Ikiwa mkutano umeshaisha, nini sababu ya doria kuendelea?

Intricate

Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
56
Reaction score
162
Pick up za kichina zilizoanza kutumika na Polisi kipindi cha Mkutano wa Nishati bado zinazurula barabarani, hasa Pugu Road.
Tena zinaendeshwa kwa mwendo wa hatari zikienda na kurudi kupitia njia ya mwendokasi huku zikiwa na mapolisi wenye silaha.

Lile gari jeusi la kutisha nalo linapiga doria continuosly. Troops za wanajeshi wakifanya mazoezi ya kukimbia mabarabarani nazo zimeongezeka siku 2 hizi.

Kuna jambo wananchi tunapaswa kulijua? Maana ni kama vile tunapewa taharuki.
 
Wanadamu hatueleweki tunataka nini,.

Ushawahi kujiuliza bila majeshi imara nini hufuatia.

Umeamka salama,unaenda kwenye mishe zako unaanza kushangaa kwanini magari ya polisi yanaenda Kwa Kasi wakati huo hawakufuati wala kuhangaika na wewe na pia wanajeshi kufanya mazoezi ni utaratibu mzuri tu kwani mishe zao zinataka utimamu wa mwili na akili

Mkuu fanya shughuli zako ,Acha watu watimize wajibu wao
 
Labda Wanapasha pasha viungo waende kumfurumusha PAKA na wale Wahuni wake maana PAKA anajifanya jeuri sana
 
Ikiwa mpaka mtu ana notice speed za magari ya polisi ujue hana kazi ya kufanya huyo.
 
Dah Bongo shida sana. Unapewa ulinzi Bure kabisa bila hata mia kulipia but pia hutaki. Matukio ya kihalifu yakizidi utarudi hapa pia kulalamika kuhusu polisi kutotimiza majukum ipaswavyo.
Nb.
Jeshi kufanya mazoezi ni sehemu ya kazi za kawaida za kijeshi kuhakikisha utimamu wa mwili na akili
 
Mmh ila likitokea janga hapa hawa huwaoni kama hivi ,uNataka kusema hatuongeagi mfano mzuri janga la kariakoo
 
siku zote walikuwa wapi?
 
Wana ringishia gari jipya si unajua ushamba mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…