Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

S

Sijasema kuwa mie ni mashuke au natumia nyota zote mbili ila rising sign yangu(mashuke) ina nguvu kuliko simba, niliposema kuwa nyota zote zinatuhusu ni kwa maana ya kwenye planet zengine tuna nyota zengine pia.
Kwa maelezo hayo unakuwa upo sahihi pia lakini ukumbuke influence za nyota zinategemea na wakati mtu aliopo kwa kipindi hicho mpangilio ulikuwa vipi wakati anazaliwa

Rakims
 
IMI Mtaalam Bado ninshida katika Elimu hii tangu kipindi Cha sheh Yahaya jina la ASajile Imelda na tarehe 24-10-1990 vinaleta nyota mbili tofauti je kiunajimu sio kosa na kama nyota MOJA nifuate IPO jina au tarehe ya kuzaliwa
Mtu yoyote ambaye jina la tarehe zake nyota haziendani basi fahamu ya kuwa nyota zenye nguvu zaidi zinakinzana na nyota yake asilia ambapo mfano nyota ya muda uliyozaliwa huwa inaplay part kuwa kukuonyesha ndio wewe kuliko nyota yako ya asili.

Au nyota ya desire yako unakuta inashinda nyota ya asili yako, Hapa nikimaanisha nyota ya Mwezi
 
Rakims inakuwaje umeachana na mtu bado unakuwa unamuota Mara kwa Mara.
kuachana kwetu sio kwa ugomvi
Zingatia nyota zinazohusika na soul mate wa mtu. Unaweza kuwa mtu hamuendani lakini nyota zenu za kiroho zinakuwa zimeshafunga ndoa
 
Nyota ya mizani imepunjwa maelezo, kama vyakula na miji ya kuishi
Pole nitakuja kujazia nyama lakini kwa kifupi kwa nchi ni Burma, China, Tibet, Argentina na Japan ikiwa ni pamoja na vyakula vyakula vyake ni Samaki wa kukaanga, mikate, biscut na vinavyotokana na ngano sana.
 
Zingatia nyota zinazohusika na soul mate wa mtu. Unaweza kuwa mtu hamuendani lakini nyota zenu za kiroho zinakuwa zimeshafunga ndoa
We jamaa mchawi 😂😂utani lakni

Mpenzi wangu alikuwa nyota ya punda mimi scorpion niliwahi kukuuliza ukasema hamtadum ni kweli licha ya kupendana.

Chaajabu bado namuwazia sana. Mapenzi haya
 
Mimi Aries mpenzi wangu alikuwa Libra.. ni katika nyota zinaendana kimahusiano. Husiano alilivunja kimasihara pasipo na sababu ya msingi na ni husiano lilonipa maumivu makali kuliko mengine. Nimechukua muda sana kumtoa kichwani sijui kwanini
 
Kwa maelezo hayo unakuwa upo sahihi pia lakini ukumbuke influence za nyota zinategemea na wakati mtu aliopo kwa kipindi hicho mpangilio ulikuwa vipi wakati anazaliwa

Rakims
Je vp kuhusu herufi ya jina la mtu linahusiana vp na nyota?
 
Je vp kuhusu herufi ya jina la mtu linahusiana vp na nyota?
Huko ni kubashiri pekee hakuna uhusiano, Isipokuwa mara nyingi utakuwa herufi hiyo ya kwanza inaingia kwenye nyota iliyochomoza muda ambao mtu anazaliwa.

Rakims S.
 
Kaka una elimu kubwa
Ola watu wanasema ni shirki elimu hii ni kweli?
 
Kaka una elimu kubwa
Ola watu wanasema ni shirki elimu hii ni kweli?
Hiyo ni capacity yao ya uelewa wa mambo imeishia hapo hivyo huwezi kumuhukumu mtu kwa uelewa wake. Naweza kukujibu ni kweli na wengine wakaona ni kweli na wengine wasione ni kweli.

Muhimu hatulingani kama vidole ndio maana wapo wengi wasiojua na wachache wasiojua,.
Hata wenye kusema ni shirki kitabu chao kinasema: Nyota ni muongozo wa kiza cha bara na bahari na ishara hizi zimechambuliwa kwa watu wenye kujua.

Sasa asiyejua atakwambia nini mkuu? na yeye ni kiburi na kukubali kuwa hajui ni ligi mpya utabishana na mtu kisa ujinga wake?
Mwisho wa siku na wewe utaonekana mjinga tu.

Rakims
 
 
Huko ni kubashiri pekee hakuna uhusiano, Isipokuwa mara nyingi utakuwa herufi hiyo ya kwanza inaingia kwenye nyota iliyochomoza muda ambao mtu anazaliwa.

Rakims S.
Kwa maana hiyo hapo herufi ya jina la mtu inahusiano na nyota.
 
Sikupingi mkuu Japo inanitesa sana, ugonjwa mkubwa wa nyota yangu ni tumbo na linanisumbua sana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…