Ijue Siri ya Crypto-Currency

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,932
Reaction score
13,306
Rais wetu mpendwa mama Samia ametoa agizo kwa BOT ianze mchakato wa kuruhusu Sarafu za mtandaoni zinazojulikana kama Crypto-Currency au virtual money zianze kutumika.

Wakati kuna baadhi ya mataifa makubwa Kama China hayataki matumizi ya sarafu hizo. Rais Samia alikuwa sahihi kabisa kuruhusu matumizi ya Crypto-currency kwa nchi yetu kwa sababu sarafu hizo ni sawa na Dhahabu hubadilisha maisha ya mtu ghafla, kutoka kwenye umaskini wa kutupwa hadi kuwa Bilionea wa kutupwa.

Mataifa makubwa yanaogopa kuruhusu matumizi ya Crypto-currency kwa sababu ya kuhofia anguko la uchumi wao.

KWANINI MATAIFA MAKUBWA YANAOGOPA CRYPTO-CURRENCY?
Mataifa makubwa yanaogopa kuruhusu matumizi ya Crypto-currency kwa sababu yana viwanda vingi ambavyo vinahitaji nguvu kazi ya vijana ,kwa hiyo inapotokea vijana wamejua Crypto-currency itawafanya wakae mbali na vibarua vya viwandani kazi zingine ngumu.
Kwa Taifa maskini kupindukia kama Tanzania, Crypto-currency ni Sarafu salama ya kutengenezea mtaji.

MTU ANAPATAJE MTAJI KUPITIA CRYPTO-CURRENCY?
Sarafu ya kwanza ya mtandaoni ni Bitcoin ambayo hadi sasa inatumika na ndo sarafu yenye Thamani kuliko zote Duniani, Bitcoin moja sasa hivi ni sawa na Tsh 136,000,000. Wakati inaanza, Bitcoin moja iliuzwa Tsh 200, wat wengi mno waliibeza ,na walionunua na kutunza leo hii ni matajiri

Baada ya mafanikio ya Bitcoin, zilianzishwa Sarafu nyingi pote Duniani.ingia hapa uzione[emoji116]coinmakertcap.com
Unanunua kwa bei sawa na Bure baada ya miezi kadhaa au miaka inapanda bei na kukutajirisha kabisa.

Thamani yake hupanda kulingana na jinsi watu wanavyoinunua,watu wakiwa wengi zaidi na Thamani yake inakuwa kubwa zaidi. Sarafu hizi hutumika kwenye manunuzi kimataifa na pia unaweza kuziuza na kuchukua Fedha Taslimu. Nimeeleza kifupi sana kwa sababu ya muda.
 
Faycat tower kuna kampuni pale wakobusy sana na hilo jambo muda muafaka twende tukajifunze .....dunia yaenda mbiovsana.....baada miaka 10 tutakuwa behind the running world tusipokuwa makini
 
Ni kweli kabisa Crypto ni fursa kubwa sana kwa vijana sio lazima umiliki coin nzima ya btc au altcoin yoyote unaweza kudunduliza pole pole
Ushauri wangu kwa vijana wenzangu wekeza kwenye btc hii inapanda thamani haraka sana kuliko uweke bank fixed upate riba ndogo
 
Kama watu walivojuta miaka 5 iliopita ndivo watakavojuta ikifika 2025 maana inasemekana kwa mwaka huu BTC itafika USD100K na Ethe itakuwa USD10K pia tuitafute elimu sana ya hii inshu maana haiepukiki wazee ndo Dunia ijayo hii...
 
Duh!!!,Ilitakiwa kabla ya kuingiza sarafu hii, Wananchi wapewe Elimu ya kutosha kwanza.
 
Wazee wa crypto wanachezea mbata kali sokoni

Wapo waliochoma mitaji.

Wapo ambao mitaji inahemea Oxygen.

Yule nguli wa kuhamasisha crypto kule Twitter ambae hapo awali aliwahi kuwa mdau wa Fx kaamua apotee hewani bila shaka mambo sio mambo

Cry-pto holders are crying [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

At the first i never believed in cryptos i knew this gonna be the greatest financil scam ever happen.

Billions of dollars are wiped

Government will never allow this shit to take over completely,which means they have to lose financial ground.
 
That will be full of shit.

Siku akifa au server zako zikiwa corrupted na pesa zenu zimekwenda
In short, Cryptos in dalili zote kuwa ni SCAM, some sort of Ponzi scheme.

Kwanza ukishanunua Cryptos inabidi sasa uanze kufanya marketing na kuitetea kwa nguvu zote. Maana it works on demand and supply.

Wafuasi wa me wanakwambia ni future of money against fiat money lakini wakati huo huo wanataka serikali izihalalishe??
 
Kama watu walivojuta miaka 5 iliopita ndivo watakavojuta ikifika 2025 maana inasemekana kwa mwaka huu BTC itafika USD100K na Ethe itakuwa USD10K pia tuitafute elimu sana ya hii inshu maana haiepukiki wazee ndo Dunia ijayo hii...
The price of bitcoin is plugging deep in dip[emoji2] sitegemei ikifika 100k $ this year

Still ni bear market
 
Ushauri wangu ni kununua altcoin iliyo chini na yenye future na ununue za kutosha.
2017 nilianza kama utani.
Jamaa yangu niliyemfundisha fx alinilazimisha nijaribu altcoins..nilimpinga mno.
Akasema nunua kidogo tu.
Nilinunua za $200 na ilikuwa 15/11/2017.

Nilishangaa ilipofika December 20/2017 ilipanda hadi $7,000[emoji849][emoji849][emoji849].

Nilifanikiwa kuuza za $2,500

Na ilipofika January ilishuka sana hadi $500

Muda huu ninapoandika inasoma B na point.

Tatizo wateja kwasasa ni wachache.
Najua baadae tutatafutana.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
The price of bitcoin is plugging deep in dip[emoji2] sitegemei ikifika 100k $ this year

Still ni bear market
Kila kitu ni kurisk mkuu.
Hata kula tu tuna risk.
Ukiogopa sana kila kitu ni kwa hasara yako.

Mimi binafsi nina washkaji zangu wanenishauri sana miaka nenda rudi kununua Bitcoin nimegoma tangu ikiwa $6,000.

Zaidi niliinunua kwa kuitumia kufanya manunuzi kama $ lkn sio ku hold.
Lakini mwaka jana jamaa alipata pesa nyini hadi 136ml/ bitcoin lkn bado sijavutiwa nayo..

Kupanga ni kuchagua.
Mule mule kuna wanaonunua na inashuka ghafla wanafilisika mazima lkn kuna wanao ngang'ang'ania na wanatoboa..
Maisha ndivyo yalivyo hayana kanuni maalum kutoboa.

Hivyo tusiwalaumu wanunuzi na wasio nunua kila mtu yuko sawa

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mambo ya mining project nyingi huishia njiani.
Bora kushauri mtu kununua kuliko mambo ya mining

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Mkuu inategemea na project inaanzishwa na nani. Hii program inaanzishwa na Remitano. Tayari wana jina zuri kwa miaka mingi. Sidhani kama wataweza kuanzisha kitu kitakachowaharibia jina. Mpaka sasa wanaenda sambamba na ratiba/muongozo (roadmap) na hakuna walichobadilisha. Ili kuwashauri watu wanunue inabidi nitoe darasa la kutosha kwanza kabla mtu hajaweka pesa yake kitu ambacho sitaweza. Kwa hiyo nawashauri kitu ambacho ni bure hivyo hana cha kupoteza hata kama kaingia bila maarifa sahihi.
 
Hongera sana mkuu. Huu ndio ushuhuda tunahitaji kuusikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…