Ikiwa sharti kuu la kula kiapo ni kuilinda na kuihifadhi Katiba ya nchi, ni kwanini viongozi hao baada ya kula viapo hivyo, wanaisigina Katiba hiyo?

Ikiwa sharti kuu la kula kiapo ni kuilinda na kuihifadhi Katiba ya nchi, ni kwanini viongozi hao baada ya kula viapo hivyo, wanaisigina Katiba hiyo?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tumekuwa tukishuhudia kila kiongozi kabla ya kukabidhiwa madaraka, ni lazima kwanza aape na katika kiapo hicho, sharti kuu ni kuilinda na kuiheshimu Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama ya nchi yetu

Sasa ni kwanini baadhi ya viongozi Mara tu wanapoanza kutumikia nyadhifa hizo wanaipuuza Katiba ya nchi na kuiona kama takataka?

Ifahamike kuwa Katiba ya nchi ni lazima uitekeleze na kuipuuza Katiba hiyo ni sawasawa na uhaini na huyo kiongozi anastahili kushitakiwa.

Sasa ninachojiliuliza ni kwa nini baadhi ya viongozi wakubwa ambao nao wameapa kuitii na kuiheshimu Katiba hiyo wakiipuuza na kuiona kama takataka na kuisigina Katiba hiyo?

Mfano dhahiri ni kwa Spika wa Bunge letu la Jamhuri, Spika Ndugai, ambaye anajua kuwa huwezi kuwa mbunge kama umevuliwa uanachama wako na chama kilichokudhamini ubunge wako.

Spika Ndugai amesema hadharani kuwa atawalinda kwa nguvu zote wabunge wa viti maalum wa Chadema, ambao chama chao cha Chadema kimeutangazia Umma kuwa kimewavua uanachama wao.

Sasa kama Spika anaonyesha mfano mbaya kiasi hicho, wa kuamua kuisigina Katiba ya nchi kadri atakavyo, hivi huyu Spika ana nia ya kulitumbukiza Taifa hili shimoni na tusiweze tena kujikwamua?
 
Wanasiasa bana.
EolbH7_WMAYAwWW.jpg
 
Tumekuwa tukishuhudia kila kiongozi kabla ya kukabidhiwa madaraka, ni lazima kwanza aape na katika kiapo hicho, sharti kuu ni kuilinda na kuiheshimu Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama ya nchi yetu...
Kumbuka katiba Ina mpa ulinzi pindi akifanya makosa latina utekelezaji wa majukumu na baada.
 
Ni kweli kingozi asiyetaka kuitii Katiba ya nchi ni sawasawa na mhaini na hatakiwi kuendelea kutumika katika wadhifa huo.

Kwa maana hiyo Spika Ndugai amepoteza sifa za kuendelea kuwa Spika wa Bunge kwa kuisigina Katiba hiyo
 
Mfumo dhaifu ndio shida ya nchi yetu
Wangekuwa wanashitakiwa na kuhukumiwa kwa haki, wasingethubu kutufanya mazombi
 
Mfumo dhaifu ndio shida ya nchi yetu
Wangekuwa wanashitakiwa na kuhukumiwa kwa haki, wasingethubu kutufanya mazombi
Mfumo dhaifu ndio shida ya nchi yetu
Wangekuwa wanashitakiwa na kuhukumiwa kwa haki, wasingethubu kutufanya mazombi
Kweli kabisa.

Wangeburuzwa mahakamani wasingefanya mzaha na hiyo Katiba yetu
 
Katika upumbavu na ushetani unaofanywa na kina ndugai jiwe na maraisi waliopita mbele ya jamaii na unaogharimu mamilioni ya fedha za walipa Kodi kwa kukufuru ni KUAPA kuilinda katiba. Kama katiba ingekuwa mtu aliye hai katiba yetu ingekuwa ilikufa iko makaburini au imeoza nzi wanaila tu.
 
Yani ufipa inamaani kwenu hakuna lililojema kwenu??🤔🤔
 
Yani ufipa inamaani kwenu hakuna lililojema kwenu??🤔🤔
Wewe unataka tukiona Katiba inavunjwa tung'aze macho tu huku tukiwa tunaangalia tu bila kukemea?
 
Back
Top Bottom