watano wa Wabunge wa Bunge la Muungano, Wajumbe watatu toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
  • Wajumbe nane waliochaguliwa na Baraza Kuu kuingia Kamati Kuu kwa uwiano wa nusu kwa nusu wanaume na wanawake na mjumbe mmoja kutoka kila kundi atoke Zanzibar na wawakilishi watano wa madiwani wa Chama, wawili wakiwa madiwani wa kawaida na watatu wawe Wenyeviti/Mameya wa Halmashauri zinazoongozwa na Chama.
  • Wengine ni Wenyeviti wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ngazi ya Taifa, wajumbe wateule wasiozidi sita watakao teuliwa na Mwenyekiti Taifa kwa kushauriana na Katibu Mkuu na kuthibitishwa na Baraza Kuu angalau wawili wawe wanawake.
  • Wengine ni wenyeviti Wastaafu wa Chama ngazi ya Taifa, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni au Waziri Mkuu atokanaye na Chama, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani au Makamu wa Pili wa Rais kwenye Baraza la Wawakilishi atokanaye na Chama, Wenyeviti wa Kanda, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini atakuwa mjumbe asiye na kura, Wakurugenzi wa Kurugenzi za Chama watakuwa wajumbe wasio na kura na Makatibu wa Mabaraza ya Chama ngazi ya Taifa watakuwa wajumbe wasio na kura

CHAMA CHA MAPUNDUZI (CCM)
1741688947311.png
  • Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ina jumla wajumbe 26 ambapo kati yao wanawake ni watano. Wajumbe hao ni Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wawili wa Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana n a CCM, Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM, Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anayetokana na CCM na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara na Zanzibar).

  • Wengine ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na CCM na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizasheni, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha, Mwenyekiti wa Taifa wa kila Juimuiya ya CCM na Mwenyekiti wa kamati ya Wabunge wa CCM.

  • Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano anayetokana na CCM, na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar anayetokana na CCM, Wajumbe Sita waliochaguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa watatu kutoka Tanzania Bara na watatu kutoka Zanzibar, wakiwemo wanawake wasiopungua wawili mmoja kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Zanzibar
THE CIVIC UNITED FRONT (CUF)
1741689056842.jpeg
  • Chama cha Wananchi (CUF) kina Baraza Kuu la uongozi lenye wajumbe 65 ambapo kati yao 24 wanaweza kuwa wanawake kutegemea na hali ya upatikanaji wao.
  • Wajumbe hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Taifa, Makamo Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Mkuu, Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wanaotokana na Chama, Rais na Makamu wa Rais wa Zanzibar wanaotokana na Chama.
  • Wengine ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taifa (18) pamoja na wajumbe 45, ambapo 25 kutoka Tanzania Bara na wanane watakuwa ni wanawake, na wajumbe 20 kutoka Zanzibar, ambao angalau sita watakuwa ni wanawake waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa kutoka miongoni mwao.
  • Wajumbe watano, watatu kutoka Tanzania Bara na wawili kutoka Zanzibar watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti Chama kutokana na wanachama wajasiri wa Chama, isipokua ijulikane tu wajumbe wasiopungua asilimia 30 ya Wajumbe hao wa kuteuliwa watakuwa ni wanawake.
  • Wengine ni wajumbe walemavu wawili, mmoja kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Zanzibar walioteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama, baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti, ambapo mmoja atakuwa mwanamke na mwengine atakuwa mwanamme, kutokana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa au wanachama wajasiri wa Chama.
  • Mwenyekiti wa kila Jumuiya ya Chama pamoja na Mjumbe mmoja aliyechaguliwa na Baraza la Taifa la kila Jumuiya ya Chama pia atakuwa mjumbe.
  • Wengine ni Kiongozi wa kambi ya wabunge wa Chama katika Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na Kiongozi wa kambi ya Wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Attachments

  • 1741688764522.jpeg
    1741688764522.jpeg
    5.1 KB · Views: 1
Ijue idadi ya wanawake katika Kamati kuu za CCM, Chadema, ACT Wazalendo na CUF

ACT Wazalendo
  • Kamati kuu ya ACT Wazalendo ina wajumbe 55 ambao kati yao 23 ni wanawake. Wajumbe hao ni pamoja na Kiongozi wa chama, Naibu kiongozi wa chama, Mwenyekiti wa Taifa, makamu wenyeviti (Bara na Zanzibar), Katibu Mkuu, Manaibu Katibu wawili (Bara na Zanzibar).
  • Wengine ni Wenyeviti wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee Taifa, wenyeviti wa kamati za kudumu (Kamati ya Maadili), makatibu wa kamati za kudumu na makatibu ngome za chama wanaoingia kwa nafasi zao lakini hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
  • Wengine ni wajumbe wanane waliochaguliwa na Halmashauri Kuu kwa kuzingatia kuwa, wajumbe sita watatoka Bara na ambao angalau wawili wawe wanawake na wajumbe wawili watoka Zanzibar ambao angalau mmoja awe mwanamke.
  • Kuna wajumbe watano wanaoteuliwa na Kiongozo wa Chama.
  • Wengine ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar waliotokana na ACT Wazalendo.
  • Nafasi nyingine ni ya Waziri Mkuuau kiongozi wa Kambi rasmi ya katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na Kiongozi wa kambi ya upinzani katika Barza la Wawakilishi Zanzibar.
  • Wengine ni Washauri wa chama Taifa na Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini.

Chadema
  • Chama cha Demokrasia na Maendeleo kina nafasi 52 za wajumbe wa kamati kuu, lakini mpaka sasa nafasi zilizojazwa ni 39 ambazo wanawake ni saba tu.
  • Wajumbe wa kamati Kuu ni pamoja na Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti Bara, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Bara, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
  • Nafasi nyingine ni za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na Chama, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na Chama, Rais wa Zanzibar anayetokana na Chama, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar anayetokana na Chama, Spika wa Bunge na Spika wa Baraza la Wawakilishi watokanao na Chama.
  • Wengine ni Wawakilishi watano wa Wabunge wa Bunge la Muungano, Wajumbe watatu toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
  • Wajumbe nane waliochaguliwa na Baraza Kuu kuingia Kamati Kuu kwa uwiano wa nusu kwa nusu wanaume na wanawake na mjumbe mmoja kutoka kila kundi atoke Zanzibar na wawakilishi watano wa madiwani wa Chama, wawili wakiwa madiwani wa kawaida na watatu wawe Wenyeviti/Mameya wa Halmashauri zinazoongozwa na Chama.
  • Wengine ni Wenyeviti wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ngazi ya Taifa, wajumbe wateule wasiozidi sita watakao teuliwa na Mwenyekiti Taifa kwa kushauriana na Katibu Mkuu na kuthibitishwa na Baraza Kuu angalau wawili wawe wanawake.
  • Wengine ni wenyeviti Wastaafu wa Chama ngazi ya Taifa, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni au Waziri Mkuu atokanaye na Chama, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani au Makamu wa Pili wa Rais kwenye Baraza la Wawakilishi atokanaye na Chama, Wenyeviti wa Kanda, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini atakuwa mjumbe asiye na kura, Wakurugenzi wa Kurugenzi za Chama watakuwa wajumbe wasio na kura na Makatibu wa Mabaraza ya Chama ngazi ya Taifa watakuwa wajumbe wasio na kura

CCM
  • Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ina jumla wajumbe 26 ambapo kati yao wanawake ni watano. Wajumbe hao ni Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wawili wa Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana n a CCM, Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM, Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anayetokana na CCM na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara na Zanzibar).

  • Wengine ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na CCM na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizasheni, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha, Mwenyekiti wa Taifa wa kila Juimuiya ya CCM na Mwenyekiti wa kamati ya Wabunge wa CCM.

  • Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano anayetokana na CCM, na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar anayetokana na CCM, Wajumbe Sita waliochaguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa watatu kutoka Tanzania Bara na watatu kutoka Zanzibar, wakiwemo wanawake wasiopungua wawili mmoja kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Zanzibar

CUF
  • Chama cha Wananchi (CUF) kina Baraza Kuu la uongozi lenye wajumbe 65 ambapo kati yao 24 wanaweza kuwa wanawake kutegemea na hali ya upatikanaji wao.
  • Wajumbe hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Taifa, Makamo Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Mkuu, Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wanaotokana na Chama, Rais na Makamu wa Rais wa Zanzibar wanaotokana na Chama.
  • Wengine ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taifa (18) pamoja na wajumbe 45, ambapo 25 kutoka Tanzania Bara na wanane watakuwa ni wanawake, na wajumbe 20 kutoka Zanzibar, ambao angalau sita watakuwa ni wanawake waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa kutoka miongoni mwao.
  • Wajumbe watano, watatu kutoka Tanzania Bara na wawili kutoka Zanzibar watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti Chama kutokana na wanachama wajasiri wa Chama, isipokua ijulikane tu wajumbe wasiopungua asilimia 30 ya Wajumbe hao wa kuteuliwa watakuwa ni wanawake.
  • Wengine ni wajumbe walemavu wawili, mmoja kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Zanzibar walioteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama, baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti, ambapo mmoja atakuwa mwanamke na mwengine atakuwa mwanamme, kutokana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa au wanachama wajasiri wa Chama.
  • Mwenyekiti wa kila Jumuiya ya Chama pamoja na Mjumbe mmoja aliyechaguliwa na Baraza la Taifa la kila Jumuiya ya Chama pia atakuwa mjumbe.
  • Wengine ni Kiongozi wa kambi ya wabunge wa Chama katika Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na Kiongozi wa kambi ya Wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Duh.....
 
..Tume ya Warioba ilipendekeza wilaya ndio ziwe majimbo ya uchaguzi.

..pia ilipendekeza kila jimbo liwe na mbunge mwanaume, na mbunge mwanamke, wanaopigiwa kura moja kwa moja na wananchi.
 
Back
Top Bottom