Ijue tofauti ya Wakili na Mwanasheria

Ijue tofauti ya Wakili na Mwanasheria

Bashir Yakub

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
96
Reaction score
1,745
IJUE TOFAUTI YA WAKILI NA MWANASHERIA.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Kila Wakili ni Mwanasheria , lakini si kila Mwanasheria ni Wakili. Wakili ni zaidi ya Mwanasheria. Ili uwe Wakili unaanza kuwa Mwasheria.

Mwanasheria ni mtu yeyote aliyesoma kozi ya sheria katika chuo kinachotambulika, na kuhitimu, na kufaulu, na kupata shahada ya sheria LLB.

Huyu sasa ndie anaitwa Mwanasheria. Moja ya kazi anazoweza kufanya ni pamoja kutoa ushauri wa kisheria katika baadhi tu ya mambo.

Wakili. Huyu ni mtu yeyote aliyesoma kozi ya sheria katika chuo kinachotambulika, na kuhitimu, na kufaulu, na kupata shahada ya sheria LLB.

Kisha baada ya kupata shahada hiyo ya Sheria@LLB akajiunga na kusoma Shule ya Sheria kwa Vitendo@Law School, akafanya mitihani na kufaulu, kisha akaapishwa na Jaji Mkuu na hivyo kuitwa WAKILI.

Kwahiyo Uwakili ni hatua ya pili baada ya Uanasheria. Unaanza kuwa Mwanasheria, kisha unakuwa Wakili.

Kazi anazoweza kufanya Wakili ni pamoja na Kumuwakilisha mtu mahakamani, kutoa ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka za kisheria, kuruhusiwa kufungua ofisi ya uwakili, kusimamia mikataba ya aina yote , kumiliki muhuri n.k.

Hizi kazi kama Kumuwakilisha mtu mahakamani, kuandaa baadhi ya nyaraka za kisheria, kuruhusiwa kufungua ofisi ya uwakili, kusimamia mikataba nk haruhusiwi kufanya Mwanasheria.

Mwanasheria hawezi pia kumiliki muhuri. Na ndio maana muhuri huo huwa umeandikwa ADVOCATE(WAKILI), na sio LAWYER( MWANASHERIA).

Wapo Wanasheria ambao sio mawakili ambao hujitambulisha kama Mawakili na hivyo kufanya kazi za mawakili, yumkini huwa ni makosa makubwa.

Na unajuaje kuwa huyu ni Wakili ama si Wakili. Ni rahisi sana, andika neno "eWAKILI" kwenye Google.

Itakuletea eneo la kuandika jina la mtu unayemtafuta. Andika jina la mtu huyo eneo hilo kisha bofya neno "TAFUTA/SEARCH".

Kama mtu huyo ni Wakili itakuletea jina na picha yake na kama si Wakili jina na picha havitatokea na itakuandikia, "Hakuna Wakili Aliyepatikana".

Basi, kila Wakili ni Mwanasheria lakini si kila Mwanasheria ni Wakili.
 
Shukrani kwa elimu hii, lakini ningependa kujua ppia kuhusu hakimu na jaji inakuaje na wao?
 
Wakili na Wanasheria ndo wanaharibu sheria.
Husije kusahau ilo abadani.
 
IJUE TOFAUTI YA WAKILI NA MWANASHERIA.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Kila Wakili ni Mwanasheria , lakini si kila Mwanasheria ni Wakili. Wakili ni zaidi ya Mwanasheria. Ili uwe Wakili unaanza kuwa Mwasheria.

TZ Ma-Bush Lawyer wengi saaaana, alafu wanapiga vishoka balaaa
 
IJUE TOFAUTI YA WAKILI NA MWANASHERIA.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Kila Wakili ni Mwanasheria , lakini si kila Mwanasheria ni Wakili. Wakili ni zaidi ya Mwanasheria. Ili uwe Wakili unaanza kuwa Mwasheria.
Asante kwa elimu. Unaruhusu kuombwa ushauri wa kisheria?
 
Na ndio kozi inayoongoza kwa kudisco wanafunzi, yaani hiyo kozi ni kama Squid game kimya kimya raia wanaondoka mkija mkimaliza ni wachache na GPA zinaning'inia
 
IJUE TOFAUTI YA WAKILI NA MWANASHERIA.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Kila Wakili ni Mwanasheria , lakini si kila Mwanasheria ni Wakili. Wakili ni zaidi ya Mwanasheria. Ili uwe Wakili unaanza kuwa Mwasheria.

Mwanasheria ni mtu yeyote aliyesoma kozi ya sheria katika chuo kinachotambulika, na kuhitimu, na kufaulu, na kupata shahada ya sheria LLB.

Huyu sasa ndie anaitwa Mwanasheria. Moja ya kazi anazoweza kufanya ni pamoja kutoa ushauri wa kisheria katika baadhi tu ya mambo.

Wakili. Huyu ni mtu yeyote aliyesoma kozi ya sheria katika chuo kinachotambulika, na kuhitimu, na kufaulu, na kupata shahada ya sheria LLB.

Kisha baada ya kupata shahada hiyo ya Sheria@LLB akajiunga na kusoma Shule ya Sheria kwa Vitendo@Law School, akafanya mitihani na kufaulu, kisha akaapishwa na Jaji Mkuu na hivyo kuitwa WAKILI.

Kwahiyo Uwakili ni hatua ya pili baada ya Uanasheria. Unaanza kuwa Mwanasheria, kisha unakuwa Wakili.

Kazi anazoweza kufanya Wakili ni pamoja na Kumuwakilisha mtu mahakamani, kutoa ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka za kisheria, kuruhusiwa kufungua ofisi ya uwakili, kusimamia mikataba ya aina yote , kumiliki muhuri n.k.

Hizi kazi kama Kumuwakilisha mtu mahakamani, kuandaa baadhi ya nyaraka za kisheria, kuruhusiwa kufungua ofisi ya uwakili, kusimamia mikataba nk haruhusiwi kufanya Mwanasheria.

Mwanasheria hawezi pia kumiliki muhuri. Na ndio maana muhuri huo huwa umeandikwa ADVOCATE(WAKILI), na sio LAWYER( MWANASHERIA).

Wapo Wanasheria ambao sio mawakili ambao hujitambulisha kama Mawakili na hivyo kufanya kazi za mawakili, yumkini huwa ni makosa makubwa.

Na unajuaje kuwa huyu ni Wakili ama si Wakili. Ni rahisi sana, andika neno "eWAKILI" kwenye Google.

Itakuletea eneo la kuandika jina la mtu unayemtafuta. Andika jina la mtu huyo eneo hilo kisha bofya neno "TAFUTA/SEARCH".

Kama mtu huyo ni Wakili itakuletea jina na picha yake na kama si Wakili jina na picha havitatokea na itakuandikia, "Hakuna Wakili Aliyepatikana".

Basi, kila Wakili ni Mwanasheria lakini si kila Mwanasheria ni Wakili.
Naomba kuuliza..je endapo mtu ana shahada ya taaluma nyingine..na anapenda kuwa mwanasheria hatimaye kuwa wakili utamshauri afanye nini..ukizingatia kuna postgraduate ya sheria..je apitie njia gani? Ambayo ni rahisi.

#MaendeleoHayanaChama
 
IJUE TOFAUTI YA WAKILI NA MWANASHERIA.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Kila Wakili ni Mwanasheria , lakini si kila Mwanasheria ni Wakili. Wakili ni zaidi ya Mwanasheria. Ili uwe Wakili unaanza kuwa Mwasheria.

Mwanasheria ni mtu yeyote aliyesoma kozi ya sheria katika chuo kinachotambulika, na kuhitimu, na kufaulu, na kupata shahada ya sheria LLB.

Huyu sasa ndie anaitwa Mwanasheria. Moja ya kazi anazoweza kufanya ni pamoja kutoa ushauri wa kisheria katika baadhi tu ya mambo.

Wakili. Huyu ni mtu yeyote aliyesoma kozi ya sheria katika chuo kinachotambulika, na kuhitimu, na kufaulu, na kupata shahada ya sheria LLB.

Kisha baada ya kupata shahada hiyo ya Sheria@LLB akajiunga na kusoma Shule ya Sheria kwa Vitendo@Law School, akafanya mitihani na kufaulu, kisha akaapishwa na Jaji Mkuu na hivyo kuitwa WAKILI.

Kwahiyo Uwakili ni hatua ya pili baada ya Uanasheria. Unaanza kuwa Mwanasheria, kisha unakuwa Wakili.

Kazi anazoweza kufanya Wakili ni pamoja na Kumuwakilisha mtu mahakamani, kutoa ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka za kisheria, kuruhusiwa kufungua ofisi ya uwakili, kusimamia mikataba ya aina yote , kumiliki muhuri n.k.

Hizi kazi kama Kumuwakilisha mtu mahakamani, kuandaa baadhi ya nyaraka za kisheria, kuruhusiwa kufungua ofisi ya uwakili, kusimamia mikataba nk haruhusiwi kufanya Mwanasheria.

Mwanasheria hawezi pia kumiliki muhuri. Na ndio maana muhuri huo huwa umeandikwa ADVOCATE(WAKILI), na sio LAWYER( MWANASHERIA).

Wapo Wanasheria ambao sio mawakili ambao hujitambulisha kama Mawakili na hivyo kufanya kazi za mawakili, yumkini huwa ni makosa makubwa.

Na unajuaje kuwa huyu ni Wakili ama si Wakili. Ni rahisi sana, andika neno "eWAKILI" kwenye Google.

Itakuletea eneo la kuandika jina la mtu unayemtafuta. Andika jina la mtu huyo eneo hilo kisha bofya neno "TAFUTA/SEARCH".

Kama mtu huyo ni Wakili itakuletea jina na picha yake na kama si Wakili jina na picha havitatokea na itakuandikia, "Hakuna Wakili Aliyepatikana".

Basi, kila Wakili ni Mwanasheria lakini si kila Mwanasheria ni Wakili.
Je Wakili kuna tofaut ipi kat yule mwanasheria ambaye amefanya school of law na usajili wake ukasoma " ameruhusiwa kutoa viapo" Je huyu kitaaluma ni wakili au?!
 
Hujatupa mrejesho wako kuhusu lile
Sakata la tigo au mlimalizana kibingwa

Ova
 
Je Wakili kuna tofaut ipi kat yule mwanasheria ambaye amefanya school of law na usajili wake ukasoma " ameruhusiwa kutoa viapo" Je huyu kitaaluma ni wakili au?!
kama yupo kwenye roll of advocates basi yy bado ni advocate .
 
Back
Top Bottom