Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
- Thread starter
-
- #21
ilibemendwa, ikaishia daraja LA Tatu KolomijeAisee kuna Mecco ya Nyakato Mwanza,sijui yenyewe vipi,wajuzi?
sijui wabongo tulikoseaga wapi,yaani nikisiaga majina ya mashirika yetu na naskia zamani kila shirika lilikuwa na bendi yakePamba ilikuwa kiboko mkuu, walikuwepo watu kutoka morogoro Reli hiyo kiboko ya vigogo, bila kuisahau ushirika ya moshi, milambo ya tabora, timu za mashirika zilikufa na mashirika yake, RTC kigoma, RTC shinyanga, ujenzi rukwa, CDA Dodoma
ahhha hahah Bujibuji Pamba ilikuwa hatari sanailibemendwa, ikaishia daraja LA Tatu Kolomije
Willy Martin.... Jamaa alikuwa yuko vzr uwanjani, sidhani kama aliwaponesha simba, ingekuwa enzi hizi simba wangeng'oa sana viti hapo taifaCDA watoto wa nyumbani ya kina Charles mgodo (kijiko )na ushirika ya kina often Martin jaffar kiango abuu na fadhili juma kina Andrew kabisama willy Martin Steven nyenge mahmood abbas siku zimekwenda wapI?
Kuna Fikiri Magoso, full tallentedDo Reli ya Morogoro niliisahau asante mkuu.
Kuna mechi ilichezwa moro kati ya reli na simba enzi za madundo mtambo profesa hivi sasa na uwanja wa taifa yanga na majimaji sasa mtangazaji ana mbwembwe kweli kisha akasema habari kutoka huko morogoro kisha ana anaendelea kutangaza mpira wa Yanga kama nusu dakika hivi kisha anarudi na huko mji kasoro bahari simba simba wana bao mbili simba wamepata mabao mawili basi wacha mashabiki wa simba waanze kufurahi kisha akamalizia na reli ya Morogoro wanaongoza kwa mabao manne duh watu wa Yanga sasa ndio wakaanza kushangilia.Do Reli ya Morogoro niliisahau asante mkuu.
Sio Charles Hilary huyo?Kuna mechi ilichezwa moro kati ya reli na simba enzi za madundo mtambo profesa hivi sasa na uwanja wa taifa yanga na majimaji sasa mtangazaji ana mbwembwe kweli kisha akasema habari kutoka huko morogoro kisha ana anaendelea kutangaza mpira wa Yanga kama nusu dakika hivi kisha anarudi na huko mji kasoro bahari simba simba wana bao mbili simba wamepata mabao mawili basi wacha mashabiki wa simba waanze kufurahi kisha akamalizia na reli ya Morogoro wanaongoza kwa mabao manne duh watu wa Yanga sasa ndio wakaanza kushangilia.
Kabla yake alikuwapo juma limonga (stop engine )ilikuwa khatari sanaKuna Fikiri Magoso, full tallented
Yaah alikuwa Charles hillary nkwanga watu walitukana sana utadhani yeye ndio kawafungaSio Charles Hilary huyo?
bila ya kuandika historia, tutakuwa manyani wa mwituni .Kabla yake alikuwapo juma limonga (stop engine )ilikuwa khatari sana
Ipi ya kina mwanga luheya na mohamed mateneke walikuwa mawinga ali pande golini hapo kati mkoba juma nkulila na anthony Ngosha huku kuna Simon kishoka mohamed (bob )chopa pale mbele?Ndovu ya arusha enzi hizo mwenye line up atupatie
umeogopa jinsi anavyopanga vikosi,kuna watoto wakike huawambii chochote kuhusu soka,si unaona sky anavyokushushia filesSamahani lakini ram, huyo kwenye avatar ni wewe kweli?
Lipuli walikuwa vizuri na sasa hivi wameingia tena ligi kuu.wakuu msiisahau na lipuli ya karne hizo
Costal na African sport zilikuwa ziko vizuri, sijui pepo gani kapita tanga jamani, naona wanazidi kuporomoka madaraja tuMiaka ile Coast Union ilipotea kidogo, ilirudi baadae. Ninamkumbuka Ahamed Amasha wa Yanga, tulimpenda sana watoto wa kike enzi zile.
Alikuwa beki mshahara yule hataki maskhara aliwahi kumvunja mguu yusuph ambweni huyu alikuwa CDA watoto wa nyumbani upande wa pili wakaja kuibuka kurugenzi dodoma ya kina mohamed mbuguni sasa kuhusu abubakari kanyoro sikumbuķi alikuwa CDA au kurugenzi nimesahauMiaka ile Coast Union ilipotea kidogo, ilirudi baadae. Ninamkumbuka Ahamed Amasha wa Yanga, tulimpenda sana watoto wa kike enzi zile.
KMKM kutoka Zanzibar unaikumbuka? Kipindi cha michezo 19:45 kila siku.Costal na African sport zilikuwa ziko vizuri, sijui pepo gani kapita tanga jamani, naona wanazidi kuporomoka madaraja tu
Kombe la muungano mnalikumbuka wandugu? Timu tatu bara timu tatu zenji halafu mechi nyumbani na ugenini lol! Malindi na Pamba Ccm kirumba, mtangazaji Dominick Chilambo.... Lol, those days was wonderful jamani, haziwezi kujirudia tena