mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,778
- 7,145
Wana JF,
Halmashauri ya Muleba ndiyo inaoongoza kuwa na utajiri mkubwa kuliko wilaya zote za Kagera kimapato. Wilaya hii ina majimbo mawili, Muleba Kaskazini na Muleba Kusini. Sehemu kubwa ya utajiri wake ni kutokana kilimo cha kahawa, ndizi, mihogo, Karanga, maharage na mtama, pia wilaya hiii inamiliki sehemu kubwa ya uvuvi ndipo hupatikana dagaa wabukoba wasiona mchanga.
Samaki waliokaushwa vizuri na hawana mchanga. Wilaya hii imejaliwa wasomi wengi wapenda maendeleo. Lakini imepata bahati mbaya sana kupata wabunge bora wa kimkakati. Mali nyingi imepotea kwa kuwa tulikuwa na wabunge dhaifu. Wabunge wengi tuliwaamini kwa kuwa ni wasomi lakini tumejikuta tunaangukia pua. Wabunge tulio nao wote ni wakazi wa Dar es Salaam, angalau sasa mmoja ametangaza kustaafu.
Huyu mwingine hatujajua kama anaendelea. Huko nyuma mbunge Marehemu Zimbiile aliacha Halmashauri inamiliki Meli MV. Muleba, pia baadhi ya boti za uvuvi lakini zilitafunwa na mchwa. Sasa mazao mengi yaliyokuwa yanasafirishwa kwenda sehemu mbalimbali za ziwa hakuna. Vipande vya lami vilivyowekwa katika majimbo haya havizidi kilometa kumi na tano. Majasho yote ya kuoshea mifugo yameaharibika. Mshine za kupandisha maji vijijini yameaharibika. Barabara uchongwa kila ukikaribia uchaguzi. Madaraja mengi upitisha gari kwa kuviziana.
Imefika hatua kwamba sasa ni wakati wa watia nia watokee kijijini sio mijiini kwani wamjini wametutapeli kwa maneno imetosha. Tunataka wabunge watakaorudisha meli zetu.