Ikifika 2030 hali haitakuwa nzuri kwa baadhi ya wanawake

Isaya 4:1
 
Research ndogo tu.....

Tafuta mwanamke aliefiwa na mme vs mwanaume aliefiwa na mke, majibu utayapata.
Wanaume wakifiwa na wake huoa tena na hutaona wakilalamika kunyanyaswa na jamii ila wanawake sasa utasikia mimi ni mama mjane nihurumieni mbona mnanifanyia hivyo ,na huunda vyama vingi ili watambulike
 
Hawa kwa wanachokiongea nimegundua hawana husiano lolote!!
Wanajisikia raha kubishana km hivi, unafikiri hawajui km zama zimebadilika? Wanajua fika.

Hapo unaweza kubishana na mtu kwa mkewe mpole na vyombo vya chakula anatoa yeye baada ya kula, ila hapa mdomo mrefu km chupa..!
Humu ni sehemu yao ya kutolea machungu 🀣🀣🀣

Wampige nani hao wamelegea 😹
 
Haha ukweli wanaujua ila wanajikaza tu humu mradi wasionekane wameshindwa hoja, we si unaona walivyopoteana hadi wanaanza kufukua comments za nyuma, siku zote ukiona mtu anahangaika na mtoa hoja ujue kashashindwa hoja huyo
Hawanaga hoja zaidi watakimbilia kukutukana malaya wakiona umewabinya mbupu ndio zao πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Na kuonea huruma ila ndio maisha uliyo ya chagua. Haya endelea na ligi.
Dooh angalia usije ukawa wewe ndio wa kuonewa huruma
Next time say no to divorce your husband when you get marriage again.
Just because you are a depressed divorcee, you think everyone out here is like you, pathetic!!
Ulosha

Ulishawahi kuona mwanaume anataka aombewe apate mume?,kinachofanya wanawake kuombewa kanisani wapate waume ni nini?
Ni kwa sababu anayeamua ndoa siyo mwanamke bali ni mwanaume maamuzi ya ndoa yapo mikononi mwa mwanaume, lakini cha ajabu pamoja na hayo maamuzi mliyonayo bado hamuoi wanawake wenye sifa zote mnazozitaka matokeo yake mnaishia kuoa wale mnaoona wana afadhali au mnaoa hao hao wenye tabia ambazo mnazilalamikia kila siku, mimi nilitegemea kwa vile ninyi hamhangaiki kutafuta maombi basi suala la ndoa kwenu litakuwa rahisi ila cha kushangaza na ninyi mnalalamika kwamba wanawake wanaringa hawataki kuolewa wakiwa na mabinti na hata wakikubali kuolewa hawana sifa za kuwa wake
 
Haya kwa hiyo una miaka is ishirini ya ndoa tokea 2019 ukijumlisha 5,unamiaka 25 au sio........?
 
Isaya 4:1
Soma sura yote acha kuokotezaokoteza
I'm not a depressed divorce mkuu,ninaye mke na watoto 3
Then next time say no to divorce your Wife when you get married again 😐😐
Haya kwa hiyo una miaka is ishirini ya ndoa tokea 2019 ukijumlisha 5,unamiaka 25 au sio........?
Hiyo inahusiana nini na mada tunayoijadili hapa nasisitiza tena naomba unioneshe uhusiano maana naona sasa umedhamiria nikuvue nguo, marital status yangu inahusiana nini na suala la wanawake wa sasa kutoona umuhimu wa ndoa hadi wakianza kuzeeka, je mimi kuolewa au kutokuolewa ndio kunabadili uhalisia uliopo kwenye jamii kwamba ndoa haina umuhimu kwa wanawake zaidi ya financial security kwani mahusiano yangu ndio kielelezo cha mahusiano yaliyopo kwenye jamii naomba unijibu haya maswali yote bila kona kona
 
Hawanaga hoja zaidi watakimbilia kukutukana malaya wakiona umewabinya mbupu ndio zao πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hawa nishawajulia huwa naenda nao sambamba, sijawahi kubishana na mwanaume jf kuhusu hizi mada halafu asikimbilie kuniita feminist au malaya na majina mengine ya hovyo, hiyo huwa ndio defensive mechanism yao ili wakudhoofishe uache kuwasema ila bahati mbaya hapa wamekutana na kisiki cha mpingo au chuma cha reli basi ndio yanazidi kujaa nyembe
 
Swadakta umesema kweli
 
Nimekuuliza ulicho post mwenyewe, kwa hiyo 2029 unafikisha miaka 30 ya ndoa? Au sio......
 
It's not about Personal attack. Ila hivi vitu vina uhusiano mkubwa.

You can imagine Uumpe keyboard Sista(nun) Au padri au sheikh au Mtu yoyote wa Dini au Mwanamke aliye katika Stable family yenye maelewano na amani Mpe Aandike kuhusu Jamii familia na Maadili ATAANDIKA NINI?

Then pia mpe keyboard Dadapoa ,, Mwanaume mzinzi mdada wa casino Mwanamke alienda kuvunja ndoa mahakamani Single Mother na mfano wa Watu hao Pia NAO WATAANDIKA NINI KUHUSU FAMILIA JAMII NA MAADILI??

Hata kama wote watakuwa na Level sawa Ya elimu lakini Mawazo yao Bila shaka hayawezi kuwa sawa kwenye Masuala hayo.

Kwa sababu utaandika na kufikili kama vile zilivyo tabia zako kwa sababu mwisho wa siku huweza kujenga hoja against Yourself. Lazima Hoja zao zitakuwa Upande wa maadili yako na Tabia zako na exposure yako.

Sasa mfano ni wewe unaedai una miaka 25 kwenye ndoa Ina maana una Miaka takribani 45 now huo ni umri kama sio unakaribia kuitwa bibi basi ni bibi tayari.

Lakini cha ajabu Unapost kwenye social media upo bar unakunywa tena katika rafudhi ya kusifia na kuonesha ni mdau mkubwa Hata kama huyo Unaetudanganya Mumeo Amekuruhusu sijui ulikuwa nae pamoja We get a picture of what kind of a family is that(japo tunajua yote hayo ni Uongo mtupu)

So Mtu kama wewe kuandika ujinga unaoandika It's something expected.

Kwaiyo hii ni kuonesha kwa jamii ya JF kuwa maneno hayo yanatoka kwa mtu wa aina gani. Kwa sababu kama Mdomo umeoza usitegemee utakuta jino zima.
 
Naomba unieleweshe hivi mwanamke anatafutaje ndoa? Mfano msichana yupo na anajitunza na hakuna mwanaume yeyote anayepropose ndoa, unataka huyo msichana afanye nini? Asitafute maisha yake asubiri tu Zemanda aje amuoe?
 
Si unaona sasa kumbe hamtaki tuongee uhalisia mnataka tuongelee mambo kulingana na maisha yetu, sasa hapo tunakuwa hatuongei ukweli bali tunaongelea mitazamo yetu, kitu ambacho hakitakiwi maana huo unakuwa ni unafiki na huko ni kujidanganya na kujilisha upepo tu

Mimi mara nyingi nasema kabisa huwa sijadili hizi mada kwa mitazamo yangu au kwa kuangalia maisha yangu binafsi, bali kwa kuangalia yale yanayoendelea kwenye jamii kwa sababu mitazamo yangu mimi inaweza isiwe uhalisia, na maisha yangu siyo kielelezo cha maisha yaliyopo kwenye jamiii

Sasa wewe unataka kusema kwamba mtu hawezi kuandika uhalisia kwa sababu huo uhalisia haumhusu yeye, aise mbona mna arguments za kipumbavu hivi kwahiyo kwa mfano serikali iliyopo madarakani ina shutuma za kuteka na kuua watu, je sitakiwi kuisema kwa sababu mimi nimepandishwa cheo mahali kupitia hiyo hiyo serikali

Je mimi kunufaika na utawala huo ndio kunabadili ukweli kwamba hiyo serikali inateka na inaua watu, kwahiyo mimi kuwa kwenye ndoa ndio kunanizuia kuongea ukweli ninaouona kwenye jamii kuhusu ndoa, yani kisa eti ndoa yangu mimi inaniendea vizuri basi natakiwa kuassume kwamba ndoa zote ziko vizuri, wakati uhalisia unaonekana wazi kabisa ndoa nyingi ni majanga na nyingi zinavunjika kila siku, yani mnataka nijadili maisha yangu binafsi katika issue sensitive zinazohusu jamii kwa ujumla

Kama wewe na wenzio mko hivyo basi mimi siko hivyo maana huo ni unafiki na ukifanya hivyo unakuwa hauisaidii jamii, bali unakuwa unayafumbia macho yanayoendelea kwenye jamii kisa wewe yako yanakuendea vizuri, mimi huwa niko straight and unprejudiced ninapojadili mada kama hizi, natumia facts na logic na siyo hisia au mihemko kama ninyi, kwahiyo msinipangie wala msinifundishe jinsi ya kujadili hizi mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…