Kwa kweli nitavunjika moyo na sidhani kama uhusiano wetu utakuwa kama ulivyokuwa zamani. Kwa mke kukufanyia hivyo ni kukuonesha dharau na kutokukuheshimu. Pia tendo lake hilo ni ishara tosha kuwa ni mtu mdhaifu na asiye na msimamo. Sitashangaa tendo hilo kuwa ndio mwanzo wa mfarakano wa ndoa yetu (kama kabla yake kila kitu kilikuwa poa). Na sijui nitalichukuliaje lakini ninachojua sitalifurahia hata kidogo. Nitahoji pia maadili yake, busara zake, akili pamoja na hekima zake kwani wanandoa wanaopendana na kusheshimiana hawawezi kamwe kufanyiana hivyo. Ndio maana moja ya kanuni zangu ktk mahusiano ya kimapenzi ni kumheshimu mwenzako popote pale:alipo na asipo.
Umeandika kwa hisia kali sana hapa kiongozi.
Itakuwa kawaida sana, infact mimi sizimii wanamuziki hata kidogo wala wacheza cinema nna appreciate kazi zao na vipaji vyao. Mimi napenda kuwa karibu na interlectualz kama akina Moyo alieyeandika kitabu kile cha madeni ya afrika akina Mandela tuta discuss kile kitabu chake cha mwendo mrefu kuelekea Uhuru/long walk to freedom. Au mtu kama Kiranga wa JF tuta discuss mambo ya poet kidogo na kuumiza vichwa katika kujibizana.
Mmh kweli huu ni mtihani...kama hii haivumiliki kama alivyosema mmoja wa wachangiaji hapo juu, utaielezeaje ile hali ya mama aliyepata ajali SA na akawa kwenye coma kwa muda mrefu, baada ya jitihada za mume wake kujaribu kumrudishia kumbukumbu kwa kuongea nae na kumkumbusha mambo mazuri waliyowahi kufanya pamoja kushindikana, madaktari wakashauri amsomee au amsikilizishe nyimbo anazopenda kusikiliza - akaanza kumpigia nyimbo za Michael Bolton...akaamka!
Annina
Nguli uliiona kwenye concert ya Fally Pupa nini maana kuna mdada huwa anaonekana alivyong'ang'ania kupanda jukwaani hadi nguo ikamchanika.
BTW: Kusema ukweli si kwenye concert tu bali popote mie nafikiri wapenzi tunatakiwa kuwa na staha japo kidogo hata kama mziki unaupenda kiasi gani au mwanamuziki unampenda kiasi gani si vema kufanya vitu ambavyo unajua vitamkwaza mwenzio. Maaana utakuta mwingine ametoka na Mr. kwenda mziki sasa kisa anaupenda basi atanyanyuka kwenda cheza na yeyote mradi kacheza- saa nyingine tunakaribisha vishawishi wenyewe.
ingekuwa mimi- pale alipozimia tu ningemrudisha nyumbani na kama angeng'ang'ania na kupanda jukwaani basi mara atakaposhuka jukwaani angenikuta nimeshatangulia nyumbani.
Nitajikaza kisabuni, nitacheza nae na wala sintomuuuliza ila dawa yake itakuwa inachemka😛ainkiller:Akirudi toka jukwaani utaendelea kutabasamu na kucheza naye tuu???
Gosh ni kweli usemayo Sio njema kabisa Nguli haileti picha nzuri katika mahusiano ..Ila siku akija Denzel Washington nitaomba muzee anipe chance nikamkumbatie kidogo tu .....sijui mapromota watamleta lini ?
Pole Nguli kama yamekukuta..
Wale wale wanaocheat wapenz wao yaani we unaona sawa mkeo kumegwa eti as long as wewe hujui!!!!!!!!!!!!!!!!Kiukwel ni hali ambayo haivumiliki na kama ukitaka kuvumilia jua wewe unaendekeza upuuzi.ukiwa na mpenzi wako popote pale hata kama ni kanisani ni lazima ajue nini umuhimu wako kwa wakati huo.inapotokea anashindwa kulielewa hilo jua hakueshimu,hii ni dharau bwana.mimi nasema hivi hata kama mkeo anamegwa nje "it's ok" tabu wewe muhusika kujua kwamba fulani anamega.kwani yeye kosa lake sio kumegwa kosa ni uzembe kugundulika anakuwa kaonyesha dharau.kama ingenitokea mm hata lifti ucku huo nisingempa.
Kwa kweli nitavunjika moyo na sidhani kama uhusiano wetu utakuwa kama ulivyokuwa zamani. Kwa mke kukufanyia hivyo ni kukuonesha dharau na kutokukuheshimu. Pia tendo lake hilo ni ishara tosha kuwa ni mtu mdhaifu na asiye na msimamo. Sitashangaa tendo hilo kuwa ndio mwanzo wa mfarakano wa ndoa yetu (kama kabla yake kila kitu kilikuwa poa). Na sijui nitalichukuliaje lakini ninachojua sitalifurahia hata kidogo. Nitahoji pia maadili yake, busara zake, akili pamoja na hekima zake kwani wanandoa wanaopendana na kusheshimiana hawawezi kamwe kufanyiana hivyo. Ndio maana moja ya kanuni zangu ktk mahusiano ya kimapenzi ni kumheshimu mwenzako popote pale:alipo na asipo.
Nimeandika kwa hisia kwa sababu ni kitu ambacho kwa kiasi flani nina relate nacho. Unajua ktk mahusiano ya kindoa ukimfanyia hivyo mwenzako ni unamwacha na kidonda ambacho kupona kwake kutakuwa kugumu sana. Anaweza akaliweka hilo moyoni mpaka siku yake ya kufa.
Na hakuna kitu kibaya kama kuwa na machungu ya muda mrefu hadi unakufa nayo. Ni mateso. Sasa kama kweli unampenda mwenzako kwa dhati sidhani kama utamfanyia hivyo. Ukimfanyia hivyo na akaumia basi mapenzi yenu will never be the same again. Every now and then he/she will be having flashbacks of what you did to him/her. It is injudicious to do that to your life partner for whom you proclaim to love.