KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Behemoth ni kiumbe wa KIROHO mwenye sifa ya ulafi na anakula kila kitu pasipo kukoma. Anakula watoto wakiwa tumboni, unashangaa mimba zinatoka bila ya sababu yoyote, unazaa watoto wanakufa vifo vya mapema (pre mature death) etc.
Kwenye maandiko ya Biblia, kitabu kitakatifu cha Wakristo, Behemoth ametajwa kama "Alaye". Malaki 3:11
Naongea na wewe ambaye kila kitu cha thamani kinapoingia kwenye maisha yako au mikononi mwako lazima kitapotea...
💥Iwe umeanzisha biadhara nzuri mwisho wa siku inapotea...
💥Iwe umejenga nyumba nzuri lazima inapotea hata kwa kudaiwa kisha kuuza...
💥Iwe ni ndoa nzuri yaani mume au mke mwisho wa siku unampoteza kwa kuachana au kufa kabisa....
💥Iwe umepata kazi nzuri na yenye mshahara mzuri mwisho wa siku unajikuta umeipoteza kwa kufukuzwa au kujisikia kuacha mwenyewe...
💥Uwe ni mradi mzuri umeanzisha mwisho wake unapotea kabisa...
💥Uwe ni muunganiko mzuri na watu wenye faida kwenye maisha yako mwisho wa siku unapotea bila sababu maalum..
Mfano kuna mtu mmoja alipata muunganiko na wazungu na wakamuahidi kusapoti kampuni yake mwisho wa siku wakaopotea na kampuni ikafa...
💥Una mchumba wa maana kwenye kukuonyesha matumaini ya maisha ya mbele mwisho wa siku anapotea na kwenda kuoa mwingine au kuolewa na mwingine....
💥Una kibali mbele za watu Fulani lakini mwisho wa siku Kibali kinapotea na walewale watu wanaanza kukuchukia au kukukataa...
💥Una ndoto nzuri ambayo umeona itapeleka maisha yako mbele lakini mwisho wa siku huoni uzito wake tena au mzigo wa kuifanya...
💥Unajikuta una fedha nyingi na mwisho wa siku zinapotea bila ya kujua umefanyia nini kitu cha maana...
Ukiona unakabiliwa na hali kama hii ujue hiyo ni vita ya roho ya behemoth..
Lakini pia kuna aina ya watu kila anachoanza kufanya kwa mikono yake lazima kimeletee hasara yaani hajawahi kupata faida hata siku Moja, iwe kwenye biashara, KAZI, mradi, huduma na mahali penginepo....
Hii ni roho ya behemoth iliyoingia kwenye maisha yako...
Nini ufanye unapokabiliwa na shambulizi la roho ya Behemoth?
Kwa kuwa Behemoth ni mlafi sana wa kila kitu, inachotakiwa kufanya ni kujinyima wewe na kuwapa wengine.
Unajinyima kwa kufunga na kutoa sadaka za kila aina kwa wahitaji.. Naomba usome mistari hii michache itakufungua sana na kuishinda kabisa roho hii maishani mwako.
BHN
ISAYA 58
Mfungo wa kweli.
3“Nyinyi mnaniuliza:
‘Mbona tunafunga lakini wewe huoni?
Mbona tunajinyenyekesha, lakini wewe hujali?’
“Ukweli ni kwamba wakati mnapofunga,
mnatafuta tu furaha yenu wenyewe,
na kuwakandamiza wafanyakazi wenu!
4Mnafunga, na kugombana na kupigana ngumi.
Mkifunga namna hiyo
maombi yenu hayatafika kwangu juu.
5Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha;
mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi,
na kulalia nguo za magunia na majivu.
Je, huo ndio mnaouita mfungo?
Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?
6“La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu:
Kuwafungulia waliofungwa bila haki,
kuziondoa kamba za utumwa,
kuwaachia huru wanaokandamizwa,
na kuvunjilia mbali udhalimu wote!
7 Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako,
kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao,
kuwavalisha wasio na nguo,
bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.
8“Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko,
mkiwa wagonjwa mtapona haraka.
Matendo yenu mema yatawatangulia,
nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.
9Ndipo mtakapoomba,
nami Mwenyezi-Mungu nitawaitikia;
mtalia kwa sauti kuomba msaada,
nami nitajibu, ‘Niko hapa!’
“Kama mkiiondoa dhuluma kati yenu,
mkiacha kudharau wengine na kusema maovu,
10mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa,
mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki,
mwanga utawaangazia nyakati za giza,
giza lenu litakuwa kama mchana.
11Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima,
nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida.
Nitawaimarisha mwilini,
nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji,
kama chemchemi ya maji
ambayo maji yake hayakauki kamwe.
12Magofu yenu ya kale yatajengwa;
mtajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani.
Nanyi mtaitwa watu waliotengeneza upya kuta,
watu waliozifanya barabara za mji zipitike tena.