Elections 2015 Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Tuache
siasa, na tusemezane au tuambiane ukweli, iwapo CCM itashinda tena uchaguzi wa mwaka huu, ushindi huo wa CCM, jee utatokana na Watanzania kufanya informed decision kufuatia CCM kukubalika na Watanzania walio wengi kwa kuwaletea maendeleo chanya ya kuonekanika, majengo, miundo mbinu, mabarabara, madaraja, uhaulishaji fedha za ruzuku kwa kaya masikini etc, etc?!, au CCM itachaguliwa kwa mazoea tuu kufuatia ignorance ya Watanzania walio wengi, hawajui ni nini maendeleo halisi na maendeleo ya kweli, kiasi kwamba, serikali inapotimiza wajibu wake kwao hayo ndio maendeleo yenyewe kwao, hivyo ushindi wa CCM unaweza kabisa ukapatikana kutokana na ku take advantage ya hii ignorance yetu?!.

If you don't really kno
w what you really need, you'll take anything that you are given!, or what you get!, na kufuatia umasikini uliotopea wa Watanzania tulio wengi kiasi kwamba people do not know the real and true taste of development, then one can not miss what you never had!, tutajikuta CCM inashinda tena na tena kwa sababu za kijinga jinga kabisa! na wote watakaoshangilia ushindi kama huu, watakuwa wanashangilia ujinga tuu, kwa kujijua (wafaidika) au kwa kutojijua (wafaidikwa) kuwa ni wajinga?!.

Naomba kukiri, nimekua in
spired kuandika bandiko hili, kufuatia mchango wa mwana JF huyu, katika bandiko fulani humu baada ya mimi kusema kuwa Watanzania wa sasa, wenye uelewa, wanaelewa CCM imewafanyia nini, hivyo wameichoka CCM na mwezi October, wataipumzisha kwa amani kwa kufanya informed decision na sio tuu kujipigia kura kwa mazoea kama ilivyozoeleka!. Kujitokeza kwa wingi kusikiliza kampeni ni jambo moja, kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ni jambo jingine, lakini pia kuichagua tena CCM ni jambo jingine kabisa!. Naamini hakuna Mtanzania mwenye akili zake timamu, ambae ataelimishwa vya kutosha kuhusu CCM imelifanyia nini taifa hili, na bado akaichagua CCM!.

Hata hivyo, naweza kukubaliana na wewe, pia bado kuna uwezekano CCM, ikachaguliwa tena!. Kwenye mada yangu hii,
[h=3]Watanzania ni Ignorants au Tumelogwa?!. October 25, Tutafanya Informed Decision au Tutachagua Tuu?!.[/h] nilisema hivi


Hili lina
weza likajirudia mwezi October, hivyo sitashangaa iwapo CCM itachaguliwa tena, ila nitaamini kuwa kweli sisi Watanzania ni ma ignorant mpaka basi!, bado tuko gizani, na tumelala usingizi mnene wa ujinga na CCM inaendelea kufaidi mavuno ya uwekezaji wake mkubwa kwenye ignorance, na itaendelea kushinda na kushinda hadi pale Watanzania tutakapozinduka au tutakapoamka kwa kufanya uchaguzi kwa kuamua kwa kufanya informed decision na kuachana na hii ignoronce ya kuchagua kwa mazoea tuu!.

Na
watakia Jumatano Njema.

Pasco


 
Haitotokea tena,tumejua haki zetu,tumeona dharau na matusi yao kwetu,tumejitambua.Hatuipigii CCM kura hata wapige magoti mpaka ya chubuke.Tunawasubiri kwa hamu bila tamu.
 
Nimeweka bayana Kama Tanzania itachagua tena ccm Mimi siasa basi na wale ndugu zangu ambao kipato chao utata lakini kura zao Kwa ccm watafute wakuwapa pesa ya chai maana 2016 nakata misaada yote.
 
ccm imechoka

na sie tumeichoka

CCM inajua kuwa haitashinda uchaguzi huu .... ndio maana sasa hivi wanafikiria mabao ya mkonno
 


With just 7 days to come, hakuna kipya cha kuwaambia wanabodi, bali ni kukumbushana tuu, tulisema nini, nini kimefanyika, nini kinafanyika sasa, na nini kitafanyika hizo siku 7 zijazo, yaani tarehe 25 October, lets not let CCM to fool all the people all the times!.

Kiukweli kabisa, sioni jinsi yoyote ya CCM kushinda tena!, Chadema inakwenda kuchukua nchi kiulaini kabisa kama imeokota!, yaani CCM inakwenda kuanguka chini kiulani kabisa kama kumsukuma mlevi!.

Lakini ili hili litimie, ni lazima kila aliyejiandikisha, ajitokeze hiyo tarehe 25, aende kupiga kura na kumchagua Edward Lowassa!, unless it is very true that we are not only ignorants!, but rather stupids!, but are we real this
ignorants?!.

If "Together we can!", and "United we Stand", against this ignorance, then, "Victory is ascertain!"

Nawatakia Jumapili njema!.

Pasco
 
Mwisho wenu mafisadi, wakabi, wadini, wakanda na wavivu umewadia rasmi ..tunawatakia heri ili mkaione Tz ya Magufuli
 
With just two days to go, there is nothing new to say, yote yameishasemwa, sasa imebaki kukumbushana tuu, tulisema nini, nini kimefanyika, uchaguzi ndio keshokutwa Jumapili, nini kitafanyika siku hiyo, na baada ya hapo, tukutane tena wiki ijayo, au tupongezane, au tupeane pole!.

Nchi hii inaweza tuu kubadilishwa kwa watu wenye uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu, na kusimama wahesabiwe!.

I'm very proud kuwa ni mmoja wa wapiga kura hiyo Jumapili.

Haya shime kwa wote waliojiandikisha, tujitokeze kwa wingi, tuitumie haki yetu ya kidemokrasia kujichagulia viongozi wetu,

We have to choose our leaders and love our choices and live with or without!.

Pasco
 
Ccm inashinda kwa kuwa Wapunzani hawajui siasa wanajua Uhamasishaji, Ccm ingemsimamisha Lowassa kuna kundi kubwa tu la kina Sitta, Mwajyembe,Membe n.k nalo lingehama wakaenda Chadema + Nguvu ya Slaa pamoja na kete ya kupinga ufisadi wangesumbua sana sana na ccm isingethubutu kubeba neno ufisadi lakin kina Mbowe walitumia kigezo cha Umati wa wana ccm kwny udhamin wa Lowassa kuamini kuwa Lowassa ataipasua Ccm ni kosa kubwa sana la kimkakati lakin limesaidia kujifunza siku zijazo
 
Watanzania wengi wanajifariji kuwa wanampigia kura Magufuli kwa kuwa yeye ni mwadilifu bila kujua kuwa Magufuli yu ndani ya mfumo huo huo wa,CCM utawala miaka 50 plus kwa siasa hizi hizo za nitawafanyia,nitawaletea.Hivyo tunaona miaka mingine mitano inapita na hali inaendelea kuwa duni hasa kwa wwle ambao hawakupata fursa ndani ya huu mfumo ama kwa kutokujua,upeo mdogo wa kuchangamkia fursa labfa kwa sababu ya elimu ndogo au kutokuwa na exposure ya kutosha.
 
CCM itashinda kwa sababu upinzani umeshindwa kuonysha kuwa ni altenative nzuri; 1. demokrasia ndani ya vyama ni za magumashi, 2. wameshindwa kusimamia mambo yaliyowainua (eg kupiga vita ufisadi), 3. wamesimamisha mgombea ambaye kabla walikuwa wameshawaaminisha watu kuwa mbaya sana.
 
Watanzania wa sasa, wenye uelewa, wanaelewa CCM imewafanyia nini, hivyo wameichoka CCM na kesho, wataipumzisha kwa amani kwa kufanya informed decision na sio tuu kujipigia kura kwa mazoea kama ilivyozoeleka!.

N
awatakia Uchaguzi mwema.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…