Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Mke wangu anaanzia herufi R kazaliwa 22/12/1984 Bukoba nyota yke ni ipi?
Herufi ya kwanza ya jina haitoi hukumu kamili na sahihi kinyota hizo ni kama uthibitisho tu

Rakims
 
Rakims mimi nyota yangu ni pisces lakini kila nikipata kazi nafanya mdamcheche naacha kisha nikikaa dukani kwangu nafurahia sana maisha na nakuwa huru.
Sasa baada ya muda tena napata kazi nafanya mda mchache naacha.
Kwa kifupi huwa sikai kwenye kaI kuda mrefu bila kuacha.
Je wenye nyota ya pisces tunafaa kufanya kazi ama biashara binafsi?
 
Habari Kiongozi
Nahitaji Msaada wa kinyota hapa
Jina langu linaanzia na R na nimezaliwa 20/06, Kuna wanawake wawili katika maisha yangu na wote majina yao yanaanzia na R, mmoja kazaliwa 01/01 na mwingine kazaliwa 11/10
 
Ndio unaweza kufanya biashara binafsi hasa zitakazounganisha maji kama soda,maji,pombe(haramu kwa waumini) n.k vimiminika pia vile vile kuchimbisha au kuchimba visima hii ndio itakutajirisha haraka mwenye nyota hii, kiganga inafahamika kama nyota ya maji ya kisima,

Jiepushe kuhusisha mchanga,moto au moto katika kujiajiri huko

Rakims
 
Habari Kiongozi
Nahitaji Msaada wa kinyota hapa
Jina langu linaanzia na R na nimezaliwa 20/06, Kuna wanawake wawili katika maisha yangu na wote majina yao yanaanzia na R, mmoja kazaliwa 01/01 na mwingine kazaliwa 11/10
Habari mkuu hapa na deal na nyota za mtu binafsi na kuchambua hapa ni free of charge lakini anaekuja p.m anatakiwa kunilipa elfu 5 ili kuweza kumchambulia lakini kwa hapa nafanya kama elimu ya kufundisha tu,
Na pia ili kuweza kuchambua mwenza mnaeendana nae kiukweli na sahihi zaidi itatakiwa unipe tarehe za kuzaliwa na majina ya wahusika maana humo kuna kutizama nyota zilizochomoza kwenye mwezi wakati unaandama sayari ya mapenzi,ndoa na ushirikiano na pia nyota za jua.

Ndio maana unaweza kukuta mtu ni adui yako kinyota lakini kafa kaoza kwako hapo inakuwa upendo huo unaunganishwa na nyota za mwezi, means mapenzi ya ndani, lakini nyota za jua ni mapenzi ya nje na nyota za sayari ni muunganisho wa mapenzi ya ndani na nje,

Ndio maana utakuta watu wanapendana kufa lakini wakikaa pamoja mapenzi yanakufa lakini pia kukurupuka wahindi huzingatia sana haya mambo Ndio maana hufanikiwa sana kasoro wapumbavu wachache miongoni mwao..

Rakims
 
Mkuu Rakims nimezaliwa 28/8/1987 jina linaanza na herufi A nyota yangu ni ipi?
 
Ahaaaa,,safi sana mkuu.nimekupata.
Ulichonambia nishawai kuota mkuu.shukran sana.
 
Mkuu Rakims nimezaliwa 28/8/1987 jina linaanza na herufi A nyota yangu ni ipi?
Kwa maelezo yako inaonekana ni virgo lakini kwa mujibu wa hiyo siku uliyozaliwa inaweza kuingia nyota inayofuata yaani mizani siwezi kujudge vizuri hilo hadi details za zijitosheleze
 
Kwa maelezo yako inaonekana ni virgo lakini kwa mujibu wa hiyo siku uliyozaliwa inaweza kuingia nyota inayofuata yaani mizani siwezi kujudge vizuri hilo hadi details za zijitosheleze
Kwn mkuu nyota c tunaangalia tarehe na mwezi wa kuzaliwa?
 
Kwn mkuu nyota c tunaangalia tarehe na mwezi wa kuzaliwa?
Hapana mkuu nyota kila mwezi unapozama na kuibuka zinageuka na pia mzunguko wa jua kwa mwaka unageuka kwa details ulizonipa nyota yako ni Mizani.
Ukiangalia kwenye hizo tarehe za wazungu watakwambia nyota yako ni Mashuke yaani ya 6 lakini kwa details ulizonipa kwa ujumla nyota yako ni Mizani ambayo ndio nyota ya kuifuata labda tutarudi nyuma kama utaulizia eneo na saa uliyozaliwa kupata uhakika zaidi maana nawasiwasi umechomozewa na nyota ya Punda kama tabia au mtizamo wa watu kwako

Rakims
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…