WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 949
NEMBO YA SIMBA
👉Kama wewe ni mpenzi wa kuangalia filamu za Hollywood, pasi na shaka utakuwa umekutana na neno MGM.
MGM ni kampuni ya utayarishaji na usambazaji wa filamu na vipindi vya Runinga iliyopo huko Marekani.
👉kampuni Ilianzishwa mnamo mwaka 1924 baada ya kuunganishwa kwa makampuni matatu ya utengenezaji Filamu ambayo ni Metro Pictures,Goldwyn Pictures Corporation pamoja na Louis B. Mayer Pictures.
Baada ya kuunganishwa kwa makampuni hayo ndipo likapatikana jina MGM ikiwa ni kifupi cha maneno "Metro-Goldwyn-Mayer" huku Marcus Loew akiwa ndio mkurugenzi mkuu wa MGM.
👉Ukiwa unatazama filamu yeyote iliyotengenezwa na Kampuni ya MGM kabla ya movie kuanza ni lazima utamuona SIMBA akiunguruma. Ile ndio nembo ya kampuni ya 👏
Hadi Leo hii Kampuni imewatumia simba wapatao Saba katika vipindi tofauti tofauti 👇
👉Simba wa kwanza kutumiwa na kampuni ya MGM aliitwa Slats Huyu alianza kutumiwa na kampuni ya Goldwyn kwenye filamu zilizotoka Mwaka 1917. Na aliendelea kutumiwa hadi 1924 ilipoanzishwa kampuni ya MGM.
👉Simba wa pili aliitwa Jackie aliyetumiwa kwenye muvi zilizotoka Mwaka 1928 hadi 1956 ikiwemo zile filamu za Tarzan zilizochezwa na muigizaji Johnny Weissmuller. Na mwingine aliitwa Telly.
👉Simba wa Tatu Coffee alitumiwa kwenye muvi za 1932 hadi 1935. Wa tano aliitwa 'Tanner', aliyetumika kuanzia 1954-1956. Wa sita ni George (1956-1957).
👉Simba wa mwisho kutumiwa kwenye filamu za MGM ni huyu anayeitwa LEO. Au maarufu Leo the Lio' yaani "Simba Leo".
Simba LEO alianza kutumiwa kwenye filamu zote zilizotoka kuanzia mwaka 1958 hadi sasa.
Pichani👇 ndio huyu Leo the lion akiwa anachukuliwa video kwa ajili ya kutumiwa kama nembo ya movie za MGM.
👉Simba huyu alizaliwa huko nchini Ireland kwenye Zoo ya Dublin akiwa anamilikiwa na mtu mmoja aliyeitwa Henry Trefflic.
Baadae alinunuliwa na kuanza kufundishwa na Ralph Helfer kwa ajili ya maonesho na filamu mbalimbali.