Ijue istilahi “Levant”

Mwita Matteo

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2010
Posts
216
Reaction score
55
Nimatumaini yangu kua umesha wahi kulisikia neno Levant, au kama hujawahi kulisikia, basi kama ni mfuatiliaji wa habari basi ulisha wahisikia kifupi cha neno hilo, hasa pale linapotajwa kundi la ISIL ambalo kirefu chake ni Islamic State of Iraq and Levant.

Levant ni nini?

Levant ni istilahi ya kijiographia na kihistoria ikihusisha eneo kubwa mashariki mwa mediterraneani. Katika matumizi mapana ya kihistoria, levant inahusisha maeneo yote ya mashariki ya mediterraneani na visiwa vyake, yaani inajumuisha nchi zote zilizo pwani ya mashariki ya medeterraneani, kuanzia ugiriki hadi Crenaica. Istalahi “levant” mawio kwa Kiswahili, ilianza kutumika kwenye lugha ya kingereza mwishono mwa karne ya 15, kutoka kwenye lugha ya kifaransa, na lilichukuliwa kutoka kwenye neno levante ambao lina asili ya italia, lenye maana ya chomoza, kwa dhana ya kuchomoza jua kutokea mashariki, yaani machweo, kwa maana hiyo neno mashriq ndio mbadala wake kwa kiarabu. “nchi au aridhi, ambayo jua huchomoza”

Katika karne ya 13 na 14 istilahi Lavante ilitumiwa na waitaliano kwa minajili ya bishara za baharini likihusisha eneo la mashariki mwa mediterania , lililo jumuisha nchi za ugiriki, Anatolia, Syria-palestina na Misri, baadae neno hilo lilitumika kumaanisha inchi za kiislamu za Syria palestina na Misri. Kwa hivi sasa neno levant, linatumika likiwa na muunganiko wa rejea za kihistoria na lina maana ya Syria-palestina, au Syria kuu,hili likiwa eneo lilio zungukwa na milima ya Taurus iliyopo Anatolia Magharibi, kwa upande wa magharibi bahari ya mediterraneani na kaskizanin eneo la jangwa la kiarabu na kwa mashariki ni eneo la Missopotamia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…