Elections 2015 Ikitokea bahati mbaya Magufuli akiingia Ikulu, atapata wakati mgumu kuliko Rais yeyote wa nchi hii

Elections 2015 Ikitokea bahati mbaya Magufuli akiingia Ikulu, atapata wakati mgumu kuliko Rais yeyote wa nchi hii

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,452
Reaction score
3,151
Kuna uwezekano mkubwa ikitokea Magufuli kwa bahati mbaya au CCM ikitumia umafia kuiba kura halafu ikaingia Ikulu atajikuta anapata wakati mgumu sana kuongoza.

1.Hana uwezo na busara za kiuongozi na hakubaliki na wana CCM wengi.

2. Ameonyesha udhaifu mkubwa katika ujuzi wa mambo hasa general knowledge na kwenye lugha ya kimataifa. Na tayari watu wengi wameshtuka na kumdharau.

3. Ameahidi mambo mengi ya ajabu ajabu ambayo hayateelezeki mfano kaahidi kujenga na kufufua viwanda nchi nzima. Na eti kuanzisha mahakama ya mafisadi kana kwamba hiyo mahakama haipo. Hili la viwanda kwa kiasi kikubwa ni la sekta binafsi na siyo la Serikali.

4. Kupiga pushup majukwaani kumempunguzia ila 'presidential demeanor' na kuonekana kama ze comedy yaani mtu ambaye si wa kumchukulia serious.

5. Upinzani utakuwa very strong na sioni kama ataweza kuhimili mashambulizi ya upinzani. Namwona Magufuli akiikimbia ofisi ya Ikulu kabla ya miaka miatano kama akichaguliwa. Kwa sababu ni mtu asiyekuwa na iwezo wa kuhimli pressure.

6. Uzoefu mdogo alionao kwenye system nzima ya nchi na uungwaji mkono mdogo alionao utamfanya kila mtu huko kwenye system aonekane mgeni. na hili litafanya kazi yake kuwa ngumu.

7. Kutokuaminiana baina ya wana CCM na manunguniko yaliyopo sasa mfano wazee kama kina Bilal, Pinda, Mwandosya, Ramadhani na wengine kutoswa kwa iabu na kuingiza tano bora watu wa hovyo kama kina Makamba na wale wanawake ambao hawakuwa na ushawishi wowote kwa jamii. Bilali ana kinyongo kikubwa! Magufuli atapata upinzani pia kutoka kwa wana CCM wenyewe.

8. Tabia ya Kikwete, ambaye ataendelea kuwa mwenyekti wa chama mpaka 2017,ya kutaka kuonekana bora zaidi kuliko wengine. Tumeona kina Rizt na Faiza Fox wakimfagilia sana kwamba yeye ni bora kuliko marais wote waliowahi kuiongoza Tanzania. Kikwete atakuwa kikwazo kikubwa kwa Magufuli kudeliver kwa sababu kutokana na uwezo mdogo wa Magufuli itabidi amtumie sana Kikwete kumuongoza cha kufanya.

9. Mwisho ni kwamba kama Magufuli akishinda kwa bahati mbaya au kwa kulazimisha tutakuwa na the worst president ever in katika Afrika.

Prof. Kitila laisema itabidi tutafute mahali pa kuficha aibu na nyuso zetu kwa maumivu ya miaka mitano ya hovyo.
 
Huu ni ukweli halisi ambao nimekuwa nikiufikiria sana juu ya huyu mgombea wa C.C.M.
KWA UJUMLA HAFAI!
 
Nakushauri anza kufunga mizigo,maana ndiye rais wa awamu ya tano Dr.John Pombe Joseph Magufuli

Atakuwa rais wa wanccm wala si wangu, na wala sitamheshim kamwe! Ila Magufuli hawezi kuwa rais wa tz. Akiwa nitahama nchi. Nasisitiza nitahama nchi
 
Wananchi wapenda maendeleo na mnaojitambua msiwe na hofu raisi ni mh.EDWARD N LOWASA.ahsanteni sana.
 
Tafadhali ccm huyu mtu wenu hana hadhi ya kuwarais wa nchi, hebu tuondoleeni vituko hivi. Tuwen serious!
 
Kwani slogans zenu hatuzijui jepeni hope raisi ni jp magufuli hayo mengine ni katika vijimbo ila magogoni hapa ni kazi tu
 
Bahati mbaya,we pumba kabisa,na tena unatakiwa urudishe hiyo elfu 7 uliyopewa
 
hebu jenga taswira magufuli awe anahutubia kikao cha umoja wa mataifa (UN).du!

Atakuwa ananukuu madaraja makubwa duniani,idadi ya samaki,na ataagiza marekani imalizie ujenzi wa madaraja kabla hajawanyanganya tenda
 
Huu ni ukweli halisi ambao nimekuwa nikiufikiria sana juu ya huyu mgombea wa C.C.M.
KWA UJUMLA HAFAI!

Kwahiyo unadhani anahitaji experience ya Miaka mingapi ili awe Rais!!? Huyo unayedhani anafaa ni hatari kuliko unavyomjua, utalia na kusaga meno. Magufuli ndiye Rais tunayemtarajia usitegemee atakuwa kama.... Magu sio jizi kama waleee
 
hebu jenga taswira magufuli awe anahutubia kikao cha umoja wa mataifa (UN).du!

Mm naona bora Magufuli maana atakuwa ameandikia hotuba kazi yake ni kuisoma tu
SHIDA KUU IKO KWA LOWASA AMBAYE HAWEZI KUSIMAMA ZAIDI YA DAKIKA KUMI SIJUI ATAKUWA ANALAZIMISHA AWEKEWE KITI!!!!! NA SHIDA NYINGINE NDANI YA UKUMBI HAWAINGII WAPAMBE SIJUI NANI ATAKUWA ANAMUINIA!!!!Maweeeeeee
 
Kama angekuwa ni wa ccm ndo kaanzisha uzi alalu kacoment mwenyewe ukawa mngemporomosea matu..... Ila kwakuwa ni nyie wenyee ahhh hakuna shida!!!
 
Back
Top Bottom