vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Baada ya nyimbo na tambo zilizotolewa tokea siku ya upangaji wa droo hatimaye first leg imekamilika huku waliokuwa wanapigwa vijembe kwanzia siku ya kwanza ya upangwaji wa droo ya robo fainali wakijipapatua kwa kikosi chao hafifu kilichokosekana wazee wa kazi watatu ( Pacome, Yao na injinia Aucho) na hatimaye kutoka suluhu na bingwa wa AFL.
Ijumaa ijayo kuna nyuso zitakuwa zinaenda kwenye mechi ya pili kwa furaha na wengine kwa huzuni.
Mechi ya Mamelod dhidi ya Yanga itatangulia kuchezwa usiku kwa majira ya Tanzania itakuwa saa tatu usiku huku Simba akicheza siku hiyo hiyo saa tano usiku kwa saa za huku Tanzania. Ni wazi kuelekea mechi ya Simba, matokeo ya mechi ya Yanga itakuwa yanafahamika hatima labda itokee mechi iende extra time. Hivyo kama matokeo ya Yanga yatakuwa mazuri ni wazi mashabiki wa Simba watakuwa wanaangalia mechi katika mazingira magumu mno ila ikitokea kinyume chake basi mashabiki wa Simba watakuwa wapo comfortable kuangalia mechi yao kwasababu wameshajua mwenzao yaliyomkuta.
Ijumaa ni mtihani mzito kwa mashabiki wa timu za Kariakoo hakika ni kitendawili kizito.