Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Mimi nina swali je kama mtu ana jina lina herufi moja inakuaje hapo "N" mwezi wa 8
 
Kiongozi naomba kufaham nyota yangu ambae jina langu ni herufi moja tu "N" mwez 8
 
IJUE NYOTA YAKO

Nyota ni Elimu ya Sayansi ya kiroho ambayo inatumika Dunia nzima. Kila mtu katika Dunia akitaka asitake, aamini au asiamini atakuwa amezaliwa katika moja wapo ya nyota hizi 12 zilizopo.
Basi yale ya juu si kweli. Hakuna mtu anayezaliwa "katika moja wapo ya nyota hizi 12". Maana "nyota" hizi, kwanza si nyota. Unachojaribu kutaja ni makundi ya nyota zinazoonekana angani. Kila moja ni nyota nyingi, makumi zinzoonekana kwa macho matupui, mamilioni ukitumia darubini.

Pili makundi hayo ya nyota yanaonekana tu kama makundi lakini hayana uhusiano kati yao. Hali halisi hayapo pamoja. (ni kama ukaribia Dar kwa feri toka Zbar, unaanza kuona ghorofa: angalia, ghorofa hizi tatu! Kumbe baada ya dakika chache ghorofa haziko tena kandokando maana umeendelea unaona sasa ziko mbali kati yao)

Tatu makundinyota (constellations) unazorejelea - je unajua kwa nini zinatajwa kwa tarehe fulani? Ufafanuzi wake ni: Jua linaonekana katika eneo la "nyota" (constellation, kundinyota) fulani. Lakini si vile! Mfano unadai "Mbuzi" (Capricornis) kipindi chake ni 21 Desemba na 19 Januari , sivyo? Hii ilikuwa kweli karne nyingi zilizopita. Siku hizi Jua linaingia katika Mbuzi tarehe 20 Januari! Maanake mnatumia makundinyota yaliyopitiliwa na Jua karne nyingi zilizopita - hizi nyota zimebadilika tayari.

Nne si "nyota" (constellations, makundinyota) 12 bali 13 zinazopitiwa na Jua kwenye njia yake angani. Namba 13 mnayopenda kusahau (au hamjui?) ni Hawaa au kwa jina la Kizungu Ophiuchus (mbeba nyoka); Jua linapita hapa 30 Novemba hadi 17 Desemba.

Mwishoni: mtu mwenye akili timamu hahitaji kujua mengi kuhusu nyota ili kuelewa maelezo yako si sahihi. Unadai eti "nyota" zinamulia tabia ya mtu? Kwa hiyo watu wote waliozaliwa katiuka kipindi fulani zina tabia za pamoja?
Ambayo ni kinyume ya halisia, kinyume ya kila maarifa. Watu 10 waliozaliwa katika kipindi kilekile si ama wapole au wachangamfu au wenye utu au ukali. Kuna mchanganyiko wa kila aina za tabia kwa kila tarehe.
 
Bado sijaelewa swali lako mkuu kila nyota inanafasi yake na majibu ni tofauti

Rakims
Kila nyota ina nafasi yake katika anga la nje, lakini hakuna nyota yenye wajibu. Nyota ni gesi joto (inayoitwa plazma), gesi haina wajibu. Binadamu pekee and wajibu. Nyota ni kitu. Kitu kikubwa sana, lakini kitu tu,
 
Haya ni kwa mtizamo wako na uelewa wako katika kupitia vitabu viwili vitatu na google,
Sana nitapoteza muda kukuelewesha maana ukitaka nianze kukuelezea kwanini zipo hivyo na zimewekwa hivyo ni darasa pana na linalohitaji muda mrefu sana kukuelewesha maana si ajabu ukarudia maswali ya watu wengine kuwa nini sababu ya jua kuwekwa katika makundi ya sayari kinyota,
hsana nikikujibu swali moja au maswali kumi yatazaa maswali thelathini na hoja arobaini na nitajikuta nazungusha muda wangu kukuelezea mambo ya karne nyingi ili uyaelewe kwa quote moja ikiwa unataka kujua kwa nini huu umebaki mtizamo ule ule na kama upo interest na elimu hii basi soma zaidi na ndio maana elimu hii ipo kwa wachache

Pia sikatai unaposema kuwa mtu mmoja na mwingine wamezaliwa katika nyota moja lakini wanatabia tofauti hii upo sawa na upo sahihi lakini cha kujua kingine ni kwamba hizi nilizoandika hapa ni nyota za watu kulingana na jua,kuna kulingana na mwezi,kuna kulingana na sayari kuna mahusiano ya kinyota kuna vitu vingi sana katika elimu hii ndio maana ili mtu aweze kujijua hasa anaenda vipi katika nyota hizi na kumpa uhakika zaidi ni lazima atoe details zote kuhusu yeye ili kuweza kupima kama tarehe ya kuzaliwa mwezi mwaka jina lake jina la mama jina la baba eneo alilozaliwa saa aliozaliwa kipindi alichozaliwa mambo mengi sana kuna decanates kuna cusps za mtu kuna lat na lon hadi kumuweka mtu sawa na aelewe mkuu inataka muda
Kuna mtu kazaliwa kwenye nyota ya mbuzi lakini hakuna hata kimoja kwenye nyota ya mbuzi kinachoendana nae na hata akijaribu kuifuata hakuna kinachotokea ndio hapo huamua kuhukumu kuwa huu ni uongo uliopitwa na wakati
Na hakuna mtu anafanana na mtu nyota isipokuwa wale tu waliozaliwa siku moja saa moja lakini nao hupishana tabia kwa maana kila dk 15 mzunguko wa nyota hugeuka
Kama nilivyosema sio rahisi kukufafanulia ukaelewa au ukaona point zangu zina mashiko kwa quote moja au kukuelewesha kirahisi rahisi mkuu wewe baki na elimu yako unayoielewa wewe

Rakims

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hakuna mtu anafanana na mtu nyota isipokuwa wale tu waliozaliwa siku moja saa moja lakini nao hupishana tabia kwa maana kila dk 15 mzunguko wa nyota hugeuka
Si vigumu mno kuielewa. Juu ya ile ya juu: sema tu nyota zipi "hugeuka" kila dk 15? Kutoka wapi kwenda wapi?
Hujui ni Dunia inayojizungusha kila siku, si nyota?

Halafu vipi kuhusu makundinyota 13 yaliyopo kwenye njia ya Jua hali halisi, si 12. Hujawahi kusikia habari za Ophiuchus?
 
Kila nyota ina nafasi yake katika anga la nje, lakini hakuna nyota yenye wajibu. Nyota ni gesi joto (inayoitwa plazma), gesi haina wajibu. Binadamu pekee and wajibu. Nyota ni kitu. Kitu kikubwa sana, lakini kitu tu,
Mkuu mtizamo wa nyota kiroho na kisayansi ni vitu viwili tofauti wewe upo sawa kisayansi na mimi nipo sawa kiroho kwa hiyo ukilazimisha niamini unachojua wewe nitakuona mjinga na mimi nikikuaminisha ninachojua mimi utaniona mjinga maana sote ni binadamu lakini tunatembea katika mazingira ya elimu tofauti.
wewe upo kisayansi wenzio wanaoamini katika sayari watasema unaakili sana lakini mimi nina imani potofu na wanaoamini mambo ya kiroho watasema mimi nina elimu sana na wewe una elimu potofu.

Huna tofauti na shehe anaehutubia kanisani na padri anaehubiri msikitini

Tupo sawa lakini katika mitizamo tofauti elewa

Rakims

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeisoma sana kwenye vitabu vya elimu ya nyota(بروج) unafahamu kwa nini iliunganishwa pamoja na nyota ya Kausa? Kama hufahamu basi rejea kwenye kitabu cha ابو معشر الفلكي kinazungumzia kwa nini iliachwa kwenye nyota ya Kausa na kwa nini haikuwa na sababu ya kuwekewa maelezo na ikaachwa karne ya ٢

Rakims

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unataka kutetea kwa nini الحواء iliachwa , ingawa ni kundinyota ya kale kabisa na Jua linapita humo kabisa - basi uitetee kwa maneno yako mwenyewe. Tafadhali usijifiche nyuma ya herufi za Kiarabu! hakuna sababu ninayokubali kuiunganisha na كوكبة القوس ("Kausa" yako si Kiarabu). Mawazo ya Abu Ma'shar hayana umuhimu kwangu. Tena hata yeye hakuiamua ( المستعين بالله alikuwa na sababu yake kumchapa kiboko sivyo?) aliwafuata tu wengine - ambao walihitaja namba 12 bila kujali nyota halisi.
 
Mkuu kama una nafasi naomba utudadavulie uelekeo wa nyota ya punda kwa mwaka huu 2020 japo kwa ufupi Rakims
 
Mkuu jaribu kuelewa pale nilipokwambia kuwa nikijibu swali lako moja yatazaa kumi na sana nitajaza thread yangu kwa kujadili na wewe kitu ambacho hukielewi na ulishaamua kutokukielewa. Hoja zako kwangu hazina msingi kama vile wewe ulivyoona za Abu Mashar kwako hazina msingi pia nitakushangaa kusema ninajificha kwenye herufi za kiarabu ni sawa na muandishi mwingine humu aliyewahi kutaka kunikosoa thread nzima kwa neno kamali kuwa kamari.

Kila mtu anauelewa wake katika mambo yote yaliyomo duniani na anasoma anachosoma sasa kama wewe utapinga hoja za watu wengine fuata zako hakuna aliyekulazimisha ndio maana kila mtu anauelekeo wake anaoufuata anavyojua na anavyojisikia.


Rakims

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lakini kuna upande haya maelezo ya nyota yanapingana sana,sio subjective
 
Kumi na tano Sept huyu ni mashuke, kwa Nini unadai Kuna nyota zangu nyingine za jina mfano herufi B na hiyo nyingine naijuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…