BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Wakati mwingine mwanadamu anapata taabu na shida kama maradhi. Maradhi kama ya saratani na mengineyo. Inatokea mpaka mwanadamu kwa maumivu ayapatayo na maradhi yake si yenye kutarajiwa kupona basi kwa taabu na shida anaamuwa kuomba bora afe. Hili pia limekatazwa kwenye uislamu. Lakini mtu akiwa katika hali kama hii ama hali ambazo zinafanana na hii na akiwa hana budi isipokuwa ni kufa na akawa anatamani bora afe, basi Mtume s.a.w ametufundisha maneno ambayo tunatakiwa kuyasema:
اللَّهُمَّ أَحْيِني ما آانَتِ الحَياةُ خَيْراً لي ، وتَوَفَّني إِذا آانَتِ الوفاةُ خَيراً لي
“ALLAHUMMA AHYINII MAA KANAT ALHAYAAT KHIRAN LII, WATAWAFFANII IDHAA KAANAT ALWAFAAT KHAIRAN LII”
(“Ewe Mwenyezi Mungu nipe uhai ikiwa uhai ni bora kwangu na unifishe ikiwa kifo ni bora kwangu”)
Maneno haya yamegawanyika katika vipengele vitatu na kila kipengele kimebeba ujumbe mzito sana. Hebu tuangalie kwa ufupi kabisa hadithi hii vipi tuielewe kwa kupitia vipengele hivi:-
Hadithi inatukataza kutamani mauti kwa madhara yaliyompata mtu kama maradhi, mabalaa, kufilisika ama kufiwa na mtu wa karibu. Haya yote yakikupata na ukiwa umekata tamaa kabisa badi Mtume anatukataza katu tusitamani kufa. Na ikiwa hakunabudi basi kuna dua yenye maneno ambayo tunatakiwa tuyazungumze kumwambia Allah, maneno haya yapo katika sehemu mbili:
Kwanza kumwambia Allah akupe uhai, yaani aendelee kukubakisha ukiwa hai, lakini tu kwa sharti kuwa ikiwa uhai una heri zaidi kwako. Hii inamaana unamwambia Allah akuuwe au akupe mauti ikiwa uhai utakuwa na madhara kwako.
Sehemu ya pili ni kumwambia Allah akufishe yaani akupe mauti ikiwa kufa ni bora zaidi kwako kuliko kuendelea kuwa hai.
Uislamu umekatiaza kuomba umauti, kujiuwa ama kuuwa. Leo hii kuna watu wanazidi kutumia dawa za kuuwa watu wakidai eti wanawapunguzia machungu ya maisha. Kuna madaktari wanathubutu hata kumaliza maisha ya wagonjwa kwa kigezo kuwa mgonjwa hatapona na akiendelea kuishi atakuwa kwenye maumivu tuu. Njia hizi zote haziruhusiwi kwenye uslamu.
BAKIIF ISLAMIC
Phone +255 755 351 262