Elections 2015 Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance?


Pasco Tanzania unayoidhania sio hiyo
 
wanabodi, mimi nimekubali matokeo kwa roho safi, kwa roho nyeupe!, na maadam niliishaiona possibility hii, sasa tujiandae kuufunga huu ukurasa, tuyaanze maisha mapya ya baada ya uchaguzi!.

Pasco
 
wanabodi, mimi nimekubali matokeo kwa roho safi, kwa roho nyeupe!, na maadam niliishaiona possibility hii, sasa tujiandae kuufunga huu ukurasa, tuyaanze maisha mapya ya baada ya uchaguzi!.

Pasco

Simple and Clear...... Usilaumu wala usitukane Watanzania ni upinzani wa kweli ulikosekana.

Huwezi leta mtu ulomponda miaka 8 umsafishe kwa miezi 2. tungekua ignorant zaidi kama tungemchagua huyooo tuloaminishwa ni mwizi na hao wanaotaka tumchague.

Ni kama uambiwe mtu ni muuaji kwa miaka 8 ukilala naye tu anakuua afu siku moja uambiwe ulale naye na hao hao walokua wanamsema will u agree?

You are grown up na wewe ni mwandishi wa muda mrefu sasa ukiahindwa ona hata fact ndogo ndogo kama hizo nadhani usiite Watz ni ignorant ita wachache ambao wameshindwa analyse mambo.
 
WATANZANIA wengi Hawajui uhusiano wa siasa na maisha Yao.

Siasa imekuwa kama tu ushabiki wa simba na Yanga.

Jamii yetu imebobea kwa Ujinga (Ignorance )
 
wanabodi, mimi nimekubali matokeo kwa roho safi, kwa roho nyeupe!, na maadam niliishaiona possibility hii, sasa tujiandae kuufunga huu ukurasa, tuyaanze maisha mapya ya baada ya uchaguzi!.

Pasco

Mkuu nakupongeza kwa kukubali matokeo Hongera sana kwa Ukomavu wako.

Pasco tunatakiwa kuwapongeza kwa dhati CDM na CUF kwa kazi kubwa ambayo wameifanya kwa muda wa miaka takriban 8 ya kupiga Vita UFISADI na kila aina ya UBADHIRIFU unaofanywa na watu walioko Serikalini.

Kila kazi njema inapaswa kupata UJIRA mzuri na Stahiki, CDM na CUF tayari wamelipwa UJIRA wao mzuri na Stahiki kwani Mtu waliyemuandama kwa miaka 8 ameshindwa kwa kazi ya mikono yao wenyewe.

ilikua lazima CDM na CUF wapoteze kama adhabu kwao kwani hata CCM kama wangemsimamisha Mtu wako wangepata adhabu hii,

Bahati mbaya sana kwamba walikutana watu 3 kwa maslahi yao Binafsi niwataje, MBOWE, SEIF na LOWASA kila mmoja akiwa na ndoto zake

MBOWE yeye alikua na malengo 4 kupata Urais, Wabunge wengi, Uwaziri Mkuu na KITITA cha RUZUKU pia kwake yeye na CDM Muungano si kipa umbele chao

SEIF yeye tangu mwanzo anaitaka Zanzibar kwa Udi na Uvumba bila kujali kitakachotokea Muungano kwake si Jambo la kipaumbele hata akamfukuza Mzee Mapalala ktk Chama

LOWASA yeye alikua anataka kutimiza tu NDOTO zake.

Pongezi kwao kwa KAMPENI ya miaka 8 Mwenyezi Mungu amewalipa
 
Hili ni swali niliulizaga ikitokea CCM kushinda, hatimaye sasa ni kweli CCM imeshinda, jee sasa kuna yeyote mwenye jibu la swali hili?

Pasco
 
Hili ni swali niliulizaga ikitokea CCM kushinda, hatimaye sasa ni kweli CCM imeshinda, jee sasa kuna yeyote mwenye jibu la swali hili?

Pasco

Ndiyo, mimi ninalo.

Nalo ni: Tanzania si kisiwa cha amani. Ni kisiwa cha wajinga na majuha.

Wajinga na majuha hawajui chochote. Kutokujua kwao chochote [yaani ujinga wao] ndo kumeifanya CCM iwe chama tawala kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi kuliko chama tawala kingine chochote kile barani Afrika.

Ni rahisi sana kumtawala mjinga na juha kuliko mwerevu.

Kati ya mtu taahira na mtu mwenye akili timamu, yupi ni rahisi zaidi kumdhibiti?
 

Nakubaliana na wewe kabisa, lakini ninawasifu mamilioni ya vijana waliochagua upande tofauti wanarudishwa nyuma na kukatishwa tamaa na mamilioni wengine walio katika ignorance ya hali ya juu.
 
Nani anakumbuka haya? 2005: Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya 2010: Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi 2015: Hapa Kazi Tu Wimbo maarufu? CCM ni ile ile. Sasa mnatarajia kipya kipi hicho watakacholeta? CCM ni ile ile! Msijiumize matumbo na vichwa vyenu!
 
Kama walivyofanya Bara, na Wazanzibari wameamua kwa kauli moja kuirudisha CCM.

Hongereni Wanzanzibari, tumeushuhudia uchaguzi, ulikuwa huru na wa haki, utulivu na amani,

Sasa uchaguzi umekwisha, tusonge mbele!.

Pasco
 
Nimeikuta hli mahli humu jf, nikaguswa nimeomba kulitumia bandiko hili kuboresha bandiko langu hili.

Pasco
 
Wale mnaendelea kumlalamikia rais Magufuli, muache kulalamika because Magufuli is our choice!, we have to live with the consequences of choices we have made!.

Pasco
 
Kabla hujawatukana Watanzania kwamba ni Ignorance!! Lazima ujitazame wewe unayetaka kuchaguliwa (mbadala) Je una Sifa? Kiasi Watanzania wanaweza kukuamini?
 
Kweli mayalla kutokana na uwekezaji wa CCM kwenye ujinga Leo tunaona kwa ujinga ule ule wanashangilia ujinga unaendelea.sizonje ata akifanya ujinga wajinga wanashangilia.akionea watu wanashangilia,kwa ujinga huu tunapoteza kizazi kijacho kitarithi ujinga.kwa ujinga huu hatuwezi kushindana kwenye soko la ajira EAC
 
Pasco hebu tumia japo kiduchu tu cha ufahamu wako ili ujibu hili swali. Mbona Chakubanga pamoja na ufahamu wake mdogo aliweza kulijibu swali hili kwa maneno machache sana? Kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki CCM ijiandae kukabidhi Ikulu. Wewe Mkuu kwanini upate kigugumizi na kuzunguka huku na kule? Hivi Chakubanga ana ufahamu mkubwa kuliko wewe Mkuu?

 
Uchaguzi wa Marudio wa Jimbo la Kinondoni na Siha ni Jumamosi hii. Sitashangaa kama majimbo yote mawili, CCM itashinda kwa kishindo!.
Hivi ndivyo Watanzania tulivyo.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…