Ikikutokea wewe Utafanyaje?

La Quica

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
1,009
Reaction score
2,315
Umemkopesha rafiki yako wa karibu Tshs 400,000 mwaka jana, lakini tokea wakati huo amekuwa mgumu kulipa deni hilo, kitu kilichochangia kudorora kwa urafiki wenu. Unamuomba akulipe basi walau Tshs 200,000 tu alafu umsamehe hiyo nyingine kwakuwa kwa sasa una ukata na matatizo na una uhitaji na hiyo hela.

Rafiki yako huyo anakuambia anaweza kukupatia tu Tshs 150,000 kwasababu ndio kiasi alichonacho. Unaona huna namna zaidi ya kukubali tu kiasi hicho. Unampatia details zako za benki na account namba akutumbukizie humo.


Kuamka asubuhi unatizama kwenye account yako unakuta kuna Tshs 1,500,000[emoji15][emoji15] Unatizama tena kwa makini huamini unachokiona lakini bado kweli ni Tshs 1,500,000.

Unatizama vizuri simu yako unakuta missed calls 53 na meseji 27 akiomba umrudishie Tshs 1,350,000 kwasababu alitaka kutuma tu Tshs 150,000 lakini akakosea akaongeza 0 moja.

Wewe ungechukua maamuzi gani?

1.Utamrudishia kiasi anachoomba urudishe Tshs 1,350,000?
2.Utachukua zile zako unazomdai Tshs 400,000?
3. Utachukua zote Tshs 1,500,000?
 
400,000/=Deni
72,000/=riba
90,000/=gharama za vocha kipindi chote ulichokuwa unafuatilia
510,000 chezea biko
28000/= chezea tatu mzuka.
390,000 Mrushie ambapo 10,000 itakuwa gharama za kumtumia!
 
400,000/=Deni
72,000/=riba
90,000/=gharama za vocha kipindi chote ulichokuwa unafuatilia
510,000 chezea biko
28000/= chezea tatu mzuka.
390,000 Mrushie ambapo 10,000 itakuwa gharama za kumtumia!
[emoji23][emoji23]duuuh mkuu

Alafu akikudai unamwambia umewekeza biko na tatu mzuka asubiri ushinde then utamrudishia pesa zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…