Ikitokea umepata milioni 100, utaifanyia nini?

Enkulu

Member
Joined
Sep 29, 2022
Posts
20
Reaction score
76
Habari wana jamvi, poleni kwa harakati za hapa na pale. Kwa wanaoteswa na MAPENZI hii pole haiwahusu, wanawake wapo 31M wanaume 30M iweje uteswe na mtu mmoja?

Nirudi kwenye lengo husika la huu uzi

Niliwahi kushuhudia watu fulani wakizozana, mada ilikuwa "Ukipata 100M utaifanyia nini?" Mmoja akasema nitajenga nyumba nzuri nikae na familia yangu, mwengine akasema nitatafuta namna ya kuzungusha hio pesa. Mzozo ukaanzia hapo...

Wa kujenga nyumba anamuona mwenzake hana akili na wakuzungusha pesa anamuona mwenzake Mirembe day scholar. Kila mtu alikuwa na hoja zake na zina mashiko kwa kila mmoja.

Kwa kawaida mizozo/mijadala ya namna hii inafanywa na watu masikini pengine hawana hata 1M lakini ni mijadala mizuri sana. Kwani inajenga na inapanua ubongo namna ya kufikiria linapokuja swala la pesa. Binafsi nilijifunza mambo mengi sana siku hiyo.

Ni siku ambayo kwa kweli niliifurahia na nilipata kitu kipya. Ni siku ilijiyojenga misingi mipya linapokuja swala la fedha, ni siku iliyonipa mtazamo mpya na positive.

Vipi wewe ndugu yangu... "UKIPATA MILLIONI 100 LEO UTAIFANYIA NINI? UTAJENGA AU UTAIZUNGUSHA?"

Usijiulize hiyo 100M utaipataje.. mambo yatakuwa mengi[emoji23][emoji23] wewe anza kufikiria ushaipata kwa namna yoyote ile tayari upo nayo hapo. Tupe mawazo yako

KAMA UTAJENGA: utajenga nyumba ya gharama kiasi gani? Utajengea yote? Je kiwanja unacho au hiyo hiyo utanunulia kiwanja?

KAMA UTAIZUNGUSHA: Utaizungusha kwa misingi gani? Utaanzisha biashara ipi? Ni biashara moja au biashara mbali mbali? Utaitumia pesa yote kwenye biashara? Utaanzisha biashara mpya au unayo biashara utakayoiendeleza?

KARIBUNI
 
Mpaka nipate nikipata nitajua saivi sioti isije ika nipa stress za maisha bure na sina kama unazo nipatie ujione
 
Nanunua Ng'ombe
Nafungua Bucha
Nauza Maziwa
Nauza Nyama
Nauza Supu ya Kongolo na Mkia

Nanunua Kitimoto wa Kutosha
Natotolesha
Nafungua Bucha
Nauza nyama
Nawauzia na Ndizi 2

Piga pesa baada ya mwaka nmezalisha milioni 300 kutoka kwenye million 100

Hivyo ndio vipaumbele vyangu,
 
Nakodisha gesti mwaka mzima na kuweka order ya mbususu
 
Dah huwezi amini ukiwa hauna hela idea unakuwa nazo nyingi ili ukipata hela basi uoga unaingia. Mfano halisi mimi nina 50M+ Kwenye acc nataka niwekeze 20M+ ila mpaka sasa sina idea business ya kufanya.

Ila nashukuru kuna mdau kaniambia nikomae na biashara ya kiwanda kidogo cha mikate bakery.
 
Naenda salon najiweka sawa kila mahali, natoka hapo naingia gym after gym nafanya full body scub and full body massage without happy ending😜

naingia sauna na steam bath...
Nikitoka hapo naenda 5star Hotel...nqpiga simu maduka ya nguo kali na viatu waje waniletee hapo nifanye shopping nikiwa hapo hotelini....

Nikishaoga na kupendeza naenda kupata dinner pamoja na wine expensive kuliko zote inayopatikana hapo....

Narudi zangu room narelax kitandani nikiperuzi jf kuwasoma watu wenye shida zao nikiwafariji na kuwapa pole.

Kesho yake natafuta financial advisor aje tuongee....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…