Ikitokea Waafrica tukabadilishiwa Bara itakuwaje?

Ikitokea Waafrica tukabadilishiwa Bara itakuwaje?

0021

Senior Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
160
Reaction score
60
Habari wadau wngu wa J/intelijensia.

Awali ya yote ngoja niwape mkasa wa stori nilizozishuhudi kutoka kwa walevi wa pombe... tena pombe za kienyeji kule kijijini. "wapi wewe wabongo ndo tulivyo akili zetu ni fupi sana. Fanya mambo kizungu bwana, hawa waafrika unao waona wanakimbilia Ulaya ikatokea siku moja bara la Ulaya wakatuambia tubadilishane Mabara.

Waafrika waende Ulaya na Wazungu waje Afrika...yaani baada ya miaka 50 Waafrika wa Ulaya wataanza tena kuzamia tena kurudi Afrika kwa wazungu".mwisho wa kunukuu. Yule mlevi aliendelea kulopoka eti waafrika wakifika kule ulaya kwanza;-wataiba vyuma vya madaraja, barabarani, relini na kwenda kuuza kama vyuma chakavu.

Usafiri wa uma mfano Reli,bandari watabinafsisha na kuuziana viongozi na wafanya biashara.. Kabla hata wiki haijaisha nikakutana na makala moja kwenye gazeti la Mwanaspoti la Jumamosi tr.7 yenye kichwa cha habari 'Equatorial Guinea wametuwakilisha akili zetu Waafrika'...Makala hii ya Edo Kumwembe imeelezea yaleyale waliyosema wale walevi juu ya akili za kiafrika.

Wadau msaada wangu tuambizane ukweli nini ukweli wa fikra za kiafrika...tuchambue kwa kutumia theory mbalimbali.....mfano wengine huzani labda ni laana toka kwa Mungu wakitumia maandiko matakatifu hasa Biblia na wengine huzani ni ukoloni ndio ulidumaza uwezo wetu wa kufikiri.
 
Ambacho nashindwa kuelewa ni kwanini umetumia neno waafrika ....nadhani ungesema Tanzania. nchi kama South africa ,rwanda ,kenya ,Tunisia,misri etc..ni nchi ambazo zimeendelea../zinakua kwa kasi.

- Tanzania ndo kuna viongozi wanaouziana mali za umma.
- Tanzania ndo kuna watu kuliko kuhifadhi pesa zao nchini wameenda peleka uswis
- Ndo kuna watu wanaopasua reli/ kukata vibao vya barabarani ili wakauze kama chuma chakavu.
- Ndio kuna asilimia chache sana ya wananchi wazalendo wenye mapenzi na nchi yao...hivo wengi huona ufahari kwenda kwa wazungu ...hata kama wanaenda kua wafanyakazi wa ndani..

Hii sio miaka ya kuficha uchafu wa hii nchi kwenye vazi la Afrika, wenzetu wako serious na nchi zao..juzi kati umeskia museven kapiga marufuku madini kutolewa nje ya nchi..,aidha umeskia wahujumu uchumi wanachofanywa rwanda , nadhani unaona kenya inavoinyanyasa tanzania na Airport sasa hivi..as if sisi hatuwezi kujenga airport.

Lets try to be realistic and face things kama vilivyo... ukiwa smart enough ku analyze mambo utagundua..kama hii hali ikiendelea ...kama kisipofanyika kitu..tunaingia kwenye civil war soon / nimeshajiandaa kisaikolojia kabisa.
Na kama usalama wa taifa walikua incompitent..kundi la panya road likasimamisha shughuli za dar kwa masaa...sijui watawezaje kuzuia vita..
 
Back
Top Bottom