*IJUE TIMU YA AS VITA CLUB - DRC CONGO MPINZANI WA PILI WA SIMBA*
*HISTORIA FUPI*
AS Vita club ni timu iliyopo katika viunga vya jiji la Kinshasa nchini Congo DRC na imeanzishwa 1935 ikiwa inaitwa Reneissance baadae 1939 ikabadilishwa ikaitwa Victoria Club na 1971 ndio ikabadilika kuwa Association Sportive Vita Club Kifupi As Vita Vita jina lake la utani ni Black Dolphins.
Uwanja wake inaoutimia unaouwezo wa kuingiza watazamaji 30,000 unaitwa Boulevard Sendwe Kalamu (Nyasi bandia). Ila mechi kubwa zote inatumia uwanja wa Taifa kwa ajili ya mashabiki wao wengi sana wanajivunia kwa hilo wakiwa nyumbani huwa uwanja unatabika kabisa ni OMNISPORTS STADE DE MARTYRS una wezo wa watazamaji 80,000.
*VIKOMBE*
Imechukua kombe la Ligi kuu kwao LINAFOOT mara 14.
Caf Champion League imeshiriki mara 14 na kuwa bingwa 1974, Runner Up 1982 na 2014, Semi final 1978.
Caf Confederation Cup ameshiriki mara 4 ambazo group stage 2008, 2009 na 2010 halafu Runner Up 2018.
Wanachezaji wakigeni 3 tu ambao ni
1. Nelson Lukong (Goalkeeper) - Cameroon
2. Oumar Sidibe (Attacking midfielder) - Mali
3. Akwo Ayuk (Forward) - Cameroon
*WACHEZAJI*
Katika kikosi Chao kuna Redcard moja kwa Mondia Kalonji (Centre Back) ndio hawezi kucheza.
Katika wachezaji wote kuna wachezaji hatari sana ambao mara nyingi ndio waanzishaji au wamaliziaji wa mpira
FORWARD
Kuna watu hawa Jean Makusu na Mundele
WINGER/MIDFIELDER
Lukombe na Kazadi Kasungu
ATTACKING MIDFIELDER
Ngoma na Kasengu
BACK/CENTRE/MIDFIELDER
Munganga na Tonombe
*MFUMO*
Kocha wao Florent Ibenge ni mpenzi wa soka la speed mwanzo mwisho na hasa wanapokuwa Away na ndio maana matokeo yao mengi wanapatia nyumbani sio ugenini na mfumo wao ni home 4-3-3 na Away 4-5-1.
Katika percentages wao ni 20% kwa kipindi vyote vitano wapo hivyohivyo hawabadiliki.
*MATOKEO YA MECHI*
*LINFOOT*
Mpaka sasa katika ligi yao DRC yenye timu 15 mzunguko wakwanza umeshamalizika kola timu imecheza medhi 14.
As Vita IPO nafasi ya 2 na ina points 35.
Mechi 14 home 6 Away 8
Win. 11 home 5 Away 6
Draw. 2 home 1 Away 1
Losses 1 home 0 Away 1
Goal For 29 home 13 Away 16
Goal Against 8 home 3 Away 5
*CHAMPION LEAGUE*
Katika Michuano hii mpaka sasa amecheza
Mechi 3 home 1 Away 2
Win. 1 home 1 Away 0
Draw. 1 home 0 Away 1
Losses 1 home 0 Away 1
Goal For 5 home 4 Away 1
Goal Against 2 home 0 Away 2
Toka June 2017 hadi sasa amecheza jumla 11 Match za Champion League na Confederation Cup Nyumbani na hawajawahi kufungwa.
*REFEREES*
Katikati ni Mohamadou Keita - Mali.
1st Asst. Seydou Tiama - Burkinafaso
2nd Asst. Sidiki Sidibe - Guinea
*LOCATION*
Mji wa Kinshasa upo mbali sana toka tulipo hivyo ni ngumu sana kwenda kwa njia ya gari maana miundombinu yake ni migumu sana kupitika njia salama ni lazima kupitia Angola via Kitwe Zambia napo ni 4600km. Njia ya Kupitia Lubumbashi kwenda mbuji Maji haifai sio salama.
Kifupi DSM mpaka Kinshasa Kinshasa Kinshasa kuliko DSM kwenda Lesotho mazingira yote, Usafiri pekee wenye afya ni kwa Ndege tu basi.(Simba inaondoka Alhamisi hii)
*MWISHO*
Tunajua mechi hii ngumu kama Taifa na kama Simba ila ni muhimu katika kupata matokeo ya aina yeyote chanja kwa maana ya point zozote zile kila la heri Simba katika mechi hii muhimu sana.
*YES WE CAN*
Sent using
Jamii Forums mobile app