Ijue inchi ya Luxembourg iliyo katika bara la Ulaya

Ijue inchi ya Luxembourg iliyo katika bara la Ulaya

Kingdom Finder

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
1,119
Reaction score
1,391
IJUE INCHI YA LUXEMBOURG ILIYO KATIKA BARA LA ULAYA

  • Ni kati ya nchi ndogo sana duniani. Ni ya 167 kwa udogo kati ya nchi 194 zilizopo katika dunia hii. Nchi ndogo sana duniani ni The Vatican iliyo ndani ya Roma. Nchi ya Tanzania ni ya 13 kwa ukubwa kwa bara la Afrika na ya 31 kwa ukubwa katika dunia.
  • Eneo la mraba wa wake ni kilomita za mraba 2586 (2,586km2). Eneo la Dar ni kilometa za mraba 1,590 (1590km2). Ukilinganisha Dar na nchi ya Luxembourg utagundua ina ukubwa wa mara 1.6 ya eneo la mkoa wa Dar.
  • Urefu na upana wa nchi ni kama 87km urefu na 57km upana. Urefu wake ni kama urefu wa Dar mpaka Chalinze na upana wake ni kama Dar na Mlandizi.
  • Hii nchi imepakana na nchi ya Ujerumani kwa upande wa mashariki, Ufaransa kwa upande wa kusini na kwa upande wa magharibi na kaskazini imepakana na nchi ya Ubeligiji.
  • Idadi ya watu wanaoishi ni wastani wa watu 634,814 kwa sensa ya mwaka 2020 na nusu ya hawa watu ni wageni. Idadi ya watu wa Daresalaam ni kama million saba kwa sasa (estimated population of Dar es salaa is about 7million). Ukilinganisha utaona kwamba idadi ya watu wanaoishi Dar ni mara 11 ya watu wanaoishi katika nchi ya Luxembourg.
  • Ni nchi ya kwanza katika bara la Ulaya kwa kiongozi wake kuoa mwanamme mwenzake (same sex partner)
  • Ni nchi ya pili duniani kwa GDP kubwa. Yaani ni nchi ya pili kwa kuwa na pato kubwa la taifa
  • Ni nchi ya kwanza katika dunia kutoa usafiri kwa wananchi wake bure. Uhitaji kuwa na ticket unaposafiri kwa bus, train na yale magari marefu yanayoitwa trams.
  • Ni kati ya nchi pekee wafanyakazi wengi wanatoka nchi za jirani na kwenda kufanya kazi katika nchi hii na kurudi kwao joini. Wafanyakazi wengi wanatoka katika nchi za Ujerumani, Ubeligi na Ufaransa
  • Ni nchi ambayo inatumia sana mapato yake kuwanufaisha watu wake katika elimu afya, makazi na usafiri na huwezi kumkuta maskini au omba omba barabarani.

Unaweza kuongeza mengine unayoyajua.
 
Habari za hii nchi nimezisoma juzi! Kuna mengi hauja orodhesha!
 
Ni nchi pekee barani ulaya kuwa na uhuru wa kwenye mapenzi ya jinsia mmoja yaani ushoga na usagaji nje nje.
 
Dar chalinze vs dar mlandizi sijaelewa. Kutokea mbagala_gongo lamboto_mbezi au kibamba? Maana dar nayo sio kijiji.
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Ni nchi ya luxembourg wafanyakazi wa serikali au binafsi hupokea mshahara mkubwa kupita nchi yoyote duniani.
 
Back
Top Bottom