Ijue Sheria ya Mtoto. Uliza swali lolote kuhusu Sheria ya Mtoto

Ijue Sheria ya Mtoto. Uliza swali lolote kuhusu Sheria ya Mtoto

Amydiz

Member
Joined
Mar 28, 2017
Posts
37
Reaction score
27
Mtoto ni mtu yeyote aliye na umri chini ya miaka 18, kutokana na kifungu cha 4 (1) cha Sheria ya Mtoto ya Tanzania ya mwaka 2009. Mtoto ana haki kama mtu mwingine (adult). Haki kama ya kupiga kura, mtoto hana. Hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 5 (1) ya Katiba ya Tanzania.

Sheria ya mwaka 2009 ya Mtoto inaeleza haki za mtoto kwamba ni pamoja kupata elimu, chakula bora, kulindwa dhidi ya ubaguzi, huduma za afya, uhuru wa kuamua na kushirikishwa katika kuamua mambo pamoja na kupumzika.

===

1572238698679.png

Haki za Mtoto kwa Mujibu wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009

➣ Haki ya kuishi (kifungu cha 9)

➣ Haki ya kupumzika

➣ Haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa (kifungu cha 9 (3)(a)

➣ Haki ya kutokubaguliwa (kifungu cha 5)

➣ Haki ya jina na utaifa (kifungu cha 6)

➣ Haki ya kuishi na wazazi wake (kifungu cha 7)

➣ Haki ya kupata huduma bora za elimu, malazi matibabu kwa ajili ya ustawi wake

➣ Haki ya kushiriki michezo na shughuli za kiutamaduni kifungu cha 9 (2)

➣ Haki ya huduma za pekee kwa walemavu

➣ Haki ya kunufaika na kutumia kwa uangalifu mali za wazazi wake (kifungu cha 10)

➣ Haki ya kutoa maoni, mawazo kusikilizwa na kutoa maamuzi ya ustawi wake (kifungu cha 11)

➣ Haki ya kutoajiriwa katika ajira zenye madhara (kifungu cha12)

➣ Haki ya kulindwa dhidi kudhalilishwa kijinsia.

Wajibu wa jumla wa Mtoto pamoja na haki za mtoto pia anawajibika katika maeneo yafuatayo:

➣ Kufanya kazi kwa ajili ya mshikamo wa familia (kifungu cha 15 (a)

➣ Kuwaheshimu wazazi, walezi, wakubwa wake wote na atawasaidia pale inapohitajika (kifungu cha 15(b)

➣ Kuhudumia jamii yake na taifa lake kwa uwezo wake wote kimwili na kiakili kadiri ya umri na uwezo wake

➣ Kutunza na kuimarisha mshikamo wa jamii na taifa(kifungu cha 15(d)

➣ Kutunza kuimarisha mambo mema ya utamaduni wa jamii na taifa kwa ujumla katika uhusiano na wanajamii au taifa(kifungu cha 15(e)

➣ Mtoto yeyote aliyepata mafunzo ya ufundi anawajibu wa kufuatilia kwa makini na kukubali kwa uaminifu, mafunzo aliyopewa na Mwalimu kwa kuhudhuria mafunzo na kuzuia uharibifu wowote wa makusudi na kutoharibu mali za mtoa mafunzo (kifungu cha 15(c)

Sababu za kuwa na ulinzi wa haki za mtoto ni pamoja na

- Watoto ni binadamu, wana haki sawa

- Watoto hawana sauti ya kujisemea au hawana uwezo wa kupigania haki zao wenyewe

- Kuwepo kwa wimbi kubwa la ukiukwaji wa haki za watoto mfano ukatili dhidi ya mtoto, utesaji na ubakaji

Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 inashughulikia haki za watoto Tanzania. Sheria hii inajumuisha mambo mbalimbali ya kukuza, kulinda, na kuhifadhi ustawi wa mtoto; masharti ya unajibishaji wa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa; masuala ya kulea, kuasili na uangalizi. Pia inatoa maelekezo na masharti yanayohusu mtoto anapokuwa katika mgogoro na sheria.

Sheria hii inatumika kutetea masuala yote ya kuboresha, kulinda na kuhifadhi ustawi wa mtoto pamoja na haki zake.

Kwa mujibu wa sheria hii mtoto ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka kumi na nane. Sheria hii inafanunua zaidi kuwa mtoto ni pamoja na mtoto yatima, mtoto aliye katika mazingira magumu, mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa, mtoto wa kuasiliwa, na mtoto anayelelewa katika vituo vya kulelea watoto.

Chanzo: Haki na Wajibu wa Mtoto kisheria kulingana na sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009
 
Last edited:
Kwa wazazi ambao wametengana, upi ndio umri sahihi unaokubalika kisheria wa baba kumchukua mwanae?

Kifungu cha 26( 2 ) cha Sheria ya mtoto, namba 21 ya 2009 kinasema kuwa ni vizuri mtoto aliye chini ya umri wa miaka saba akae na mama. Hata hivyo ni vema kufahamu kuwa kifungu hiki hakikusema ni lazima( shall) mtoto wa umri huo akae na mama.
Kifungu kinasema suala la mtoto chini ya umri wa miaka saba kukaa na mama ni dhana inayoweza kutozingatiwa( rebuttable presumption). Ni dhana inayoweza kutozingatiwa kwa maana kuwa zipo sababu ambazo mtoto chini ya umri huo inaweza kuamuliwa kukaa na baba au mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kufaa zaidi kuliko mama.
Kwahiyo lazima tuzingatie kuwa sio lazima mtoto chini ya umri wa miaka 7 kukaa na mama.

Pia nivizur uelewe kuwa sehemu ya kwenda kudai haki yako hiyo ya kukaa na mtoto ni
•mahakamani
•ustawi wa jamii

Pia kitu kikubwa kinacho zingatiwa n Kama huyo mtoto anaweza kujieleza atachagua pakukaa either kwa baba au kwa mama, Na mahakama itabariki uteuzi huo au laa
UNAWEZA UKAULIZA TENA KWA UFAFANUZI ZAIDI
 
Je watoto wa nje ya ndoa haki zao ni ni zipi? Mf. Elimu, afya, malazi??? Kama baba ana mtoto ambae kamzaa nje ya ndoa anawajibikaje katika hili?
Pia sheria imamlindaje mama wa mtoto (ambae hana ndoa na huyu baba) dhidi ya vitisho na unyanyasaji kutoka kwa mzazi mwenzie anapotakiwa kutoa matunzo tajwa?
Kuna sheria inayombana baba kutoa maana saa nyingine hawatoi kwa wakati au pungufu na makubaliano.
 
Muulizwa naona ametoka, ngoja arudi kwani nami nasubiri majibu.
 
Je watoto wa nje ya ndoa haki zao ni ni zipi? Mf. Elimu, afya, malazi??? Kama baba ana mtoto ambae kamzaa nje ya ndoa anawajibikaje katika hili?
Pia sheria imamlindaje mama wa mtoto (ambae hana ndoa na huyu baba) dhidi ya vitisho na unyanyasaji kutoka kwa mzazi mwenzie anapotakiwa kutoa matunzo tajwa?
Kuna sheria inayombana baba kutoa maana saa nyingine hawatoi kwa wakati au pungufu na makubaliano.
Kwanza kabisa kuhusu haki za mtoto wa nje ya ndoa,
mtoto wa nje ya ndoa Ana haki sawa Kama mtoto yeyote. Kwan Sheria ya mtoto (the law of the child Act) ya 2009, kifungu Cha 5 imekataza mtoto asibaguliwe kivyovyote vile.
Pili kuhusu kutunza mtoto
kuhusu malezi ya mtoto n jukumu la Baba na mama wa mtoto kumtunza mtoto wao, hii n kutokana na Sheria ya ndoa( the law of marriage Act) [Cap 29 R.E 2002] kifungu Cha 1291&2 ,
Pia mahakama inamamlaka ya kumuamuru anaye daiwa kuwa baba wa mtoto (biological father) kumtunza mwanae hii ni kwa mujibu wa sheria ya mtoto ( the law of the child Act)2009 chini ya kifungu Cha 43(1)
Pia kwenye kesi ya Omari Mahita V Rehema Shabani, mahakama ilimwamuru baba wa mtoto aliye zaliwa nje ya ndoa aitwaye Juma Omari Mahita ( mtoto) atoe matunzo ya mtoto wake

Kwakuongezea hapo, kwa kesi za baba kutokutoa matumizi ya mtoto ni vyema kwa mama kumpeleka mzazi mwenzie ustawi wa jamii au mahakaman na kudai matunzo ya mtoto, Kwan baba wa mtoto anawajibu wa kumtunza mtoto wake. Na hii haijalixhi hata Kama mtoto huyo amezaliwa nje ya ndoa
 
Kifungu cha 26( 2 ) cha Sheria ya mtoto, namba 21 ya 2009 kinasema kuwa ni vizuri mtoto aliye chini ya umri wa miaka saba akae na mama. Hata hivyo ni vema kufahamu kuwa kifungu hiki hakikusema ni lazima( shall) mtoto wa umri huo akae na mama.
Kifungu kinasema suala la mtoto chini ya umri wa miaka saba kukaa na mama ni dhana inayoweza kutozingatiwa( rebuttable presumption). Ni dhana inayoweza kutozingatiwa kwa maana kuwa zipo sababu ambazo mtoto chini ya umri huo inaweza kuamuliwa kukaa na baba au mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kufaa zaidi kuliko mama.
Kwahiyo lazima tuzingatie kuwa sio lazima mtoto chini ya umri wa miaka 7 kukaa na mama.

Pia nivizur uelewe kuwa sehemu ya kwenda kudai haki yako hiyo ya kukaa na mtoto ni
•mahakamani
•ustawi wa jamii

Pia kitu kikubwa kinacho zingatiwa n Kama huyo mtoto anaweza kujieleza atachagua pakukaa either kwa baba au kwa mama, Na mahakama itabariki uteuzi huo au laa
UNAWEZA UKAULIZA TENA KWA UFAFANUZI ZAIDI
Mimi nimeuliza hivyo mkuu kwasababu nina matatizo makubwa na mzazi mwenzangu, kutokana na changamoto hizo nashindwa kumuhudumia mwanangu, kwa sasa mtoto ana miaka minne, mimi nimeoa tayari, kila nikijaribu kufanya mawasiliano na mzazi mwenzangu ili nitoe matumizi ya mtoto naambulia matusi na kejeli, huu ni mwaka ww pili sasa sitoi chochote na sijafanikiwa kumuona mtoto, mtoto yuko dar mimi kwa sasa nafanya shughuli zangu mikoani, nichukue hatua gani niweze kumpata mwanangu?
 
Ni adhabu gani itatolewa na Mahakama iwapo baba atachelewa kutoa matumizi ya mtoto au akikaidi amri ya Mahakama ya kumhudumia mtoto?
 
Ni adhabu gani itatolewa na Mahakama iwapo baba atachelewa kutoa matumizi ya mtoto au akikaidi amri ya Mahakama ya kumhudumia mtoto?
Swali zuri sana, shida mtoa post hatumuoni hapa akitusaidia ufanunuzi kwenye baadhi ya hoja.
 
Mimi nimeuliza hivyo mkuu kwasababu nina matatizo makubwa na mzazi mwenzangu, kutokana na changamoto hizo nashindwa kumuhudumia mwanangu, kwa sasa mtoto ana miaka minne, mimi nimeoa tayari, kila nikijaribu kufanya mawasiliano na mzazi mwenzangu ili nitoe matumizi ya mtoto naambulia matusi na kejeli, huu ni mwaka ww pili sasa sitoi chochote na sijafanikiwa kumuona mtoto, mtoto yuko dar mimi kwa sasa nafanya shughuli zangu mikoani, nichukue hatua gani niweze kumpata mwanangu?
Wakati mnazaa ulikua umeshaoa ? Au bado ....
 
Hapana mkuu, ila nilikuwa na mahusiano na mwanamke wangu wa sasa na alikuwa anajua.
Muache kuchezea hisia za watu kama ulikua na mahusiano yeye ulikua nae kwa ajili gani..... Na ukute kipind ana mimba you mis treated her afu utegemee akijifungua ajilambe lambe kwako kisa child support !!!!!! Pole
Kua na amani huko mlipo Mungu atawabariki watoto
 
Ushauri wa hovyo kabisa huu, inaonyesha na wewe ni muathirika wa child support, nilimhudumia mtoto vizuri mpaka alipofikisha miaka miwili, naona umepata sehemu ya kupunguzia hasira zako.
 
Mimi nimeuliza hivyo mkuu kwasababu nina matatizo makubwa na mzazi mwenzangu, kutokana na changamoto hizo nashindwa kumuhudumia mwanangu, kwa sasa mtoto ana miaka minne, mimi nimeoa tayari, kila nikijaribu kufanya mawasiliano na mzazi mwenzangu ili nitoe matumizi ya mtoto naambulia matusi na kejeli, huu ni mwaka ww pili sasa sitoi chochote na sijafanikiwa kumuona mtoto, mtoto yuko dar mimi kwa sasa nafanya shughuli zangu mikoani, nichukue hatua gani niweze kumpata mwanangu?
Pole kwanza kwa matatizo, lkn kesi Kama yakwako n Jambo la busara kwanza kuyaongea kifamilia. Kama imeshindikana nenda ustawi wa jamii, ambapo huyo mlalamikiwa ataweza kufika. Na Kama itashindikana Basi itapelekwa mahakaman na mtapata haki zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria inasemaje mwanamke akiamua kusema mtoto sio wakwako wakati wewe unafahamu kwamba mtoto ni wa kwako..
Japokuwa hujawai kumlea tokea mwanamke akiwa na mimba
 
Alixhakupaga taarifa yakuwa mimba n yakwako
Sheria inasemaje mwanamke akiamua kusema mtoto sio wakwako wakati wewe unafahamu kwamba mtoto ni wa kwako..
Japokuwa hujawai kumlea tokea mwanamke akiwa na mimba

#97blessed
 
Mtoto n mtu yeyote aliye na umri chini ya miaka 18, kutokana na kifungu Cha 4(1) Cha Sheria ya mtoto ya Tanzania ya 2009,
Mtoto anahaki Kama mtu mwingine (adult),
haki Kama ya kupiga kura
mtoto hana, hi n kwa mujibu was ibara ya 5(1) ya katiba ya Tanzania

Sheria ya mwaka 2009 ya mtoto inaeleza haki za mtoto kwamba ni pamoja kupata
elimu,
chakula bora,
kuliindwa dhdi ya ubaguzi,
huduma za afya,
uhurua wa kuamua na kushirkishwa katika kuamua mambo pamoja na kupumzika.
Mimi naomba kujua sheria ya adoption Tanzania inamlindaje mtoto? Je wizara inayohusika na watoto pamoja na ustawi wa jamii huwa ina-adopt? Na kama inaadopt ni kifungi kipi cha sheria ya mtoto kinaeleza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom