IJUMAA & JUMAMOSI SPECIAL: Tuchezeni mchezo wa masomo kwa kumtag member aje akujibie maswali yako hapa.

You sir, are truly a bold person and more importantly a scholar sikutegemea jibu refu kwa kuwa wengi ninaokutana nao ktk "what banged " huwa hawakubali kutoa maelezo marefu wakiogopa kujicontradict ili kulinda heshima ya taaluma zao.

You are far too kind.

Mimi siamini sana katika kulinda heshima.

Ukilinda heshima sana utashindwa kujifunza. Utaogopa kusema unavyofikiri - hata kama unafikiri kwa makosa- ili kulinda heshima.

Kuna mtu alinikuta ma thread ya chit chat siku moja akanishangaa Kiranga umefikaje huku, nikamwambia huku mimi ni kwetu, sema niliondoka zamani nimerudi unanishangaa.

Ukiwa husemi sana, kwa kulinda heshima, halafu umekosea, utabaki na makosa yako watu hawajakukosoa.

Mimi nakubali kukosolewa, tena naweka insurance policy kabisa katika majibu yangu, kwamba nimeandika kwa elimu yangu ndogo ya kusoma vitabu vilivyoandikwa kwa the general public, wala sisemi kwamba ni mtaalamu mwenye formal training.

Na zaidi, nimejitahidi kuweka vitabu vyenyewe hapa, ili wengine nao kama wana wasaa, waweze kuvisoma, na kama kuna uelewa tofauti, tujadiliane.

Nimeweka kitabu cha Stephen Hawking, hiki kingine cha Steven Weinberg naona kina MB 20 hakitaweza kuwa uploaded hapa unfortunately.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…