Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
IJUMAA KUU; KIFO CHA YESU KRISTO MSALABANI (SIMBA WA YUDA)
Leo 14:25pm 15/04/2022
Basi tangu saa sita mchana Yesu alipowekwa msalabani na kugongelewa misumari pale Calvary,akapaza sauti yake akasema Eloi,Eloi lamasabakhthani(Mungu wangu,Mungu wangu mbona umeniacha?) mara giza likatanda, Yohane 19:28-30 Kisha, Yesu aliona kwamba yote yaliyokuwa yameandikwa na Manabii yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.” Hapo palikuwa na bakuli limejaa siki. Basi, wakachovya sifongo katika hiyo siki, wakaitia juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni. Yesu alipokwisha inywa hiyo siki, akasema, “Yametimia!” Kisha akainamisha kichwa, akakata roho.
Yohana 19:19-24
19Pilato aliandika ilani akaiweka juu ya msalaba. Nayo ilikuwa imeandikwa hivi: “Yesu Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi.” 20Wayahudi wengi waliisoma ilani hiyo, maana mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji. Tena ilani hiyo ilikuwa imeandikwa kwa Kiebrania, Kilatini, na Kigiriki. 21Basi, makuhani wakuu wakamwambia Pilato, “Usiandike: ‘Mfalme wa Wayahudi,’ ila ‘Yeye alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.’” 22Pilato akajibu, “Niliyoandika, nimeandika!”
23Askari walipokwisha msulubisha Yesu, walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bila mshono. 24 Basi, hao askari wakashauriana: “Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani.” Jambo hilo lilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo:
“Waligawana mavazi yangu,
na nguo yangu wakaipigia kura.”
-Kifo cha Yesu pale msalabani Calvary,yote yalikwisha.
Pale Calvary yote yalikwisha,tuliponywa magonjwa yetu pale Calvary kwa kifo cha Bwana Yesu,Malaria itakupata lakini haitakumaliza maana malaria ilishamalizwa pale msalabani,mtu wa ulimwengu malaria itammaliza,kifo cha mtu wa ulimwengu ni tofauti na kifo cha mwamini,kifo cha mwamini ni pumziko jema, it's home to glory,kwa mwamini hapa duniani ni kama tumekuja sokoni kununua bidhaa na bidhaa yenyewe ni kutenda yaliyo mema,baada ya kununua hiyo bidhaa utarudi nyumbani muda wako ukifika(Kifo) imeandikwa Hekima ya Solomoni 4:18 Watadhihaki kifo cha mtu mwema lakini Bwana atawacheka,Wao watakapokufa hawatazikwa kwa
heshima; na hata wafu watawapuuza milele,Isaya 57:1Mtu mwadilifu akifa, hakuna mtu anayejali; mtu mwema akifariki, hakuna mtu anayefikiri na kusema: “Mtu huyo mwema ameondolewa asipatwe na maafa.
Kwa kuwa sasa tumefanywa kuwa waadilifu kwa damu ya Kristo, ni dhahiri zaidi kwamba Yesu Kristo ametuokoa katika ghadhabu ya Mungu. Maana, tulipokuwa bado maadui wa Mungu baada ya Adam na Eva kutenda dhambi ya asili na kupewa adhabu ya kifo na adhabu nyingine lakini bado Mungu alitupatanisha naye kwa kifo cha Mwanae wa pekee ambae alimtuma aje duniani awe mwanadamu afe msalabani kwa dhambi za wanadamu, afanyike dhabihu na sadaka ya upatanisho wetu sisi wanadamu na Mungu, na kwa vile sasa tumepatanishwa na Mungu, ni dhahiri zaidi kwamba tumeokolewa kwa uhai wa Kristo, wala si hayo tu, ila tunafurahi pia katika Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametupatanisha na Mungu.
- Kwanini mtu mwema afe kifo cha kusikitisha,kutundikwa msalabani!?
Pamoja na umaarufu wake Yesu alikufa kifo cha aibu na mateso makali. Alipigwa mijeredi, akavuliwa nguo na kuvikwa taji la miba kichwani, na kisha kusulubiwa msalabani. Ni kitu gani kilichosababisha mtu huyu mwema na mnyenyekevu kuuawa kifo hicho cha mateso? Yeyote anayesoma habari ya kifo cha Yesu na kusulubishwa kwake katika injili anaweza kushangaa kwa nini mtu mwema hivi na asiye na makosa afe kifo cha kusikitisha hivyo.
Kwanini Yesu hakujitetea?Tunapata majibu kutoka kitabu cha “Isaya 53" – cha ajabu haya yaliandikwa miaka mia tano kabla ya kifo cha Yesu.
Kama wakristo tunaamini hili na mistari mingine katika Biblia inavyosema, kwamba haya yote yalikuwa ni mpango wa Mungu kwa wokovu wetu sisi Wanadamu tangu tulipoadhibiwa kwa gharika wakati wa Nuhu,na Mungu aliapa kutotuadhibu tena. Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu,Mungu alimtuma Bwana Yesu mwanae wa pekee ili afe na kuteseka ili sisi tusiteseke hivyo Alikuwa upatanisho wa dhambi zetu sisi wanadamu" Yesu Kristo alijeruhiwa kwa makosa yetu alisulubiwa kwa maovu yetu adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kupigwa kwake sisi tumepona sisi sote kama kondoo tulipotea kila mmoja wetu aligeukia njia yake mwenyewe na Mungu akaweka juu ya Yesu Kristo maovu yetu sisi sote nae akasulubiwa badala yetu”.
Isaya 53:5-6 Yesu ndiye kimbilio letu nyakati zetu,unapokimbizwa na Simba ndotoni,ita jina la Yesu,unapopita chini ya bonde la uvuli wa mauti,ita jina la Yesu,yeye aliyekufa msalabani, ametupatia jina lipitalo majina yote, Jina la Yesu ndio ngome yetu, Yesu ni mfariji,Yesu ni wokovu wetu, Yesu ni furaha yetu,ondoka katika ukiwa, Yesu ni mfariji, usikate tamaa kumbuka Bwana Yesu aliyashinda yote pale msalabani Calvary,uyapitiayo Bwana Yesu alishakushindia umebaki moshi tu nao utaisha,ni sawa na kuzima moto na kubaki moshi, Bwana Yesu aliuzima moto pale msalabani, Calvary.
Utazame msalaba,mtazame Bwana Yesu pale msalabani Calvary, yote yamemalizika, wagonjwa yameponywa, kuonewa kumemalizika, yote yalikwisha pale msalabani. Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza, wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia. Alidharauliwa na kukataliwa na watu, alikuwa mtu wa uchungu na huzuni. Alikuwa kama mtu kinyaa kwa watu; alidharauliwa na tukamwona si kitu. Hata hivyo alivumilia majonzi yetu, na kubeba huzuni zetu.
Sisi tulifikiri amepata adhabu, amepigwa na Mungu na kuteswa. Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu, aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu. Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai; kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Pengine nifafanue hapa, kuwa Yesu kama mwanadamu alikuwa tabia ya uadilifu, uaminifu na uchamungu wa kweli. Tofauti na watu wengi wa kipindi chake, Alikuwa tayari kutetea haki na kuulinda ukweli hata kwa gharama ya uhai wake. Kila ukweli ulipopindishwa, Yesu alisimama kidete kuunyoosha bila kujali nguvu, uwezo, na mamlaka waliyokuwa nayo wapindisha ukweli. Kwa nguvu na mamlaka ya kiroho aliyokuwanayo alitangaza habari njema za ufalme wa Mungu, huku akiwakemea makuhani, mafarisayo, na watu wengine wenye mamlaka waliokuwa wakitumia nafasi zao kuwadhulumu wanyonge.
Ni mchakato huo wa kuitetea KWELI uliomtia matatani. Kwa sababu hiyo Wayahudi wa kale waliona kifo chake ni cha KUJITAKIA na si dhabihu takatifu,nabii hakubariki kwao,lakini ilishatabiliwa miaka mingi iliyopita na ilipaswa kutimia, Marko 1:7-11
7 Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye uwezo kunizidi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. 8 Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawaba tiza kwa Roho Mtakatifu.”Yohane 1:29
Kesho yake, Yohane alimwona Yesu akimjia, akasema, “Huyu ndiye Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu! yalipotimia ndipo tulipopata neno SIMBA WA YUDA(THE LION OF JUDAH) likimaanisha mkombozi aliyezaliwa kutoka ukoo wa Yuda aliyekuwa mtoto wa nne wa Jacob, Mwanzo 35:23-26
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.