IjukaOmuka: Fatma Mwassa, asante kwa kuwakumbusha wana Kagera wakumbuke nyumbani, lakini ukurasa wa instagram wa mkoa hauna post tangu January 2024

IjukaOmuka: Fatma Mwassa, asante kwa kuwakumbusha wana Kagera wakumbuke nyumbani, lakini ukurasa wa instagram wa mkoa hauna post tangu January 2024

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nadhani Gerson Msigwa aanze kupima utendaji wa sektretariat za habari kwa kuangalia social media engagement. Na wakifanya hivyo, Makao Makuu ya Idara ya Habari (Maelezo) iwe inapewa taarifa

Imagine. Ukurasa rasmi wa ofisi ya mkuu wa mkoa (Instagram page) hauna habari yoyote iliyowekwa tangu January 2024. Hii haimtendei haki mkuu wa mkoa ambaye kafanya mengi sana kwa mwaka nzima. Haimtendei haki Rais Samia ambaye kapaisha bei ya kahawa na kuondoa tozo za hovyo. Hata hilo ofisa habari wa mkoa hakutaka kuliweka?

Nadhani sasa kila mkoa, halmashauri, Idara au taasisi, zifanyiwe mapitio na Wizard katika mitandao yao kama iko hai. Msigwa hawezi kuwa kila sehemu, unlike katika sehemu yao, fanya jukumu lako.

Watanzania wengi kwa sasa wanapata habari katika social media, kwa hiyo uwepo wa serikali mitandaoni ni muhimu sana, kwa kuwa itakuwa inaongea na wananchi.

Pengine fursa za uwekezaji zingekuwa posted hapa, walangira wangezidi kukumbuka kwao, pengine tamaduni, na mambo ya kijamii yangewatekenya. Au changamoto zingewavuta warudi kuzitatua

N. B.: mikoa yote wanakumbuka kwao isipokuwa hawa jamaa, imebidi serikali iwakumbushe warudi Kikuraijo, Kanyigo na Mushaha.

#SimbaNguvuMoja
Screenshot_20241222-073338.jpg
Screenshot_20241222-064420.jpg
 
Wana KuGIS, sasa mbona hamchangii mada ya mkoa wenu?
 
N. B.: mikoa yote wanakumbuka kwao isipokuwa hawa jamaa, imebidi serikali iwakumbushe warudi Kikuraijo, Kanyigo na Mushaha.
Badala ya kushauri umeleta vijembe na kusifia tu. Jambo usilolijua hilo tamasha sio mara ya kwanza kufanyika ila mwaka huu zimeingia na siasa.
Na matamasha haya yanafanyika sana kagera mwisho wa mwaka ngazi za kata kwa kuchangia maendeleo kwenye kata so usijitie ujuaji kwa kitu usichokijua. paka sasa vijijini wanakagera wameshafurika kutoka sehem mbalimbali kwa ajili ya siku kuu .
Lakini nikubaliane na wewe kwenye idara ya habari wamelala sana hata ukienda website ya mkoa huoni chochote cha maana.
 
Back
Top Bottom