Uchaguzi 2020 Ikifika muda wa kupiga kura Oktoba 2020, nakuomba urudi kituo ulichojiandikisha

Uchaguzi 2020 Ikifika muda wa kupiga kura Oktoba 2020, nakuomba urudi kituo ulichojiandikisha

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,013
Reaction score
1,183
Habari Tanzania

Nakuomba ewe mpiga kura ambaye uliyejiandikisha mwaka 2015 baada ya uchaguzi; kutokana na harakati za maisha ulihama eneo lako la kujiandikishia kupiga kura. Mwaka 2019 na 2020 hukuwezajiandikisha kabisa aidha kwa kukata tamaa au sababu zilizokuwa nje ya uwezo wako, tafadhali sana nakuomba ikifika muda wa kupiga kura Oktoba 2020 nakuomba urudi kituo ulichojiandikisha awali ili uweze kupiga kura yako kwa viongozi walio sahihi. Hii inakubalika.

Twende tukapige kura kwa watu sahihi, hakuna kukata tamaa tena.

#VijanaTanzaniaStandUp

Karibu.
 
Hii sio kwa watu sahihi! ila kwa Rais Sahihi, manake mie nimehamia Kilosa, nilijiandikisha Dar sasa Diwani wa kata yangu pale Dar na mie wapi na wapi? Hata hivyo hoja yako ni sahihi! Kwa Rais sahihi tumuunge mkono
 
Kilichotokea Mwanza kimenishtua,

Ile ni political shift, ngome ya CHADEMA imehama toka kaskazini kwenda Kanda ya ziwa. Si kwamba CDM imekataliwa kaskazini bali ushawishi wa CDM umeongezeka lake zone na kuizidi kaskazini.

Kitendo cha wananchi wa Mwanza kukwea daraja alilojenga Magufuli ili kumlaki Lissu ni sawa na mwanamwali anayetumia vitu alivyohongwa na danga ili kum-impress mwanaume anayempenda.
 
Kama una kitambulisho cha kupigia kura nadhani unaweza kuruhusiwa kupiga kura ya Rais nje ya eneo ulilojiandikisha.Kuna form maalum utapewa kituoni,utaijaza kisha utaruhusiwa kupiga kura,lakini hii ni kwa kura ya Rais tu sio mbunge na diwani.
 
Hii sio kwa watu sahihi! ila kwa Rais Sahihi, manake mie nimehamia Kilosa, nilijiandikisha Dar sasa Diwani wa kata yangu pale Dar na mie wapi na wapi? Hata hivyo hoja yako ni sahihi! Kwa Rais sahihi tumuunge mkono
Usiogope kikubwa wewe rudi muda ukifika kapige kura yako.
 
Mlihamsishana musiende kuboresha tarifa zenu kwenye daftari la mpiga kura. Hilo lilikuwa goli la kwanza!

Chadema mwaka huu mtafurahi tu wenyewe mbona
 
Mlihamsishana musiende kuboresha tarifa zenu kwenye daftari la mpiga kura. Hilo lilikuwa goli la kwanza!

Chadema mwaka huu mtafurahi tu wenyewe mbona
Kwenye huu uzi sijaona mtoa mada akizungumzia CDM, ila amewahamasisha watanzania wenzake kupiga kura kama ninavyoona TBC wakihamasisha.

Wewe unaiugua CDM tu kiasi kwamba kila anayehamasika kupiga kura unafikiri ni kura ya CDM! Ndio maana mnapenda kupita bila kupingwa.
 
Back
Top Bottom