Ijue vizuri Tahajudi (meditation)

Imani ndio tunda liletalo haki
Hiyo elimu inawahusu waumini,asante mleta mada kwa elimu
 
Nataka nifanye meditation sijui nan atanifundisha. Uzi mzuri sana
 
Meditation naitumiaga kupata usingizi haraka tu
 
Hivi kwanini Waswahili wametumia tamko "Tahajudi" kumaanisha ndiyo "Meditation" ?
 
Kuna Ile miziki yake ya meditation inapatikana you tube.
Uwa nikitaka kulala naweka nasikiliza.
Uwa naota ndoto nzuriii.
 
hapo wataalamu wa kutohoa ndo wangetuambia
Maneno muafaka kwa tamko "Meditation" yangefaa kuwa ni "Taamuli" au "Tafkiri" au "Tadaburi". Ila tamko "Tahajudi" wamelibabatiza maana kwani limekaa kisheria zaidi, yaani ni maalumu.
 
Napenda sana hii kitu nimesha wahi kufanya mara kadhaa zote hizo lakini najikuta natoka ndani ya mchezo kwamfano.....nimekaa tahajudi kwa dk30 kitendo cha kusikia sauti ya mtu au kitu flani kimeanguka au kuotwa najikuta mawazo yanatoka kule yanarudi kuwa kawaida
 
Asante mkuu kwa maarifa hayo,mi nilidhani tahajudi,wanaitumia waislamu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…