Mfanyakazi akifariki kabla ya kustaafu:
Kitanyika kikao cha familia kuteua msimamizi wa mirathi.
Kama next of kin aliyeandikishwa na marehemu kwenye file atateuliwa tena na familia kusimamia mirathi, sawa.
Kama next of kin hatateuliwa na kikao hicho, basi watasaidizana na aliyependekezwa katika familia.
Kikao cha familia kitaandika muhtasari utakaopelekwa mahakamani kufungua shauri la mirathi.
Mirathi(mafao) ikishatoka,hugawiwa mahakamani kwa dependants waliopo kwenye file, yaani: mke/mume, watoto, yule mdogo ndiye mnufaika anayepatiwa kiwango kikubwa kuliko wenzake wote pamoja na wazazi kama watakuwa hai.